PreGE2025 Rais ajaye atumie muundo huu wa baraza la mawaziri

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wala usipoteze muda, wataalamu walishasema na kuchambua, Tanzania inapaswa kuwa na mawaziri wasiozidi kumi tu, yaani wizara zisizozidi tisa. Na hapa walipendekeza hizi wizara.
1. Waziri mkuu
2. Wizara ya Fedha
3. Wizara ya mambo ya nchi za nje
4. Wizara ya Ulinzi
5. Wizara ya Jamii
6. Wizara ya huduma
7. Wizara mtambuka

Ufafanuzi.
FEDHA (Uchumi, biashara, uwekezaji, kilimo, uvuvi, uchimbaji madini, Utalii nk)

JAMII (Vijana, watoto, kazi, michezo, mazingira, utamaduni, makazi, habari, utangazaji, sheria, katiba, mahakama, bunge nk)

HUDUMA (Afya, Elimu, Polisi, Magereza, uchukuzi, miundo mbinu, mawasiliano)

MTAMBUKA (Mambo mengine yote ambayo yanashindwa kufit kwenye wizara moja mahususi au mambo yenye kuhitaji kuunganishwa na wizara zaidi ya moja).
 
Hii sasa ufanisi utakua mdogo sana, nchi zetu bado zina changamoto nyingi huwezi lundika sekta nyingi sehemu moja
 
Hii sasa ufanisi utakua mdogo sana, nchi zetu bado zina changamoto nyingi huwezi lundika sekta nyingi sehemu moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…