Raila kawekwa na Uhuru kuvuruga biashara za Ruto, kasema Wakenya wagomee vifuatavyo

Raila kawekwa na Uhuru kuvuruga biashara za Ruto, kasema Wakenya wagomee vifuatavyo

Nashangaa wale wanaosema kuwa wakenya wako smart kwenye issue zao, msiishie mtandaoni, nendeni Kenya muone maisha halisi ya wakenya haswa vijijini. Kenya ni miongoni mwa mataifa yenye watu wa hovyo kuliko unavyoweza kudhani iwapo hujabahatika kuishi huko. Mkifika Kenya msiikomee mijini pata wasaa wa kuzama vijijini kwa muda wa kutosha
Wakenya wengi wanataabika umasikini wao umewafanya Wasomali wapate nafasi ya kuwamiliki kupitia biashara na kununua maeneo mengi...mjini wengi wana maisha nafuu ila huko nje ya miji ni balaa...
 
Wanatumiwa tu kwa maslahi ya wachache maskini ya mungu

Wanaotumiwa ni hawa wote?

Screenshot_20230321-071500.jpg

Na usiyetumiwa ni wewe?

Kwa hiyo ungedhani walihitaji ushauri nasaha kutokea kwako?

Na umefikiria kweli ya dhati yako ukafikia hitimisho hilo?

FpojyuNWIAAJNp3.jpeg

Kwani CV yako Iko wapi angalau tuone?

Zingatia tafakuri ya Dkt. Mollel.
 
Wakuu,

Sasa anaemsukuma huyu Odinga kufanya vurugu zote hizo ni Uhuru kenyatta na ndio mfadhili mkuu wa hiyo migogoro..
Ruto na Uhuru ni kitu kimoja na si Laila na Uhuru. Wakati wa uchaguzi, ilikuwa ni trick ya kisiasa iliyopelekea Uhuru kuonekana wanakinzana na Ruto.

Ilifanyika hivyo ili kuhakikisha Ruto anachukua mamlaka kirahisi; possibly system ya nchi ndiyo iliyokuwa inafanya mchezo huo huku Uhuru, Ruto na Laila wakiwa ndiyo waigizaji wenyewe.

Uhuru na Ruto ni kitu kimoja; usije ukadanganyika hata siku moja
 
Ruto na Uhuru ni kitu kimoja na si Laila na Uhuru. Wakati wa uchaguzi, ilikuwa ni trick ya kisiasa iliyopelekea Uhuru kuonekana wanakinzana na Ruto. Ilifanyika hivyo ili kuhakikisha Ruto anachukua mamlaka kirahisi; possibly system ya nchi ndiyo iliyokuwa inafanya mchezo huo huku Uhuru, Ruto na Laila wakiwa ndiyo waigizaji wenyewe. Uhuru na Ruto ni kitu kimoja; usije ukadanganyika hata siku moja

Uko wrong au hauna taarifa za kutosha juu ya Kenya
 
Uko wrong au hauna taarifa za kutosha juu ya Kenya
Kabla sijawa wrong kama unavyoniona wewe leo, awali niliwahi kuwa na fikra kama ulizonazo wewe sasa hivi; kwa hiyo nilianzia kule ambako wewe bado upo mpaka muda huu; sijafika hapa nilipo kwa bahati mbaya. Nilipitia utafiti wa kutosha hasa wakati wa uchaguzi wenyewe
 
Nashangaa wale wanaosema kuwa wakenya wako smart kwenye issue zao, msiishie mtandaoni, nendeni Kenya muone maisha halisi ya wakenya haswa vijijini. Kenya ni miongoni mwa mataifa yenye watu wa hovyo kuliko unavyoweza kudhani iwapo hujabahatika kuishi huko. Mkifika Kenya msiikomee mijini pata wasaa wa kuzama vijijini kwa muda wa kutosha
Wacha vijijini huko ambako wanakufa na njaa na mifugo ikifa hovyo
Mpaka wanyama pori wakienda Kenya wanakufa kwa kiu

We angalia mijini pia mkenya hata kukuvunjia miwa hawezi kwa sababu ni tabia waliyonayo ya uchoyo

