Rais ajaye afikirie kuunda Wizara kamili ya Usalama wa Taifa na si Idara moja tu ndogo ya Usalama wa Taifa

Kuna umuhimu gani hasa wa kukirasimisha hicho chombo kuwa wizara? Binafsi naona China na Urusi waliunda wizara ili usimamizi wa moja kwa moja kutoka serikali kuu uwe mkali, rais na mawaziri waweze kutumia chombo cha usalama watakavyo.

Lakini kwa nchi kama Marekani, Canada na Uingereza, hakuna wizara kuna idara tu. Zinapewa rasilimali na serikali lakini zinakuwa na uhuru kiasi fulani. Wataalamu wanafanya kazi kwa ajili ya usalama tu na si harakati za kisiasa.

Sasa ikiletwa wizara si ndo CCM itaiweka mfukoni kabisa kama Putin alivyoifanya MGB na Xi alivyoifanya MSS? Wanatumia vyombo vya usalama kulazimisha ushawishi wao wa kisiasa.
 
Katiba pia wanaweza wasiielewe vile vile wakaiita kijitabu, utawafanyaje?
Watu ambao huwa wana mawazo kama haya nina hili jibu. Kuna nyumba mbili ziko mtaani mmoja zimefanana kwa kila kitu. Moja ina uzio na geti za nondo, pia ving'ora na nyingine haina chochote. Zote haziishi mtu ila zina mali ndani. Wezi watavunja ipi kwa urahisi? Tukirudi kwenye katiba, ukipunguza kabisa madaraka ya rais na viongozi wengi wakapatikana kwa kuchaguliwa. Wanaoteliwa ilazimishwe wapitishwe kwanza na bunge. Tume ya ya uchaguzi isiundwe na rais n.k n.k. Hitimisho: tungekuwa na katiba nzuri Samia kwa vyovyote asingepita kipindi hiki.
 
Kwenye kupunguza madaraka sawa lakini tumejipangaje hilo bunge likipangwa kama wanavyofanya sasa hivi si litakuwa bunge lake tena, maanake wanamwaga hela tu.
 
Kurasimisha ni tofauti na kuunda kuwa wizara kamili.

Hizo nchi ulizitaja ni kweli zina taasisi hizi na ni taasisi kamili chini ya wizara husika.

Huu ni mfumo mzuri wa kuwa na taasisi na si kaidara tu ambako leo apewa waziri fulani au kesho yahamishiwa ofisi ya raisi na kadhalika.

Hata Putin mwenyewe au Xi wakizingua waweza kuondolewa na taasisi hizo ambazo wao wamezikuta.

Hizo ni wizara ndo zaongoza taasisi hizo Marekani ni state department (CIA) na Homeland Security (FBI)

UK wao wana wizara ya usalama wa ndani Home Office (MI5) na wizara ya mambo ya nje Foreign & Commonwealth Office (MI6) na hata Australia wana ASIS Ujasusi wa nje na ASIO Ujasusi wa ndani lakini zipo chini ya wizara maalum.
 
Mbona nina mashaka mkuu, CIA ni taasisi inayojitegemea na FBI ni chombo cha serikali cha kuchunguza uhalifu... M15 na M16 zina uhuru kiasi...
 
Ikukupendeza ongea mchakato wa kupata Katiba mpya pendekezwa itokanayo na ile rasimu ya warioba.

Ukimsikia Gwajima rasheed anasemea suala la independence ya idara nzima ya Usalama.
 
Katika Usalama wa nchi, inatakiwa proffessionalism, kwa maana halisi ya Intelligence, na si utumishi wa kisiasa.
 
KGB siku haipo kuna FSB iliyoundwa baada ya kuanguka kwa ussr.

Naungana na wewe usalama wa taifa lazima ubadilishwe.
 
 
Marekani CIA wameondoa Marais wengi kwasababu ya interest za nchi
 
Katika Usalama wa nchi, inatakiwa proffessionalism, kwa maana halisi ya Intelligence, na si utumishi wa kisiasa.
Huo ndo msingi wa kuanzisha Wizara kamili ambayo pamoja na majukumu mengine itasimamia utaalam na ushauri wa kitaalam kwa serikali yoyote ile iliyopo.

Isitoshe waziri wa usalama ni lazima atoke kwenye jamii hiyohiyo ya wana usalama au jeshini khasa MI.
 
Wiki ijayo nchini China kutakuwa na mkutano mkuu unohusu masuala ya Usalama Duniani utaofanyika kuanzia tarehe 17-19 katika ukumbi wa mikutano wa China National Convention Centre.

Mkutano huu umeandaliwa na umoja wa wanasayansi wa kijeshi wa China au China Association for Military Science pamoja na Taasisi ya masomo ya kistratejia au China International Strategic Studies.

Wahudhuriaji wapatao 1800 toyari wamepokea mwaliko wakiwemo wajumbe, waangalizi na waandishi wa habari.

Mgeni rasmi katika mkutano huo atakuwa waziri wa ulinzi wa China bwana Dong Jun ambae ndie atatoa hotuba rasmi au Keynote Speech.

Nchi 100 zimethibitisha kuhudhuria mkutano huo zikiwemo nchi za Nigeria, Vietnam, Mexico, Ufaransa, Brazil, Russia na Singapore.

Muandaaji wa mkutano huo kanali Wu Jiangang amesema nchi zingine bado hazijathbitisha lakini ana imani zitafanya hivyo.

Je, Tanzania itatuma mwakilishi huko?

Mkutano huu wafuatia mkutano mwingine wa kila mwaka ulofanyika nchini Singapore unoitwa Shangri-La Dialogue ambao ulifanyika kati ya tarehe 30 May hadi 1 June mwaka huu na ambao wahusu masuala ya usalama.

Mkutano huu ulihudhuriwa na wajumbe wapatao 500 kutoka nchi mbalimbali na mgeni rasmi alikuwa raisi wa Ufaransa bwana Emmanuel Macron.

Nchi kama Tanzania hii inakuwa fursa nzuri ya waziri wa usalama (kama tungekuwa nae) na ujumbe wake wa maofisa wa ngazi za juu wa JWTZ kuhudhuria ili kupata mawili matatu ya kujifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…