Rais ajiuzulu, huduma ya kununua LUKU imekwama tena leo Juni 20, 2021

Rais mbona ni wa mbali sana? Kuna bosi wa Tanesco, na wengine
 
Kwakweli sijawahi kupata hasara katika biashara zangu kama hizi ninazopata tangu awamu hii iingie madarakani!

Leo mimefungua saluni kama kawaida siku ya jumapili wateja ni wengi.Haraka nikasema ninunue umeme niwahudumie lakini nimejaribu zaidi ya mara 10 imeshindikana!

Kwakweli pamoja na kuwa nilikuwa na mpiga vita Magufuli lakini hali hii sijawahi kuona! Kwakweli kutenda kosa sio kosa bali kurudia kosa! Kwa hali hii ni wazi kwamba Rais ameshindwa kazi na ameonyesha udhaifu kwa kushindwa kuwachukulia hatua wahusika! Akiwa kama kiongozi mkuu wa nchi jambo hili halikupaswa kujirudia tena kwa mara ya pili na hii inaonyesha alishindwa kuchukua hatua hapo awali na sasa ni vyema akajiuzulu tupate kiongozi mwingine!

Mbaya zaidi tunaoathirika ni sisi raia wanyonge.Kwa hali hii serikali imeshindwa kazi na haina uwezo wa kusimamia kazi zake hivyo tunaomba iondoke!!
TANZANIA bado tupo 2G, wenzetu wapo 5G, angalia hata malipo ya Serikali kila siku utaambiwa hakuna mtandao, mara sijui control number haitoki, yaani JIWE alitukimbiza pahakla ambapo miundombinu yetu bado kabisa.
angalia mambo ya NIDA kutoa ID wameshindwa, eti mtu anapewa namba kwenye kikaratasi, hii nchi kwakweli daa.
 
Bila kumfukuza kazi Kalemani haitaweza kuiweka Tanesco sawa
 
funga saluni uza machungwa hayatumii umeme
Umekaa kwa shemeji yako unajamba na kula bure, unafikiri maisha ni mtelezo?

Unajua amekosa faida kiasi gani kwa siku ya leo? Hiyo familia yake utailisha wewe?

Ni saluni ngapi zimefungwa nchi nzima? Mashine za kusaga nafaka, viwanda, nk

Huko kote pesa zinapotea kizembe tu kwa sababu ya Luku kugoma.

Halafu baadae muanze kulia lia mnataka kodi? Kodi itoke wapi?

Jinga we! Na uhame hapo kwa shemeji yako!
 
TANZANIA bado tupo 2G, wenzetu wapo 5G, angalia hata malipo ya Serikali kila siku utaambiwa hakuna mtandao, mara sijui control number haitoki, yaani JIWE alitukimbiza pahakla ambapo miundombinu yetu bado kabisa.
angalia mambo ya NIDA kutoa ID wameshindwa, eti mtu anapewa namba kwenye kikaratasi, hii nchi kwakweli daa.
Hata kwenye BIMA ya afya utasikia system inasumbua hapo utasubilia dawa mpaka ujute!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Kwakweli sijawahi kupata hasara katika biashara zangu kama hizi ninazopata tangu awamu hii iingie madarakani!

Leo mimefungua saluni kama kawaida siku ya jumapili wateja ni wengi.Haraka nikasema ninunue umeme niwahudumie lakini nimejaribu zaidi ya mara 10 imeshindikana!

Kwakweli pamoja na kuwa nilikuwa na mpiga vita Magufuli lakini hali hii sijawahi kuona! Kwakweli kutenda kosa sio kosa bali kurudia kosa! Kwa hali hii ni wazi kwamba Rais ameshindwa kazi na ameonyesha udhaifu kwa kushindwa kuwachukulia hatua wahusika! Akiwa kama kiongozi mkuu wa nchi jambo hili halikupaswa kujirudia tena kwa mara ya pili na hii inaonyesha alishindwa kuchukua hatua hapo awali na sasa ni vyema akajiuzulu tupate kiongozi mwingine!

Mbaya zaidi tunaoathirika ni sisi raia wanyonge.Kwa hali hii serikali imeshindwa kazi na haina uwezo wa kusimamia kazi zake hivyo tunaomba iondoke!!

E0NhMwdXIAAW0HL (1).jpeg
 
Huna bajeti umeme wa buku buku kila siku utaendelea kulalamika hadi yesu atarudi. Weka umeme wa kutosha default zipo siku zote. Hata Tanesco wakirekebisha bado kesho utakuja kulalamika tu.
Bajeti yake ya Luku wewe haikuhusu.

Hata akinunua Luku ya mia, sio hoja hapa.

Umeme unatakiwa kuwa wa uhakika masaa 24.
 
Jamani ongezeni kelele tu hadi aachie kiti, maana wengi sana Bi Mkubwa hata hawaelewi anaendaaaaa au anarudi!??? Hata ikitokea hitilafu ya umeme au maji mwako, unganisheni doti tupate ushahidi wa kutosha, sawa!???
 
Back
Top Bottom