Rais amepotoshwa, si kweli kuwa mkoa wa Dar unachangia 80% ya pato la taifa. Kwa sababu;


Mimi najuwa anamiliki hisa za makampuni mengine mengi tu.....sio mikate na lambalamba tu
 
Kodi kutoka mishahara ya Wafanyakazi wa Serikali wote nchini, inakatwa Hazina na kubakia huko huko Dsm!

Hata imports karibu zote zinapitia Dar hasa bandarini na kama mjuavyo kwamba kwa kiasi kikubwa sisi kama nchi tunanunua zaidi kuliko kuuza nje. Kwa hiyo kodi karibu ya imports zote nchini inalipwa Dar. Of course Dar pia ina viwanda vingi zaidi kuliko mkoa mwingine wowote.Ni ukweli usiopingika kwamba Dar ndio hub (of course ni makosa pia nchi kutegemea sehemu moja kwa kila kitu) ya uchumi wa nchi yetu japo sidhani kama ni sahihi kusema kwamba Tanzania inaitegemea Dar kwa asilimia 80% kiuchumi hata kama mapato inayokusanya Dar ni asilimia 80% ya mapato yote nchini. Kwani kwa kusema hivyo ni kama vile unamaanisha kwamba imports zote ni kwa ajili ya soko la Dar pekee kitu ambacho si sahihi.

Kuna tofauti kubwa kati ya kukusanya kodi/mapato na kipi kilichozalishwa mpaka hiyo kodi ikapatikana. Sheria kwa mfano, hainizuii mimi kulipa kodi Dar na nikafanya biashara zangu say kwa 80% mkoani. Ninachotakiwa kufanya ni kulipa kodi TRA, ni office ipi ya TRA niliyolipa it doesn't matter. So kodi inayolipwa Dar haireflect shughuli za kiuchumi za Dar peke yake bali ni za nchi nzima.
 
Hii ni aibu kwa raisi wetu kwamba yeye hajui pato la taifa linatoka wapi au Ana wasaidizi vihiyo wanampa ripoti za uongo, ripoti ya BOT inaonyesha Kuwa zaidi ya asilimia 45 ya pato la taifa linatokana na madini ya dhahabu, je dar wanamigodi? Au mtuambie pato la taifa Ina maana gani? Mzunguko wa hela au balance za hela Kwenye Malawi ya benki Ndio mnasema pato la taifa? Halafu tunasema Huyu mtu ana shahada ya uchumi, aibu tupu,,,!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…