Rais ajaye afikirie kuunda Wizara kamili ya Usalama wa Taifa na si Idara moja tu ndogo ya Usalama wa Taifa

Ili watekeji wawe wengi?
 
Haya mawazo sijui kwa nini mnadhani yanaweza saidia lolote? CCM haina dhamira ya kujenga taifa la haki na kufuata misingi ya demokrasia. Kama dhamira haipo, mengine yote ni kazi bure na upotevu zaidi wa pesa tu.

Ni kama Gwajima anapowakingia kifua watendaji wa vyombo eti "wakisema, watafukuzwa kazi", halafu bado anawaita "competent" utadhani maana ya kuwa competent imebadilika.

Eti anasema Rais aendelee kuwateua ila asiweze kuwafukuza kirahisi bila idhini ya kamati ya Bunge. Wakati huo huo, Bunge lenyewe wamelichafua limekuwa kibogoyo.
 
Kuunda wizara ya usalama wa ataifa iambatane na mfumo wa chama kimoja kama ilivyo china na Rusia hapo itafanyakazi kwa ufanisi. Unapoongelea demokrasia ni vema ukalingamisha hilo jambo na nchi za kidemokrasia kama ilivyo marekani na baadhi ya nchi za ulaya ili hili jambo lilete mantiki kamili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…