Masikini hao tuwape sehemu kwetu waje walime maana wana njaa sana mpaka huruma
Ardhi kubwa inamilikiwa na viongozi na matajiri wakubwa
Mkenya anajisifia ana shamba ukimuambia wapi anakuambia nyuma ya nyumba
Kumbe ni garden
 
wale wanaoandamana wanaamini wanapiganiwa maskini kumbe watu wanapigania maslahi yao binafsi tu
Ndio maana naendelea na shughuli zangu hata nikiona Kuna mkutano wa Injili maana najua mwisho kuna masuala ya kukwanguana Sadaka, mkutano wa Siasa pia the same wanapigania maslahi yao kwa asilimia kubwa na yenu kwa asilimia ndogo
 
Kabla sijawa wrong kama unavyoniona wewe leo, awali niliwahi kuwa na fikra kama ulizonazo wewe sasa hivi; kwa hiyo nilianzia kule ambako wewe bado upo mpaka muda huu; sijafika hapa nilipo kwa bahati mbaya. Nilipitia utafiti wa kutosha hasa wakati wa uchaguzi wenyewe

Hauna taarifa sahihi rudi kajifunze upya, urafiki wa uhuru na. Ruto ulishakufa miaka mingi, urafiki wa raila, uhuru, gideon moi, kalonzo, eugine wamalwa , ndio umetamalaki na kuna beef kwenye hayo magenge mawili kundi moja ni la watoto wa viongozi wastaafu ambao hawakutaka kabisa mtu kama ruto ambae hakua kwenye cycle ya familia ya kiuongozi apate madaraka, hivo ni kama sasa hivi Tanzania usitarajie kupata rais aina ya magufuli yaani ambae hayupo kwenye circle ya familia za viongozi sahau, kwahiyo hakuna cha uigizaji wala nini ndio maana uhuru anaunga mkono maandamano na anatoa pesa nyingi mno kufanikisha hilo, hotuba za karibuni za Riggy G alisema wazi wazi juu ya hilo japo lilijulikana zamani, akina Raila walikuja kustuka muda umeenda ndio wakagundua Ruto ni mafia maana chebukati kaoa dada yake na spika wa bunge la kitaifa, upande wa martha koome ambaye kaja yake kawa IGP wana udugu na rahel ruto, kwahiyo ugomvi ulianzia hapo, lazima uwe na uwezo wa kufeth taarifa ndio ueleze unachofahamu
 
Ndio maana naendelea na shughuli zangu hata nikiona Kuna mkutano wa Injili maana najua mwisho kuna masuala ya kukwanguana Sadaka, mkutano wa Siasa pia the same wanapigania maslahi yao kwa asilimia kubwa na yenu kwa asilimia ndogo

Kwenye maisha unajipigania mwenyewe ukipoteza muda kwamba unapiganiwa unakua umekosa akili
 
Hauna taarifa sahihi rudi kajifunze upya, urafiki wa uhuru na. Ruto ulishakufa miaka mingi, urafiki wa raila, uhuru, gideon moi, kalonzo...
Umeingia deep sana; mimi ni mTanzania ila naipenda sana Kenya yetu.

Wakati wa utoto wetu, baada ya taarifa ya habari tulikuwa tunaimba wimbo uliokuwa ukipigwa KBC unasema hivi:

..Sisi wanaKenya tumeapa, kuwa nawe pamoja siku zote. Wewe ndiwe Rais Moi Dereva, wetu Kenya hatuna mwingine...

Ahsante sana kwa taarifa
 
"semeni dynasty ni mbaya .. hustler atawale"

Hivi hustler Fund bado Iko imeishia wapi!?
 
Umeingia deep sana; mimi ni mTanzania ila naipenda sana Kenya yetu.

Wakati wa utoto wetu, baada ya taarifa ya habari tulikuwa tunaimba wimbo uliokuwa ukipigwa KBC unasema hivi:

..Sisi wanaKenya tumeapa, kuwa nawe pamoja siku zote. Wewe ndiwe Rais Moi Dereva, wetu Kenya hatuna mwingine...

Ahsante sana kwa taarifa

Nadhani sasa tuko pamoja mkuu
 
Back
Top Bottom