Raila Odinga awataka wafuasi wa NASA wasiende kazini kesho


Kiongozi wa Muungano wa Upinzani NASA nchini Kenya Raila Odinga amefanya mkutano wake wa kwanza wa kisiasa tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi nchini humo.
Kwenye mkutano wake huo mtaa wa Kibera katika.mji mkuu Nairobi, Raila amewaambia wafuasi wake wasiende kazini kesho akisema Muungano huo utatangaza hatua watakayochukua Jumanne.

Upinzani umepinga matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 ambao tume huru ya Uchaguzi IEBC imemtangaza Rais Uhuru Kenyatta kuwa mshindi.
Rais Uhuru anatarajiwa kuapishwa tarehe 28 kama hakutakuwa na keshi itakayowasilishwa mahakamani kupinga matokeo hayo.
 
Usipoenda kazini bila taarifa yeyote ina maana hutolipwa mshahara na kuna uwezekano wa kufukuzwa kazi,

Iwapo hutokwenda kazini kwa "siku kadhaa" bila taarifa unaweza tolewa kazini, Sasa hawa ambao hawatokwenda kazini kama wanategemea mshahara tu watakula wapi?

Nani atachukua jukumu la kuwahudumia? Kama wakifukuzwa kazi? ni nani atawatetea ili warudishwe makazini na kwa sheria ipi?

Kabla ya kuacha kwenda kazini kwa mgomo ni vizuri kutafakari hayo maswali hapo juu.
 
huyu bwana ana maneno...mbona nchi nyngi duniani huwa na walioshinda na walioshindwa ktk uchaguzi...mbona asikubali tu matokeo na maisha yaendelee....kenya ni yako bwana?
 
Huyu Raila anategemea watu wa slum wambebe kwenye mkakati wake unaofuata baada ya kushindwa na Uhuru...binafsi hua sielewi hii mentality ya hawa viongozi wa aina hii...amekua Mp wa Lang'ata ilipo Kibra na hakuwafanyia cha maana...hata akiwa waziri mkuu pia hakuna la maana watakalomkubuka nalo...sasa wanategemea nini kwake na ameshindwa...wasikumbali kurubuniwa kwa maslahi binafsi ya Raila na kundi lake...hawa ni wapiga dili na kete iliyombaki kwao ni kutengeneza vurugu Kenya ili waitwe na President Uhuru waunde serikali ya mseto...hili sioni wakifanikiwa maana hata vurugu zenyewe kwa sasa ni kwa hawa wanywa gongo Kibra, Mathare na Kisumu....
 
Bad looser!!
Africa, wapinzani ikiwemo chadema hawajawahi kukubali matokeo hata yawe transparent kiasi gani!!
Ni kama ndio utaratibu.
 
Mtu yeyote ni mkubwa kuliko kenya!!
 
Kama haki yake imeporwa m namuunga mkono aitafute tu kwa juhudi zote maana aliyeipora ndio kayataka yote haya ckua upande wa odinga bt kwa hili mzee km unaona umeingiliwa kwny haki yako jitahidi upambane na hali yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…