Raila kwa Balozi wa Marekani: Kenya Sio Koloni la Marekani, Funga Mdomo wako, jiepushe na Siasa za Kenya

Raila kwa Balozi wa Marekani: Kenya Sio Koloni la Marekani, Funga Mdomo wako, jiepushe na Siasa za Kenya

Kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga, amemjibu Balozi wa Marekani Mchini humo, Meghan Whitman, kuwa Kenya sio koloni la Marekani na kumtaka Whitman kujiepusha na siasa za Kenya, la si hivyo Watafanya mazungumzo ili arudishwe Marekani

Hii ni Siku moja baada ya Whitman kusema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2022 ulikuwa Huru na wa Haki, na Rais William Ruto alimshinda Odinga kwa njia ya haki

Akizungumza katika Mkutano huko Eldoret amesema, "Mwishowe, nataka kumwambia balozi huyu. Acha Wakenya waendelee na mambo yao. Ikiwa Maandamano yanaweza kuleta mazungumzo kati ya Serikali na Upinzani basi kila kitu kiko sawa na Maandamano. Mwambie balozi huyu Kenya sio Marekani, Kenya sio Koloni la Marekani, funga mdomo wako au tutakurudisha Nchini kwako,"

Chanzo: Tuko Kenya


Mzee ameshidwa afikirie kustaafu badala ya kupoteza muda wake. Hakuna cha maana anapigania
Kwa sasa zaidi ya ubinafsi wake
 
Back
Top Bottom