Raila Odinga arejea nchini Kenya baada ya mapumziko ya siku 4 visiwani Zanzibar

Raila Odinga arejea nchini Kenya baada ya mapumziko ya siku 4 visiwani Zanzibar

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
72f8932e37a85656a8cf1409d72cba0f.jpg
f46433aa111d1f779c76c113560ef87b.jpg


Kiongozi wa Muungano wa Upinzani NASA nchini Kenya, Raila Odinga, amerejea nyumbani baada ya kujichimbia kwa siku nne Zanzibar nchini Tanzania.

Mwanasiasa huyo ambaye amegoma kuutambua ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta alikuwa visiwani Zanzibar kwa mapumziko baada ya kumaliza ziara ya siku 10 nchini Marekani.

Taarifa za kurejea nyumbani kiongozi huyo zimethibitishwa na Msemaji wake, Dannis Onyango ambaye aliiambia gazeti la Nation kuwa Odinga amerejea Kenya.

Pia Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Philip Etale amezungumzia kuwasili Odinga mjini Nairobi.

Ingawa baadhi ya picha zimekuwa zinaonyesha mwanasiasa huyo akiwa mapumzikoni katika hoteli moja Zanzibar lakini ziara yake imehusishwa na hali ya kisiasa nchini kwake.

Mapokezi ya Odinga mwishoni mwa wiki aliporejea Kenya baada ya kuwa nje ya nchi kwa siku kumi yalikumbwa na taharuki baada ya kutokea ghasia zilizohusisha wafuasi wake na polisi.
 
Watu wana memory fupi sana. This is not the first time, inaonekana anapenda hizo mambo..

Senetor orengo in both pics, labda yeye ndo anaeza kutuelezea ni nini hua kinaendelea
http1_bp_blogspot_com-U4FxaC04iwcU6uhbzvg7WIAAAAAAAAB-oz-f4CPxe8ecs1600Raila.jpg
httpsvenasnews_co_kewp-contentuploads201704raila-alcohol.jpg
 
Alafu huyu atakua ana m remont rais wetu amkomoe mwenzie! ila hila zetu wabongo hazijawahi kutupa mafanikio,tusubiri kuaibika
 
Ninyi mnapigana na polisi ,mwenzenu anapewa uno la kizanzibar


Akirudi Kenya mwepesiii
 
Common male behavior in all socio-economic classes....there are some exceptions though...
 
Back
Top Bottom