Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 280
- 173
Kwa muundo wa Baraza la Mawaziri la sasa naona kuna haja kubwa ya kufanya maboresho ili kuziweka pamoja sekta zinazohusiana na kupungunza wingi wa Wizara usio na tija lakini pia baadhi ya sekta kusimama zenyewe.
Kwa mfano; Kuna Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, wakati huohuo kuna Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, (Kwa nini sekta ya Habari iwe Wizara tofauti na sekta ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari?)
Kuna Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati huohuo kuna Wizara ya Muungano na Mazingira (Kwa nini sekta ya Mazingira ikae Wizara tofauti na sekta ya Maliasili?)
Kuna Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na pia kuna Wizara ya Katiba na Sheria (Kwa nini Utumishi wa Umma na Utawala Bora isiende pamoja na Katiba na Sheria?)
Kuna Wizara ya Uchukuzi, pia kuna Wizara ya Ujenzi (Hizi sekta zina uhusiano wa karibu sana, tunaweza kuziita sekta pacha, sasa kwa nini ziwe Wizara mbili tofauti?)
Kuna Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, wakati huohuo kuna Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu (Hapa naomba kuuliza, kwani tunaposema Makundi maalum tunamaanisha nini?, Kwenye Makundi maalum si ndio kuna, Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu au?, Haya yote kheri, kwenye Wizara ya Maendeleo ya Jamii, kuna kitu hapo kinaitwa Jinsia na Wanawake, naomba kuuliza tena, kwani wanawake hawapo kwenye hilo neno Jinsia?
Na unakuaje na Wizara ya Mipango na Uwekezaji na wakati huo kuna Wizara ya Viwanda na Biashara? (Unatenganisha vipi sekta ya Uwekezaji na sekta ya Viwanda na Biashara?)
Ili kuongeza ufanisi, utendaji kazi, uwajibikaji na kupunguza kama sio kumaliza kabisa muingiliano wa kiutendaji kati ya taasisi za umma, nashauri muundo huu utumike
▫️Wizara ya Mambo ya Ndani
▫️Wizara ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA
▫️Wizara ya Ustawi wa Jamii, Utamaduni, Sanaa na Michezo
▫️Wizara ya Sayansi na Teknolojia
▫️Wizara ya Elimu
▫️Wizara ya Afya
▫️Wizara ya Maji
▫️Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
▫️Wizara ya Ardhi, Mazingira na Mipango miji
▫️Wizara ya Ulinzi na JKT
▫️Wizara ya TAMISEMI
▫️Wizara ya Katiba, Sheria, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
▫️Wizara ya Mambo ya nje na Uhusiano wa Kimataifa
▫️Wizara ya Uchukuzi na Miundombinu ya Usafirishaji
▫️Wizara ya Mipango na Fedha
▫️Wizara ya Madini, Maliasili na Utalii
▫️Wizara ya Nishati
▫️Wizara ya Biashara na Uwekezaji
▫️Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana
▫️ Wizara ya Muungano, Sera, Bunge na Uratibu.
NOTE: Isiwe tu kwa Rais ajaye, bali napendekeza pia itungwe sheria ya Muundo rasmi wa Baraza la Mawaziri, sio kila anayeingia madarakani analeta utaratibu wake.