Raila au Uhuru Ikulu Leo ?

Raila au Uhuru Ikulu Leo ?

Status
Not open for further replies.
Binafsi nataka raila odinga asiwe rais anaongea kwa dharau sana, lakini ukiivemuona uhuru na rutto wanaongea wakiwa active sana wanatia hamasa
 
Uhuru hakamatiki Urais


Wakati Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ikiwataka wananchi wa Kenya kuwa na subira wakati ikiendelea kukusanya na kuhesabu kura, mgombea wa Jubilee, Uhuru Kenyata anaendelea kuongoza kwa kura dhidi ya mgombea wa Muungano wa Cord, Raila Odinga.

Tangu kura zianze kuhesabiwa juzi jioni, Kenyatta amekuwa akiongoza wagombea wengine wa urais katika uchaguzi huo.

Tamko la Mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan jana asubuhi lilitokana na malalamiko yaliyoanza kutolewa na wananchi na vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo kuwa matokeo yanacheleweshwa.

IEBC ilikuwa imeahidi kutangaza matokeo ya urais ndani ya saa 48 baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura juzi saa 11 jioni hakukuwa na matokeo hayo.

Kwa siku nzima jana, matokeo ya awali yaliendelea kutolewa lakini kwa kasi ndogo ikilinganishwa na juzi, huku mgombea urais kupitia Jubilee, Uhuru Kenyatta akiongoza akiwa na kura 2,735,353 (53.49%) dhidi ya Raila Odinga wa Cord aliyekuwa na 2,145,721 (41.96%) hadi kufikia saa 1 jioni jana.

Hassan alisema matokeo hayo yalichelewa kutokana na matatizo yaliyojitokeza ya baadhi ya mashine za utambuzi wa wapigakura kukwama na kusuasua kwa mtandao (network down) juzi usiku.

Aliwataka wananchi kuwa watulivu na wavumilivu wakati wakiendelea kupokea matokeo ya awali, kwa kuwa matokeo rasmi yangesubiri wasimamizi kuwasili Nairobi kutoka mikoani, wakiwa na karatasi rasmi za matokeo kwa ajili ya kulinganisha, hatua ambayo alisema isingewezekana ndani ya saa 48.

Alisema wasimamizi kutoka katika majimbo 290 na kaunti 47 walikuwa safarini kutoka mikoani kwenda Nairobi, hatua ambayo ingesaidia tangazo rasmi la matokeo.

“Tunatarajia wafike mchana wa leo (jana),” alisema Hassan alipozungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kujumlishia kura, Bomas.

Hassan alitupilia mbali madai ya Muungano wa Cord kuwa matokeo hayo yanacheleweshwa akisema hayana msingi kwa kuwa sheria ya uchaguzi inaruhusu matokeo kutangazwa ndani ya siku saba, hivyo alikuwa bado na siku sita mkononi kisheria.

Alitumia nafasi hiyo kuzima furaha ya baadhi ya watu: “Hadi sasa tumepata matokeo kutoka vituo 23,000 kwa nchi nzima.

Hakuna anayestahili kushangilia, hakuna anayestahili kulalamika. Huu siyo muda wa kushangilia wala kuhuzunika,” alisema Hassan. Katika uchaguzi huo kulikuwa na vituo 31,981.
Alisema hawawezi kurudia makosa yaliyofanywa na iliyokuwa Tume ya Uchaguzi (ECK), mwaka 2007 yaliyoharibu uchaguzi na kusababisha machafuko.
“Tuko makini sana na suala hilo na ndiyo maana tumetumia gharama kubwa kuandaa mtandao huu. Hatuna nia ya kubadili matokeo yaliyotoka vituoni wala maeneo ya kuhesabia kura. Kila kura iliyopigwa itahesabiwa na itatangazwa,” alisema.
Polisi na msimamizi
Msimamizi mmoja wa uchaguzi aliripotiwa kuuawa kwa bahati mbaya na polisi juzi usiku wakati wakisafirisha masanduku ya kura kwenye kituo cha kujumlishia kura cha Kangema, Muranga, Mkoa wa Kati.

Askari na msimamizi huyo walikuwa wanasafiri kwenye gari moja, ndipo bunduki ikamponyoka na risasi kufyatuka ikielekea kwa msimamizi huyo.

Mkuu wa Kituo cha Polisi Muranga Mashariki, Chris Mushimba alisema aliyeuawa alikuwa Msimamizi wa Kituo cha Ichichi na uchunguzi wa awali unaeleza ilikuwa ni bahati mbaya.
Waangalizi wapongeza
Timu za waangalizi wa uchaguzi wa kutoka Afrika Mashariki (EAC), Comesa na IGAD wameipongeza IEBC kwa kuendesha uchaguzi huru na haki kwa kufuata kanuni sheria na taratibu, licha ya kasoro za kiufundi zilizojitokeza.

Akisoma taarifa ya awali jana, Mwakilishi wa EAC, Abdulrahman Kinana alisema kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa, wana imani kuwa matokeo yatakuwa ndiyo matakwa halisi ya Wakenya.

