The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
Wakati wa Magufuli niliwahi andika hapa kama Magufuli anao watu wa kumwambia ukweli na akawasikiliza, nilitoa mfano wa Fidel Castro alivyokuwa anaogopwa na watu wengi sana lakini walikuwepo watu wawili walikuwa wana uwezo wa kumwambia ukweli Raul Castro mdogo wake na Comrade Che Guevara. Hawa wawili walikuwa na uwezo wa kumwambia ukweli na makosa yake bila kupepesa macho na akawasikiliza.
Juzi Rais Samia kasema madini yachimbwe kwenye mbuga, cha muhimu hela. Hii kauli si sahihi kabisa tena sio sahihi kutoka kwa Rais wa nchi.
Rais alipaswa kwanza kupata elimu ya kutosha kuhusu uchimbaji wa madini na athari za mazingira, lakini la muhimu zaidi alipaswa kuniuliza kwanini Viongozi kabla yake wote walisita au kukataa kutoa vibali vya kuchimba Mbugani?
Je hata kama tukikubaliana na Rais cha muhimu hela, kwani Rais hajui utalii ndo unaingiza hela Tanzania kupita madini?
Rais hajui au hana ushauri wa kumwambia kuwa athari za kimazingira huko Mbugani zinaweza moja Kwa moja kuathiri utalii na kupunguza mapato kuliko hata kuongeza hayo mapato?
Rais hajui kuwa hayo makampuni ya madini huwa yanaahidi sana mambo mengi mazuri lakini mwisho hushindwa kutekeleza kuanzia Kodi hadi taratibu za kulinda hayo mazingira? Kampuni ya madini inaweza sababisha sumu kwenye vyanzo vya maji ya wanyama hadi binadamu, na hili sio nadharia imewahi tokea na ushahidi upo.
Madini yanaweza chimbwa yakaisha na mapato ya maana yasipatikane, imeshatokea..na haitakuwa la ajabu ikitokea tena.
Mbuga za Wanyama zilzopo Tanzania haipatikani tena kwingine duniani, ni urithi wa dunia. Mbuga kama Serengeti ina Wanyama Wengi kupitia Mbuga yeyote duniani, hii Peke yake ni dhahabu kuliko dhahabu yenyewe.
Mbuga kama Selous ukubwa wa Ardhi tu ni zaidi ya nchi ya Belgium, halafu leo tunaanza tena kuruhusu uharibifu wa mazingira Mbugani mradi ipatikane hela? tuharibu kuku anaetotoa mayai ya dhahabu ili tukatafute mayai mengine tumboni?
Rais akikosea aambiwe hadi aelewe.