Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Baada ya kinara wa upinzani Kenya Mheshimiwa Raila Odinga Kufanya mazungumzo ya kuleta maelewano na Rais Uhuru Kenyatta, siasa za Kenya zimepata mtikisiko mkubwa kuelekea siasa za 2022. Mtu wa kwanza kuathirika ni William Ruto katika kutaka kuwa mgombea urais mwaka 2022, Ruto alikuwa akijiamini kuwa baada ya kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi mkuu uliopita yeye ana haki ya kuwa mgombea urais 2022 na jamii ya wakikuyu wamuunge mkono kwasasa hilo halipo tena kwani tishio la Raila Odinga dhidi ya wakikuyu halipo tena baada ya mazungumzo ya jana.
Kundi lingine ambalo limeathirika pia ni akina Kalonzo, Wetangula na Mdavadi ambao siku ya kuapishwa kwa Raila Odinga walimsaliti kwa kumkimbia kundi hili linatumia mgongo wa Raila Odinga katika kufanya mazungumzo ya kisiri na serikali kwa maslahi yao binafsi za kisiasa, baada ya Raila Odinga kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Uhuru Kenyatta ushawishi wa kundi hili haupo tena.
Miguna Miguna pia ametelekezwa kisiasa baada ya kuwa ajenti wa Jubilee ndani ya NASA kwa kujifanya General wa NRM huyu Miguna Miguna aliandika kitabu dhidi ya Raila Odinga (Peeling Back the Mask) kilichojaribu kumchafua sana Raila Odinga kisiasa kabla ya hapo Miguna Miguna alikuwa msaidizi mkubwa wa Raila Odinga na akamsaliti.
Uamuzi wa Raila Odinga unafaa kupongezwa pamoja alichelewa sana kuuchukua na ulisababisha maisha na mali ya wakenya kupotea