Kinana ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CCM, aliwataka wadau wa uchaguzi, Serikali na wengine, kuendelea kulinda amani, licha ya changamoto za kiusalama zilizojitokeza katika maeneo ya Garisa, Kilifi, Mombasa na Wajir.

Alivipongeza vyombo vya habari kwa kutimiza wajibu wao kuelimisha umma na kuwa makini dhidi ya habari ambazo zingeweza kuhatarisha amani.

Kwa upande wa polisi, alisema walifanya kazi yao vizuri, hawakutisha watu na walionekana wakiwasaidia wapigakura.

Alishauri IEBC kuendelea kupitia daftari la wapigakura mara kwa mara, msajili wa vyama vya siasa apewe mamlaka kisheria kusimamia chaguzi za awali ndani ya vyama na elimu ya uraia itolewe ili kupunguza matukio kadhaa yaliyojitokeza kama vile kuharibu kura.


source: Mwananchi
 
Kwa ufupi sana maana sina muda tupo na heka heka, kwa haraka sana kinachotokea Kenya

ndio kilichojili Tanzania mwaka 2010 uchaguzi mkuu. Jiulize Uhuru alikwenda Ikulu Ya Magogoni

kufanya nini? Nae Ruto alikuja bongo kufanya nini? Pia Emilion M. Kibaki nae alikuja pale magogoni

tukazuga anazindua barabara, ayo yote ni kwanin, Je yale ya Kilavu mnayaona? Mnamo jumapili usiku

kuna ndege ziliingia kenya usiku? Jiulize zina nin na akina nani?

Taarifa ni kuwa sasa wasimamizi wataambiwa waje na matokeo makao makuu maana mtambo au mfumo

wa kieletroniki umekwama, na apo ndio maumiv uanza taaratibu kwa chaguo la wananchi.
 
Wananchi wa Kenya leo wanapiga kura kuwachagua viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza baada ya kupata Katiba Mpya, ambao unawapambanisha vikali watoto wa waasisi wa taifa hilo ambao sasa ni marehemu.
Uchaguzi wa leo unaelezwa kuwa na kinyang’anyiro kikali ambacho hakijawahi kushuhudiwa baina ya wagombea wawili wa urais, Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee na Raila Odinga wa Cord.
Uhuru ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta, wakati Raila ni mtoto wa aliyekuwa Makamu wa Kenyatta, Jaramog Oginga Odinga.

MAMBO MUHIMU:
Kinachofuta; Iwapo mgombea Rais atafikisha zaidi ya nusu ya kura kwauchaguzi waleo, atatangazwa mshindi.
Ikishindikana, unafanyika uchaguzi wa marudio baina ya wagombea wawili wa kwanza, kati yao atakayepata kura nyingi atatawazwa kukalia Ikulu ya Kenya.
Walikotoka; Anayechaguliwa leo Rais wa nne wa Kenya. Marais watatu waliotangulia ni Jomo Kenyatta, Rais wa kwanza, Daniel Arap Moi, rais wa pili, na anayeondoka, Mwai Kibaki.
Wagombea wawili wanao pambana vikali; Uhuru Kenyatta na Raila Odinga – Ni watoto wa waasisi wa Taifa la Kenya, wakati Uhuru ni motto wa rais wa kwanza, na Odinga ni motto wa aliyekuwa Makamu wa rais.
Je ni nani atakayeingia ikulu leo? (……..) “chagua jibu moja tu, (a) au (b)
(a) Raila Odinga
(b) Uhuru Kenyatta


Uhuru Kenyatt, Age 52,
Education: he went to st. Mary 's in Nairobi, and then studied political Science at Amherst College.

And
Raila Odinga, Age 65,
education: Technical University, Magdeburg in Germany. In 1970, he graduate with a degree in Mechanical Engineering.
 
Kuna halufu ya u.s.hu.z.i Kenya na kitanuka tu, kila mwananchi anapenda aone haki ikitendeka sasa huu uhuni wa mitambo au mtandao upo low utaamsha hisia hasi kwa wananchi matokeo yake hayatokuwa mazuri.
 
