Raila Odinga: ‘Nitagombea urais Kenya 2022’

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kwamba atagombea urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo mwaka wa 2022.

Alitoa tangazo hilo katika kongamano la Azimio la Umoja siku ya Ijumaa. "Ninatangaza kwamba ninakubali kujiwasilisha kama mgombeaji urais," Raila alisema.

Alizindua vuguvugu la Azimio la Umoja, ambalo alisema litakuwa muungano. Kiongozi huyo wa chama cha ODM alisema hivi karibuni atatoa manifesto yake.

Raila alisema maafikiano yake na Rais Uhuru Kenyatta sio yenye nia ya kujitajirisha. Alisema kuwa hatawahi kuuliza chochote kutoka kwa mwafaka huo isipokuwa kwa nafasi ya kutumikia.

“Lazima niongeze hapa kwamba kwa maridhiano haya, siombi chochote na kamwe sitaomba chochote isipokuwa nafasi ya kutumikia,” alisema.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alisema kuwa kuleta amani si biashara ya kujitajirisha, bali ni wito kutoka kwa Mungu.


==========

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ametangaza rasmi kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao nchini Kenya kwa tikiti ya Muungano wa Azimio la Umoja.

Basi la Azimio la umoja linaloongozwa na Raila Odinga, liling'oa nanga katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani, uliochorwa rangi mpya za samawati na nyeupe za chama cha ODM. Aidha kila pembe ya uwanja huo yenye viti elfu sitini kulikuwa na mabango ya herufi za R zenye rangi ya chungwa, kuashiria jina la kiongozi huyo mwenye sifa ya kupigania demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya.

Kiongozi huyo ambaye alizuru taifa zima kabla ya kongamano la leo alibainisha hoja 10 ambazo ni mwarubaini kwa changamoto zinawakabili wakenya. Raila aliahidi kuwa serikali yake itatenga shilingi za Kenya bilioni mbili za kuwapa vijana kila mwaka. Kuhusu suala la afya,

Raila ameahidi kuwa kila Mkenya atakuwa na mpango wa bima ya afya, huku serikali yake ikiwalipia wale wasiojiweza. Huku Kenya ikiongoza kwa ukosefu wa nafasi za ajira Afrika Mashariki, Raila amesema kuwa, atahakikisha kuwa vijana wanapata kazi kwa kuboresha sekta ya jua kali. Hii itakuwa mara ya tano kwa Raila kuwania kiti cha urais.

"Nilipoongea na Wakenya nikawauliza niendelee au nisiendelee, nawajibu nitaendelea na tarehe nane tisa mwezi ujao, baba atakuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha urais.”, alisema Raila.
 
Nchi ya kabila 3 hiyo, Gikuyu, Kalenjin na Jaluo, kabila zingine ni watazamaji tu. Matiang'i anasifa zote za kiutendaji kuwazidi hao farasi wawili, lakini tatizo ni kabila lake.

Sifa zoote anazo, lakini "aah jama, mkisii?(Nyerere 1995)[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kabisa ukabila kwa Kenya ni tatizo sana.
 
Huyu ndugu yake na MK254 ameshastfu siasa?
View attachment 2040023

Huyu kilichomponza ni alichokonoa sysem huku akijua stakabadhi zake haziko sawa kwamba alishaukana uraia na kuukwa wa kule Canada kisha akarudi kinyemela na kugombea uongozi, alivumiliwa kwenye vyote hivyo ila akapitiliza na kukanyaga nyaya fulani hivi.

Anyway hongera Raila kwa kuzindua vuguvugu lako na azimio la kugombea urais, nawatakia nyote kila la heri pamoja na wengine kama vile Ruto n.k. japo mumenikera kwa hizi kampeni zenu za kabla ya wakati wake, kikubwa tudumishe amani, tutangulize uzalendo, kila mmoja auze sera zake za namna gani ataendelea kuiboresha nchi yetu ili iendelee kuwa kiongozi ukanda huu kwenye kila kitu.

Mungu awabariki wote watakaojitokeza, ni ndugu zetu, wazalendo wa nchi yetu na kila mmoja ana maslahi mema kwa taifa letu, kikubwa tuwasklize kisha tufanye maamuzi kwa kuzingatia hivyo vigezo na bila kushinikizwa. Tuendelee kuwa mfano bora wa kuigwa na majirani, hivi kule Tanzania yule Mbowe kesi yake iliishia wapi, bado yuko jela? Kitambo sijafuatilia siasa za Bongo tangu CCM iliponyakua kila kitu 100% kwenye uchaguzi mkuu wa kitaifa, niliwaona wenzetu kama ambao wamepagawa au sijui kitu gani kiliwaingia akilini.
 
Bila kuitaja Tanzania huoni raha
Yaani unataka tuwaige kwenye suala ukabila?
Mnatakiwa muwe karibu sana na Mungu,huyo Ruto simuamini hata kidogo
 
Bila kuitaja Tanzania huoni raha
Yaani unataka tuwaige kwenye suala ukabila?
Mnatakiwa muwe karibu sana na Mungu,huyo Ruto simuamini hata kidogo

Nyie mna nini cha kuigwa, kila nikitulia nicheck siasa za kwenu naona madudu tu kila uchao, mara kiongozi mkuu wa upinzani ameswekwa jela anatuhumiwa ugaidi mithili ya akina Alshabaab, Alqaeda na ISIS. Makomando wanatoa ushahidi sijui eti walifinywa ili wambambikie...

Viongozi wengine wanasotea Ubelgiji na Canada walikotorokea wakihofia maisha yao. Halafu makundi ya kikabila kama lile maarufu la Wasukuma mnaloliita Sukuma gang yanamsumbua mama.
CCM yenyewe ambayo imeng'ang'ania madaraka miaka yote mnakwaruzana ndani kwa ndani, mara kundi la wahuni sijui akina Nape vs PolePole, mara PolePole nyumba yake imevurugwa na wasiojulikana, humo picha zinaonyesha chumba chenyewe ukiambiwa cha kiongozi utashangaa, kina mavitu ya ajabu ajabu.

Mnachohitaji kwenu huko ni kuonja uongozi mbadala, yaani ifike mpokeze uongozi kwa upinzani ili mfaidi mawazo tofauti na hayo ya chama kimoja miaka yote mumeganda sehemu moja tu na katiba ya mkoloni. Sisi tulipobadilisha na kuachia upinzani uchukue uongozi, yaani uchumi wetu ulipaa na ukifuatilia utaona kuanzia hapo ndio tuliipa Tanzania buriani na kuiacha mbali sana kiuchumi.

Msipobadilika, mtaendelea kukwama kwenye umaskini wote huo licha ya raslimali nyingi mlizo nazo.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…