Raila Odinga awataka wafuasi wa NASA wasiende kazini kesho

Aliyekuwa mgombea wa Nasa, Raila Odinga amewataka wananchi wa Kenya wanaomuunga mkono wasiende kazini kesho mpaka pale atakapotangaza msimamo wake kuhusu kile alichodai uwepo wa wizi wa kura kipindi cha uchaguzi.


Akizungumza na wafuasi hao waliojitokeza kwa wingi katika eneo la Kibera Odinga alisema siku Jumanne ndiyo atatoa msimamo wake.
Odinga aliwakilisha muungano wa Nasa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 8 nchini Kenya, lakini alishindwa kufurukuta baada ya Uhuru Kenyatta kutetea kiti chake kwa kupata ushindi wa asilimia 54.


Odinga aliwaeleza wafuasi wake kuwa walitambua fika kuwa uchaguzi huo ungegubikwa na wizi wa kura na hivyo ndivyo ilivyokuwa.
“Tulitabiri wangeiba kura na hicho ndicho kilichotokea.Hatujamaliza bado. Hatutakata tamaa. Subiri hatua inayofuata nitatoa msimamo Jumanne,”
“Ni wazi kuwa mamlaka husika zimeshindwa kuchukua hatua stahiki na badala yake wanaua watu. Kura zimeibiwa hakuna cha kuficha hapo.


“Ila ninachoweza kuwaambia kwa sasa kesho msiende kazini,”alisema Odinga
Wakazi wa Kibera walifurika kwa wingi kumsikiliza Odinga ambaye aliongea kwa mara ya kwanza katika eneo hilo tangu Kenyatta atangazwe kuwa mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho.
Huenda agizo hilo la Odinga likaungwa mkono katika maeneo ambayo muungano huo una wafuasi wengi kama Magharibi mwa Kenya na mitaa ya Kibera na Mathare iliyopo mjini Nairobi.


Kauli hiyo ya Odinga imekuja muda mfupi baada jumuiya za kimataifa kumtaka awatulize wafuasi wake.
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alikuwa mpatanishi mkuu baada ya mzozo wa kisiasa nchini Kenya uliotokana na ghasia za uchaguzi uliofanyika mwaka 2007, alimtaka Odinga kutumia mifumo ya kisheria kutafuta haki kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais.


"Namshukuru kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kampeni ya uchaguzi ya amani aliyoiendesha. Amekuwa mtetezi jasiri wa demokrasia," alisema Dkt Annan kupitia taarifa.
"Kwa hivyo, namhimiza sasa afuatilie malalamiko yake kupitia mifumo ya kisheria iliyowekwa na aweke maslahi ya taifa mbele, kama alivyofanya kwa uzalendo mara nyingi awali."


Mwaka 2007, watu zaidi ya 1,000 walifariki na wengine 600,000 walihama makazi yao wakati wa ghasia za kikabila zilizozuka baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.


Hali ya sintofahamu imeendele kuwamo nchini Kenya tangu yalipotangazwa matokeo ambayo yalipingwa na wapinzani na kusababisha kuibuka kwa vurugu.
Hadi sasa watu 16 wamepoteza maisha kufuatia vurugu hizo huku wapinza wakiwatuhumu polisi kwa kutumia nguvu kubwa kupambana na raia.
 
aache siasa hizo.
Uchaguzi umeisha wakenya wajenge nchi yao.
Wakifukuzwa kazi atawaajiri huko Chato?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo kajionyesha kwa nini hakufaa kuwa rais.
Wakenya wanazidi kuthibitisha hawakufanya makosa walikuwa sahihi kabisa ,Raila hakufaa kuwa Rais

Sent using Jamii Forums mobile app
asiyekwenda kazini afutwe kazi

Uhuru atosha
Nina imani comments kama hizi zitadumishwa hata baada ya matokeo ya 2020. Kumbe wapinzani hapa Tz huwa wanajitia kauzu wakati ukweli huwa uko wazi kabisa
 
Sawa. Na wasiende tu kazini. Halafu, wakiitwa wa nchi jirani waombe ajira wasijilize kipuuzi!
 
Raila kapumzike chato utoe stresss,wakenya wamechagua mpenda democracy
 
sisi wapinzani wenzio wa tz tunasema uchaguzi ulikuwa wa huru na haki chama tawala hakikuiba na wala pia sisi huku hatuibiwi!
 

hizi akili za kiraila bana!! hiv wewe kwa akili zako za kiraila una malezi bora yapi?!! au malezi bora ya kibera!!
haya kwa akili zako za kiraila kesho hakuna raia kwenda kazini, na kibera nzima imeshangilia tamko hilo.
 
Well said mkuu.Na ndio ujue Raila ni mnafiki mkubwa anataka wambebe na kuwatumia kujinufaisha yeye kisiasa lakini wakifanya fujo na kuuliwa yeye anasema eti "i don't contol the people"
 
We mpumbavu sana. Wewe unaweza kutuhakikishia una akili. Uwe na adabu. Kwa Rais wetu. Kama kwenu somalia. Rudi tu. Afu JF mnaachia wajinga kama Hawa. Badala ya hoja analeta matusi. Usipoheshimu chako ujue sio chako unachako.

Mkuu hata mimi nawashangaa ma Moderators, sijui kwa nini wanavumilia moral decay ya kiwango hiki hapa? Kama Taifa tuna wajibu wa kumpa Head of State heshima yake it doesn't cost us a penny - some members thrive on matusi sijui kwa nini?
 