Kenya awaits
election
results:
" Reuters NAIROBI" Kenyan
authorities hope to
deliver the final
outcome of a
presidential vote on
Wednesday, after partial results showed
a lead for a politician
wanted in the Hague
over tribal violence at
the last election five
years ago. Counting since
Monday's vote has
been slow, and a new
electronic voter
system has been
plagued by hitches, leading to complaints
by political parties and
anxiety among voters
fearful that a flawed
process could lead to
another violent dispute. Deputy Prime Minister
Uhuru Kenyatta, 51,
has kept an early lead
since results started
trickling in after polls
closed on Monday, but some strongholds for
his rival Prime
Minister Raila Odinga,
68, have yet to declare
their results. After problems with
the electronic system,
the electoral
commission said it
would rely instead on
results being delivered manually to a national
tallying centre
overnight. It said it
hoped to declare the
winner on Wednesday
and urged Kenyans to remain calm. Results released on
Tuesday with half of
ballots counted
showed Kenyatta, son
of Kenya's
independence leader and one of Africa's
richest men, leading
with 53 percent,
against 42 percent for
veteran politician
Odinga. Kenyatta and his
deputy presidential
running mate are both
wanted in the Hague
on charges of
unleashing death squads after the last
vote in 2007, which
both men deny. The last election saw
some 1,200 people
killed in ethnic
violence after
outgoing president
Mwai Kibaki was declared the victor
over Odinga. This
time, Monday's vote
saw at least 15 people
killed in pockets of
violence but no repeat so far of unrest on
such a large scale. If neither major
candidate wins 50
percent of the vote,
Kenyatta and Odinga
would have to face
each other in a second round run-off,
pencilled in for next
month if necessary. "We can confirm that
our returning officers
are expected to bring
the physical results at
any time now, which
will lead to the final results. What matters
here is the final result
and they are coming
in," Ahmed Issack
Hassan, chairman of
the Independent Electoral and
Boundaries
commission, told a
news conference on
Tuesday evening. Hassan repeated that
despite the hitches, he
expected the vote to
be fair and credible. "We therefore
continue to appeal for
patience from the
public," he said earlier
in the day. "Nobody
should celebrate, nobody should
complain." To try to prevent a
repeat of the
contested outcome
that sparked the
violence after the
December 2007 vote, the new, broadly-
respected election
commission is using
more technology to
prevent fraud, speed
up counting and increase transparency.
But the new system
has come up short of
its expectations
 
Update
=======
Mitambo yaharibika uchaguzi Kenya
Mtandao wa elektroniki wa uwasilishaji na utangazaji wa matokeo ya kura za wagombea urais Kenya umeshindwa kufanya kazi juzi na jana na kuzusha wasiwasi miongoni mwa wananchi.

Mtandao huo ulianza kusuasua tangu juzi mchana na hadi jana mchana ni kura chache tu zilizokuwa zimeongezeka, huku Uhuru Kenyatta wa Jubilee akiendelea kuongoza kwa asilimia 53 dhidi ya Raila Odinga aliyekuwa na asilimia 42 ya kura halali.


Hali hiyo imezua hofu miongoni mwa wananchi, wengi wakianza kuhoji iweje matokeo hayo yacheleweshwe ilhali Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ilikuwa imeahidi kuwa yangetolewa ndani ya saa 48 baada ya vituo kufungwa Jumatatu.


Mwenyekiti wa IEBC alisema mfumo huo wa kielektroniki umekwama na kwamba hadi jana walikuwa wanahesabu kwa njia ya kawaida baada ya wasimamizi wa uchaguzi kurejea Nairobi kutoka mikoani.


Pia tume hiyo ilikuwa na mpango wa kuingiza kura zilizoharibika kwenye hesabu ya asilimia za wagombea kadri sheria inavyotaka kwa kuwa nazo ni kura zilizopigwa, hatua ambayo inaelezwa itaathiri matokeo na kusababisha uchaguzi wa marudio.


Katika matokeo ya awali yaliyokwishatangazwa, kura 320, 000 zilizoharibika hazikuwa zinajumlishwa.


Hatua hiyo imewagawa wagombea hao wawili wanaochuana vikali, Uhuru na Odinga. Wakati uongozi wa Muungano wa Cord umeitaka IEBC kuacha kuonyesha matokeo ambayo hayahusishi kura zilizoharibika, Mgombea Mwenza wa Uhuru, William Ruto alipinga kitendo hicho, akisema tume ilikuwa inataka kuvuruga uchaguzi.


Vyama vyote viwili, Jubilee na Cord viliwataka mashabiki wake kuwa watulivu kusubiri matokeo hayo.


Vigogo waanguka ubunge
Katika matokeo ya ubunge, baadhi ya wanasiasa maarufu, wakiwamo mawaziri, naibu mawaziri na waliokuwa wabunge wameanguka vibaya.
Mawaziri walioanguka ni Henry Kosgey wa Maendeleo ya Viwanda, Sally Kosgei (Kilimo), Charity Ngilu (Maji) na Amos Kimunya (Usafirishaji).


Naibu Mawaziri walioangushwa ni Ndiritu Mureithi, Mwangi Kiunjuri, mbunge wa zamani wa Naivasha, John Mututho na Kiema Kilonzo aliyekuwa anagombea ugavana wa Kitui.


Kosgey ambaye pia ni Mwenyekiti wa ODM alianguka katika nafasi ya useneta baada ya kiti hicho kunyakuliwa na Stephen Sang wa United Republican Party (URP).


Source: Mwananchi
 
….KENYA BALLOT 2013 – Presidential Results @ 03:30
Uhuru KENYATTA = 1,716,206
And

Raila ODINGA = 1,132,272
 
Mpaka sasa kwa jinsi matokeo yalivyo Uhuru ndiyo wa kwenda Ikulu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom