Kenya 2022 Raila's Hard Earned Presidency

Kenya 2022 Raila's Hard Earned Presidency

Kenya 2022 General Election

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Acheni Raila awe rais ale bata.

Mapito ya kisiasa ya Raila Odinga:-
  • Alituhumiwa kwa kikundi cha vuguvugu cha MWAKENYA 1980 kilichochagiza mabadiliko ya mfumo wa siasa za Kenya kutoka kuwa za kiimla kwa mkono wa chuma wa dikteta Daniel Arap Moi.

  • Alibambikwa kesi ambayo haikusikilizwa Mahakamani ya uhaini na kunyimwa haki ya dhamana na kusekwa jela kwa miaka 6.

  • Awali ya namba 2 hapo juu, aliwekwa kizuizini nyumbani kwa miezi 7.

  • Alitoka jela kwa matishio ya kaka yake Dr. Oburu Oginga aliyekuwa Jasusi Mwandamizi wa KGB Urusi aliyempa Moi ultimatum ya masaa 48 kumuachilia huru bila masharti mdogo wake kinyume na hilo ndege-vita za Kirusi zingetua Nairobi kumung’oa Moi madarakani. Ikumbukwe enzi hizo zilikuwa za vita baridi kati ya US na USSR waliotaka kujitanua duniani. Ukoo wa Oginga ni wajamaa wa mrengo wa centre-left-wing na Moi alikuwa m-capitalist.

  • Kwa kinywa chake mwenyewe Raila, anasema kule kwenye chambers za mateso alipewa mateso ya kila aina ikiwemo waterboarding, kupigwa na kupata majeraha ya mwili mzima na akawekwa kwenye kichumba kilichojazwa maji saizi ya shingo yaliyokolezwa upupu, pilipili na chumvi kwa siku 9 akipewa chakula kilichochanganywa na kinyesi ili atangaze kuachana na siasa. Jibu lake lilikuwa ni fanyeni mfanyalo lazima Kenya iondoke kwenye udikteta hata kwa roho yake yuko tayari.

  • Alichukuliwa na wenzake wakapelekwa jengo refu la pili Kenya la Nyayo House usiku wa manane wakapandishwa ghorofa ya 24, na wenzake wale wakatupwa dirishani hadi chini bongo zikatapakaa barabarani (ili kesho ionekane kwamba wamegongwa na magari), wakamwambia Raila kwamba umeona hao wenzako wamekufa, sasa wewe kesho uandike barua ya kuomba msamaha (amnesty) kwa Moi na kuahidi kuachana na siasa milele. Akawambia nitupeni na mimi pia lakini mabadiliko Kenya hayakwepeki hata kwa roho yangu. (Mnakumbuka Mandela pia alipopewa hundi ya ela nyingi na Makaburu ili asaini iwe kama blackmail ya kuachana na siasa za ukombozi alisema nipeni nisaini, alipopewa akaandika I want freedom for South Africa not cheque)

  • Alipotoka jela kwa msaada wa kakake Jasusi Dr. Oburu aliyempa mbinu za kutorokea Tz kufuatia taarifa za siri kuvuja kwamba anatolewa ili apangiwe mauaji nje ya jela, na alipokuta pasi yake imefutwa na serikali ya Moi, alifanikiwa kutoroka na kuja Tz na Mwl aliyekuwa na urafiki na familia ya Jaramogi Odinga kwa vigezo vya Ujamaa wao, EAC, PAFMECA na PAN-AFRICANISM alimpa Raila pasi ya Tz na tiketi ya ndege (mali zake zilishikiliwa na Moi (assets frozen)) na kumuombea aende Norway ambako watampa pasi ya UN ya kusafiria duniani kote kasoro Kenya, mbinu hii ilifanikiwa na akaanza kampeni kubwa ya kumbana Moi kimataifa na kufanikiwa kutengeneza mazingira ya demokrasia mpya Kenya iliyoanza rasmi 1992. Mwl alimpa pia Sam Nujoma pasi na tiketi ya kwenda UN kudai uhuru, Nujoma alitoroka kwa punda miezi mitatu porini kufika Tunduma. Mwl pia alimpa Thabo Mbeki pasi baada ya yakwake ya Afrika Kusini kufutwa kwa tuhuma za kushiriki Umkhonto we Sizwe (Spear of the nation).

