Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Kiongozi wa Muungano wa Upinzani NASA nchini Kenya Raila Odinga leo anatarajiwa kutoa maamuzi magumu kuhusu hali tete ya kisiasa nchini Kenya baada ya Uchaguzi.
Bw. Odinga ambaye aliwaambia Wakenya wasiende kazini siku ya Jumatatu (jana), wito ambao hakuitikiwa na wengi hata wale wafuasi wake. Maamuzi yake yanasubiriwa kwa hamu nini atawaambia Wakenya hususan wafuasi wake hao.
Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanasema huenda akakabidhi kesi yake hiyo kwa umma wa Wakenya
Bw. Odinga amepinga matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 ambao tume huru ya uchaguzi IEBC ilimtangaza Rais Uhuru Kenyatta kuwa mshindi.
Updates
Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema muungano mkuu wa upinzani NASA utafungua kesi kwenye Mahakama ya Juu ya nchi kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu.
Odinga amewaita wanasiasa walioshinda "vifaranga vya computer", alisisitiza kwamba matokeo ya uchaguzi yalibadilishwa kwenye computer za Tume ya Uchaguzi.