Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,890
- 26,440
Nchi ikiwa na idara ndogo ya Usalama kama kitengo kimoja tu na kukosa kiongozi mahiri na katiba inosiginwa kila mara, huyumba sana na kukosa mwelekeo na yale tunoyashuhudia leo ni matokeo ya kuyumba wa idara ya Usalama wa Taifa na hata pia kutuhumiwa kijihusisha na vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi.
Mataifa makubwa kama Russia na China wana wizara kamili zinoshughulikia Usalama wa Taifa. Kwa Russia KGB ndo ilokuwa taasisi ya usalama ikiwa imeanzishwa rasmi mwaka 1954. KGB ni kirefu cha maneno Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti ilundwa na kupewa majukumu ya kulilinda taifa la ilokuwa umoja wa Kisovieti au USSR, kulinda dhidi ya ujasusi wa nje na pia kulinda uongozi wa nchi , kusimamia vikosi vilolinda mipaka, pamoja na kufuatilia mienendo ya raia.
Pamoja na mambo mengi maovu ambayo KGB imeelezewa kuyatenda katika kipindi cha utawala wa Joseh Stalin na Vladmir Lenin, taasisi hii ilihakikisha taifa la Urusi haliangamizwi wala kudhuriwa na maadui wa ndani au nje na ilikuwa na wafanyakazi wapatao 250,000. KGB ilikuja kuwa wizara kamili mwaka 1946 ilipoitwa Ministry of State Security au MGB sambamba na wizara ingine ya mambo ya ndani MVD na wizara zote zilisimamiwa na bwana Lavrenty Beria.
Majukumu ya msingi ya Beria yalikuwa ni kusimamia mpango wa nyuklia pamoja na kuangazia ujasusi wa kutambua shughuli za nyukilia zilofanywa na Marekani pamoja na Uingereza. Ni wakati huo majasusi wa Joseph Stalini tiyari walikwishatambua kuwepo kwa mipango ya nyuklia ilokuwa ilifanywa na Marekani na Uingereza.
MGB nayo ikiongozwa na V.S Abakumov chini ya usimamizi wa Beria ilikuwa na jukumu la kuhakikisha yasimamia uzuri vita ya pili ya Dunia na kuimarisha nguvu yake upande wote wa Ulaya Mashariki huku ikifanya operesheni zote za kijasusi na kusisitiza uzalendo kwa maofisa wote.
KGB ikiwa wizara kamili ilikuwa na idara zipatazo 20 ndani yake miongoni mwao zikiwemo idara ya ujasusi wa nje, ujasusi wa ndani, ujasusi wa kitekniki, ulinzi wa viongozi na ulinzi wa mipaka yote ya nchi. Baadae KGB ikawa imepanua shughuli zake za kijasusi khasa wa nje kiasi cha kuwa sambamba na idara ya ujasusi wa nje ya CIA ya Marekani majasusi wake wakitumia mwavuli wa uandishi wa habari au wafanyabiashara.
Kwa njia hizo KGB iliweza kupata taarifa zote za kisayansi na kiteknolojia ambazo ziliwezesha kutengeneza nyambizi, ndege na makombora. Sambamba na hilo idara yake ya ujasusi wa kijeshi au GRU ambayo majukumu yake yalikuwa ni opereshini za kijeshi tu, KGB iliweza kufanikiwa sana kupata taarifa za kijasusi kwa ufanisi mkubwa kutoka kwa nchi mahasimu na washirika wao.
KGB haikufanya kazi zake kwa uzuri kipindi cha Mikhail Gorbachev jambo lilopelekea kuwepo na jaribio la kumpindua kwasababu ingawa aliiheshimu KGB lakini sera zake za mabadiliko hazikuwapendeza majasusi wengi ambao waliona kuwa Gorbachev ana ajenda ingine khasa lipoonekana akiwavutia zaidi nchi za magharibi.
Baada ya jaribio hilo la mwaka 1991 mapinduzi liloongozwa na viongozi wa ngazi za juu ya KGB aiwemo mwenyekiti wake bwana Vladmir Kryuchkov, Gorbachev akaamua kuivunja KGB na kuondoa vikozi vingi ambavyo baadae vilimegwa na kuwa huru kuanzisha idara za ujasusi katika nchi za Ukraine, Belarus na nchi zingine zilounda umoja wa kisovieti.
Baada ya kuvunjika kwa USSR KGB ikaja kuwa chini ya Russia na raisi Boris Yetsin akasimamia kumegwa kwa KGB na kuundwa kwa idara za ujasusi wa nje SVR na ile ya ujasusi wa ndani ya FSB chini ya wizara kamili. Leo hii KGB ni idara kubwa zaidi duniani ikiwa na majasusi wapatao 480,000 na kati ya hao 200,000 husimamia mipaka ya nchi.
KGB ina watoa taarifa wapatao milioni moja na kiongozi yoyote wa Russia huitegemea taasisi hiyo na idara zake kwa taarifa zote za kijasusi, ufuatiliaji wa viongozi wakuu, na raia wote. KGB hushiriki kinagaubaga katika matengenezo yoyote ya sera ya kigeni au "foregn policy".
Yapo masuali kwamba pamoja na nguvu kubwa ya KGB lakini ilishindwa vipi kuzuia kuanguka kwa ilokuwa USSR. Lakini majibu ni rahisi tu kwamba kulikuwepo urasimu, baadhi ya majasusi kuwa double agents kwa mataifa mahasimu na wengine hata kukimbilia Marekani na Uingereza. Kipo kipindi ambacho wadadisi walikuja na hitimishi kuwa KGB ilikosa ujuzi wa kufanya uchambuzi makini kuhusu hali ya kisiasa nchi humo na kushindwa kuzuia matukio yanotokea yanotishia usalama khasa katika kipindi cha miaka 15 ilopita.
Lakini pamoja na hayo bado KGB ilifanikiwa kumpata mmoja wa majasusi wake kwa jina la Vladmir Putin ambae kwa ujuzi wake wa masuala ya kijasusi ameweza kuiimarisha idara za ujasusi za Russia na kuzifanya kuwa moja ya idara zenye nguvu duniani na pia kulifanya taifa ya Russia kuwa moja ya mataifa makubwa tishio kwa nchi za magharibi na Marekani.
Pia Putin ameweza kufanikiwa kuwa karibu na China, India na Korea Kaskazini nchi ambazo zote zina silaha kali za nyuklia na zinofanya biashara na Russia zikibadilishana mafuta, teknolojia na ujuzi mwingine muhimu.
Tanzania yaweza kabisa kuiga mtindo wa uundaji wa taasisi imara ya ujasusi mithili ya KGB ambayo itasimamiwa na wizara kamili ya ulinzi wa taifa na kupitia njia hiyo usalama wa taifa waweza kufanywa ni ajenda ya kitaifa ambayo itahusisha wananchi wote bila kuwa ni idara moja tu ambayo haina usimamizi unofuata katiba na misingi ya usalama wa nchi kwa ujumla.
Wiki ijayo ntaelezea Wizara ya usalama ya China na majukumu yake kwa taifa hilo kubwa Duniani.
Credit: Nimemtumia mwandishi Robert W, Pringle ambae ameandika historia ya kuanzishwa kwa KGB.