Kama kweli aliyafanya hayo basi huyo alikua "super president", sema sasa binafsi sina namna ya kuyahakiki hayo ila kutegemea nyuzi zinazoanzishwa na Watanzania wakimjadili alivyokua rais wenu huyo, wanayoyaandika kama ni ya kweli atakua aliikwamisha sana hiyo nchi, hebu soma hii analysis ya huyu
Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza
Nimesoma maneno yake yote. Yaliyojiri ni haya:-
1. Haja-acknowledge source yoyote ya takwimu zake, amezikoseshea uhalali (hajazitendea haki kwa sababu siyo zake na wala yeye siyo mtafiti aliyesajiliwa), kwenye media haziwezi kuchapwa, kwenye social media zinagombaniwa kwa sababu huko posts hazihaririwi, kazi ya kuhariri iko kwa mtoa post mwenyewe, sasa hapa unategemea justice kweli kwa anayechambuliwa?
2. Hajatueleza kisayansi ni vipi kama nchi Tz tumeingia Uchumi wa Pato la Kati la Chini? ikiwa uchumi huo wetu ulikuwa taabani/ulikuwa unaborongwa kama anavyosisitiza? Na kama tumeingia ngazi hiyo ya Uchumi wa Pato la Kati la Chini tukiwa na uchumi-mahtuti kama anavyotuaminisha je, ni kwa nini nchi zenye chumi-mahtuti na rekodi mbovu za demokrasia na haki za binadamu kama Somalia, Sudan, Rwanda, Burundi, DR Congo, Zimbabwe, Mali, Afrika ya Kati, Djibout, Eritrea, Burkina Faso, South Sudan, Darfur, Uganda nk hazijaingizwa kwenye ngazi ya Uchumi wa Pato la Kati? Je, Magufuli alihonga Breton Woods (WB na IMF) kutupandisha hadhi? Je, kisayansi-ya-uchumi, kiuchumi-siasa na kimaadili inawezekana kuhonga Breton Woods?
3. Kuingiza nchi kwenye Uchumi wa Pato la Kati siyo dhamana ya BoT, AU, EAC, SADC nk ni dhamana na jukumu la taasisi za Breton Wood. Mojawapo ya vigezo vikuu vya taasisi hizi katika kuithibati chumi za dunia ni hali ya kisiasa kwenye nchi husika (demokrasia na haki za binadamu) ambazo kama hazijakaa vizuri basi usitegemee chochote toka kwa taasisi hizi za Kibeberu (siyo za Kijamaa wala Kikomunisti).
Katika muktadha na mantiki ya hoja hii no. 3, Tz haikustahili kuingizwa kwenye ngazi hiyo ya uchumi kwa sababu baadhi ya watu wake akiwemo mchambuzi huyo kupitia vikundi-maslahi vyao walichagiza kwamba Magufuli anakandamiza demokrasia na haki za binadamu (sikanushi wala sikubali hii kwa sababu sina ushahidi wa kisayansi wa kutosheleza kukana au kukubali), sasa hapa mnafiki ni yupi? Mchambuzi? Taasisi za Breton Wood? CCM? Serikali? Bunge? Mahakama?
4. Amelinganisha uchumi wa JK na wa JPM, sawa kufanya hivyo kwa sababu huwezi kubaini kizuri au kibovu bila kufanya ulinganifu, sasa je, Mtz wa daraja la tatu la maisha; wa kipindi cha JK na JPM wana tofauti gani hasa hata ukiwapima kwa macho tu? Maskini wa wakati wa JK na maskini wa wakati wa JPM siyo kwamba wote tunaimbiwa ngonjera kwamba wanaishi chini ya dola moja ya Marekani kwa siku? Mara nyingi chambuzi zetu kwa kaliba zetu, kwa mrengo wetu na kwa malengo yetu huwa hayana substance.
-Tajiri akichelewa kulala riziki ya maskini ipo, akichelewa kuamka riziki ya maskini haipo, tajiri hatakiwi kulala-