Wasipokwenda kazini maana yake hospitali na vituo vyote vya tiba vitafungwa, mitambo ya kusukuma na kusambaza maji na umeme itazimwa nk. Wakenya watakufa kwa kukosa huduma ya tiba eti kwa ajili ya mtu mmoja kakosa upresida! Badala ya kupeleka malalamiko yake mahakamani anataka watu wafe! Ingalikuwa Tz mtu wa aina hiyo DC angekuwa ameshamuweka kokoroni for 48 hours baada ya hapo polisi wangalishugulika naye pamoja na mkojo wake kikamilifu before kumkabidhi kwa primary magistrate court na DPP!
 
kaka wala hujakosea...katiba ya Kenya ya sasa ni mradi wa Raila pamoja na wakenya wengi..alipiginia hii katiba iliyopo mpaka akafanikiwa..moja ya nguzo kuu ya hii katiba ni kua na Tume huru ya uchaguzi na pia kua Mahakama huru..ajabu leo hii Raila huyu huyu anadai haendi tena mahakamani kudai haki yaki anayosema ameporwa...sasa mtu wa aina hii ni hatari sana kwa ustawi wa nchi maana mbele hayumo na nyuma hayumo ni kama kinyonga...kwa sasa kete yake iliyobaki ni hawa ma slum dwellers Nairobi na kadhalika kuleta fujo...hivi leo ndugu zangu na maisha yalivyo bana atokee mtu akwambie usiede kazini sababu hajawa Raisi kweli inaingia akilini....na haleti mbadala wa jinsi ya kupata chakula, ada za shuke watoto n.k....hii gap ya wenye nacho na maskini ndio msingi wa Nasa....hivi kwa nini asiede Muthaiga au Runda kuwaambia wakaazi wa huko huo upumbavu wake...poor Raila he knows the poor,illetrate, naive slum dwellers s what he can hold unto..
 
Raila anaonekana hataki kukubali matokeo., ni.wakati sasa Rais Magufuli ambaye ni rafiki yake binafsi ajitenge na kusema hamuungi mkono tusikie

Sisi watanzania hatutaki vurugu zitokee Kenya , Aige mfano wa.Edward lowassa ambaye pamoja na ushahidi wa kuibiwa kura kuwepo na vituo vya Tallying centre vya Chadema kuvamiwa na vijana kama 100 wataalamu wa IT kuwekwa ndani bado alijizuia na..kukaa kimya pamoja na wananchi..kuwa tayari kupigania ushindi na...kuandamana kupinga Magufuli kuiba...kura .

Ni unafiki kama...yeye Lowassa hajamzuia...kutawala asimshauri huyo rafiki yake amuache Uhuru...atawale.
Kwanza Raila pia alishiriki kuibia watanzania kura mwaka 2015,..akimtuma.msaidizi wake mmoja...kuongoza timu.ya IT ILIYOKUWA.DOUBLE TREE HOTEL..na kumeletea rafiki..yake pesa za kampeni

Bora wakenya mmemuadhibu Raila . mnhetawaliwa kwa visasi kama..huko Tanzania
Pia raila ni..project ya muda...mrefu...ya kutawala afrika mashariki ya Kagame na Museveni...tayari wamekamata Congo kupitia Kabila.
TANZANIA tumeshatekwa..kupitia..huyu..ndugu yao mwaka 2015 na walitaka kutumia Raila kuteka Kenya
THE BAHIMA EMPIRE SYNDICATE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasipokwenda kazini wataenda kula kwake? Huyu Odinga ameshakuwa kama Lyatunga Mrema yule wa vunjo.
 
Raila anasema eti umoja wa mataifa, U.N, wachunguze kura ZAKE zilivoibiwa! 😀 Huyu mzee ameanza kuchizi kabisaa, na bado! Hehe!
Kwani ni yeye pekee ameibiwa? https://jamii.app/JFUserGuide this mwitu Odinga ,ule uchaguzi wa 2013 yeye pekee kaibiwa sasa tena 2017 yee pekee kwanini hawapingi matokeo ya MP's ,Senators au ma Gavana? This man is full of selfish BULLSHIT.
 
Mkuu hata mimi nawashangaa ma Moderators, sijui kwa nini wanavumilia moral decay ya kiwango hiki hapa? Kama Taifa tuna wajibu wa kumpa Head of State heshima yake it doesn't cost us a penny - some members thrive on matusi sijui kwa nini?

Hii moral decay unayoilalamikia hapa unafanya ivi pia wale watawala wanaposimama majukwaani na kuwatukana watawaliwa au maadili yanatakiwa yafatwe na upande mmoja,ukiona mpaka watu rahimu kama wa Tz wameamua kuwatusi viongozi wao basi jua kua tatizo sio raia pekee yao hata hao wanaongoza wana poromosha matusi na maneno yasiyo na staha kila leo,yupo mmoja kila akipata nafasi lazima awaite 'wapumbavu' wanainchi ambao wamewahi kumpa ridhaa ya kuwaongoza na kama mliitaka demokrasia lazima mukubali gharama zake pia Obama kachezea sana matusi na Trump kila siku anayaoga matusi.
 
Sasa nimejua kwa nini ni rafiki wa bwana yule kwa akili hiyo!
Kwani tofauti yake na hawa wetu ipo wapi? Si wa kwetu walizira ufunguzi wa bunge la 11 ama umesahau. Huyu na Maalim Seif wanatofautiana nini? Seif kaahidi ninyi kina Mwakabanje kua ktk miezi mitatu mtapata nchi yenu.

Dr kama kweli wewe ni dokta wa kweli siyo kama Luta Nelson ama Remmy basi unaiaibisha fani ya udaktari.
 
Raila anasema eti umoja wa mataifa, U.N, wachunguze kura ZAKE zilivoibiwa! 😀 Huyu mzee ameanza kuchizi kabisaa, na bado! Hehe!
Hahah sisi huku chadema walisema wataenda huko kwenye mahakama ya ICC kupinga matokeo ya uchaguzi sijui hata iliishia wapi aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…