  • Mwanaye kipenzi chake Fidel Castro Odinga aliuawa (assassinated) 2015 kama namna ya kumzima Raila kuachana na siasa na pia asiache mbegu yake ya siasa (Fidel Castro Odinga) ichipue na kuja kusumbua Kenya.

  • Mwaka 1966 Jaramogi alijiuzulu umakamu wa rais baada ya kuhitilafiana na Jomo Kenyatta na Jaramogi kuunda chama chake cha KPU 1967 na Jomo Kenyatta kukipiga marufuku na kumuweka kizuizini nyumbani Bondo Sakwa Siaya County. 1969 ziara ya kwanza ya Jomo Kenyatta Kisumu/Nyanza ilisababisha mauaji ya halaiki na kikosi cha ulinzi wa rais baada ya rais kushambuliwa kwenye mkutano wa hadhara kwa tuhuma za kumsaliti Jaramogi kwenye kinyang’anyiro cha urais. Jaramogi miaka ya mwanzo baada ya uhuru alijenga tabia ya kusafiri na wanae Raila na Oburu kwenye mikutano mikubwa ya ndani na ya kimataifa kama namna ya kuwajenga kisiasa. Mke wa Jaramogi Mary Juma alikataa wanae wasifundishwe siasa la hasha anaachika, jibu la mumewe lilikuwa ni kwamba Kenya lazima iwe huru hata kwa roho za wanae, mwaka 1984 mamake huyu alifariki Raila akiwa kizuizini na alitaarifiwa miezi miwili baada ya msiba kwisha.
Baadhi ya Mafanikio yake kwa uchache:-
  • Raila amewahi kupitia usuluhishi wake kumng’oa rais haramu Laurent Gbagbo bila kujali matishio, alisuluhisha Mugabe na Tsvangirai bila kujali matishio ya Mugabe. Ujumbe wake ulikuwa ni kwamba despots lazima waondoke Afrika. AU imekuja kuasili falsafa hii.

  • Amekuwa Special Envoy wa UN takriban mara mbili na sasa ni High Representative wa AU kwa masuala ya miundombinu Afrika.

  • Alitetea kisiwa (pekee duniani kisichokuwa na fukwe) ambacho ni mazalia ya samaki wengi cha Migingo na kumzulia chuki na Museveni aliyepeleka vikosi kisiwani hapo kuvamia wavuvi na kuwahujumu mali zao na kushika doria. Kenya inamiliki 6% ya ziwa Victoria, Uganda 43% na Tz 51%.

  • Aliondoa wavamizi wa ardhi oevu ya kwenye chanzo cha mto kwenye msitu wa Mau ambao unategemewa na nchi za Nile kuingiza maji ziwani.

  • Amejenga mabarabara akiwa waziri wa ujenzi na waziri mkuu.

  • Ameandika katiba mpya ya aina yake duniani.

  • Amekuwa bingwa wa maridhiano na Kibaki na Uhuru.

  • Amegombea urais mara 6 tangu 1992 kwenye demokrasia ya kiliberali.

  • Ameunda vyama vi 4 (NDP, LDP, NAK, ODM) na amekaa KANU, KPU na FORD Kenya, na miungano (coalitions 3 za NASA, NATIONAL RAINBOW ALLIANCE, AZIMIO ONE).

  • Ame-foil assassinations sita zikiwemo za sumu (ambayo hii moja ilimnasa lakini hakufa), ujambazi na ajali ya chopper.

  • Hakuna Afrika hii mwanasiasa amepata mateso makali kama Raila Odinga.
 
Huyo babu apumzike, akalee wajukuu. Awaachie na wenzie. Hivi anaamini bila yeye Kenya haiwezi kuendelea?
 
Huyo babu apumzike, akalee wajukuu. Awaachie na wenzie. Hivi anaamini bila yeye Kenya haiwezi kuendelea?
Katiba ya Kenya inasema umri wa kugombea urais ni miaka 18, ilishushwa toka miaka 35. Bunge liliondoa ukomo wa umri wa kugombea wa miaka 70 kwamba inakandamiza haki za watu kutaka kugombea.
 
Yetu macho masikio tuone nani mbabe wa Kenya ?
 
Back
Top Bottom