Tuesday, September 1, 2009
libeneke la tanzanite account ya CRDB
Habari za kazi ndugu Michuzi,
Natumai unaendelea vyema kabisa na shughuli za kila siku.Kuna jambo nataka ushirikiano na wasomaji wa blog ya jamii. Mie ni mwanafunzi na nasoma India. kama inavyojulikana India hawaruhusu kubeba boxi ukiwa denti. Hivyo wengi tunategemea pesa za kujikimu kutoka kwa Wazazi/Walezi ama Wafadhili mbalimbali.
Kuna njia nyingi za kutumiwa pesa lakini wengi tuliona ni muhimu kuwa na account ya Tanzanite(CRDB),mwanzoni nilikuwa nasikia watu wengi wakilalamika kwamba account hii inasumbua, haswa linapokuja swala moja kwamba mtu anaambiwa ame overdraw hivyo account yake ina deni.
Kuna watu wameacha kutumia baada ya kuambiwa wana madeni makubwa wanadaiwa. Je, naomba kuuliza kwenye account kukiwa na millioni 1 bank inaweza kukupa millioni 2? haswa ukifikiria huduma yenyewe tunatumia ni ya Tembocard?
Kwa kawaida viwango vya makato baada ya Transaction huwa vinajulikana lakini kwa bank hii ya CRDB mwisho wa siku mtu unaona maluweluwe na kweli nami wameniambia wananidai hivyo wamekata pesa zote ambazo nilipaswa kupata na bado wanasema nadaiwa 27,000 ya Kitanzania!
Swali muhimu ni hivi Tanzanite account inatakiwa iwe na 5000 rupees ama 100usd na si chini ya hapo?? Je, inakuwaje mtu ana draw pamoja na hizo 5000rupees na zaidi? tuseme machine zina matatizo ama mfumo mzima una matatizo ama wafanyakazi wa CRDB bank wana mbinu zao?
Maana kama mchezo ni huu watakuwa wanatumaliza sie vijana tunaotoka familia za chini. Je wadau tuendelee na Huduma hii ama turejee kwenye West union,money gram ama bank zingine za kimataifa kukwepa hatari hizi?
Mdau aliyelizwa India
© Michuzi | Tuesday, September 01, 2009
|
Permalink |
Mtumie Rafiki Yako |
Maoni: 24
- Tarehe Tue Sep 01, 01:37:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
Kimei wafafanulie vijana.
-
- Tarehe Tue Sep 01, 02:03:00 PM, Mtoa Maoni:
tzforchange
KIUHALISI NCHI MASIKINI NA NCHI TAJIRI HUDUMA YA JAMII NI TOFAUTI. MFANO TANZANIA UKIENDA KUPATA HUDUMA OFISI YA SERIKALI AU SHIRIKA LA UMA MUHUDUMU ATAPENDA AKUONGEZEE VIKWAZO ILI UONE UGUMU WA KUPATA HIYO HUDUMA NA INAFIKIA KWAMBA MWANYA WA RUSHWA UNAPATIKANA.NCHI ZILIZO ENDELEA MFANYA KAZI ANAHAKIKISHA ANAMUHUDUMIA MTEJA KWA HAKI NA KWA URAHISI WA HALI YA JUU . AKIKOSEA KIDOGO ANA HAKI YA KUFUKUZWA KAZI. KWAHIYO MPAKA SASA TAZANIA KWA UFANISI WA WAFANYA KAZI IKO NYUMA KIASI KIKUBWA AJABU. KUNA WATANZANIA WANAPESA ZA HAKI WALIO NJE YA NCHI LAKINI HAWARUHUSIWI KUFUNGUA ACCOUNT WAKIWA NJE PESA ZINAPOTEA HIVIHIVI. ZAMBI YETU YA ASILI NIKUONA WATU HAWAFANIKIWI. NAKARIBIA KUNYOOSHA MIKONO TZ4CHANGE INAKUWA NGUMU SANA
-
- Tarehe Tue Sep 01, 02:36:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
CRDB hawaruhusu overdraft ila kwa huduma ya visa huwa unaweza ukadraw ukalipwa na visa hlf wenyewe wakati wa settlement usiku akawalipa visa so visa huwa na ile initial balalnce ,sasa kama unaweza kuwatyme unaweza ukadraw benki mbili tofauti at the same tym ukia nje kwa hiyo unapata over drat ila ukija baadae kuweka hela wanakata.Mimi nimesha tumia sana hizo na shukuru siku ya mwisho nataka niwapige overgraft ya paundi 200 system ikagoma ikabidi nibaki kuwa mteja wao hivi hivi ningelamba hiyo ningeingia mitini.siunaju a wabongo kulipa deni ukimkopesha tu anainngia mitini kwa mbongo over draft haifai iwe ulaya au bongo wabongo WEZIby nature
-
- Tarehe Tue Sep 01, 02:38:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
nakushukuru sana mdau wa india maana nilikuwa mbioni kumuuliza mzee wa libeneke aende kwa wataalamu wa CRDB aniulizie kama nikichukua pesa kupitia saving account kwa VISA electronic huku india nitakatwa kiasi gani kwa kila nitakapo toa pesa hapa india kwenye benk km icici,citi bank,na benk zingine
pia nilitaka kujua ni ammount gani wanatumia nikitoa pesa yaani kutoka kwenye madafu kuja kwenye rupees wanatumia kiwango gani? maana pesa huwa inabadilika mara 1rps =27tshs kwahiyo nilitaka kujua hilo kwakuwa kuna ndg zangu wanatumiwa pesa kwenye account yangu na tunapata shida hata tukiangalia exchange rate kwenye net nakuomba sana anko michuzi unisaidie kwa hili
mdau india hyderabad
nakupa e-mail yangu kwa jibu jjozzee@yahoo.com
-
- Tarehe Tue Sep 01, 03:28:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
Tanzanite account ni wezi kweli,mie nilifunga account yao baada mwezi tu,walikua wanakata hela bila ya ridhaa yangu,muwe macho sana.
-
- Tarehe Tue Sep 01, 03:40:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
Doh nashukru kwa hizi comment chAche tu zimenipa mwangaza wa kutokufungua hii account. Tanzania ni moja ya nchi nilioamua kukata tamaa nayo. Hakuna haki kwa chochote kile....Kuna mengi ya kuongea ila hapa si uwanja wake. Asante wadau waliotoa mwangaza kiasi.
-
- Tarehe Tue Sep 01, 03:41:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
Michu kwanini usimshute kigogo au mtu wa CRDB ajibu swali hili maana linatusumbua wengi, na mimi niko kwa Obama kila nikicheki balance nakuta imeshuka
-
- Tarehe Tue Sep 01, 04:45:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
CRDB Tanzanite account ni matapeli wala msijihusiche nao, Mtapoteza pesa zenu bure, kama unataka kuwapa pesa zako bure basi fungua account nao.
-
- Tarehe Tue Sep 01, 05:26:00 PM, Mtoa Maoni:
mchagga halisi
ndugu zangu jaribuni kutumia HSBC BANK kutoa hela zenu utakua na uhakika zaidi kama umeliwa au vipi kwa sababu wanaonyesha balance kwa Tshs.so mapema tuu kabla hujatoa utatua iko kiasi gani,pia hawana makato kibao kama bank nyingine.
-
- Tarehe Tue Sep 01, 05:35:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
Malengo ya hii akaunti ni mazuri sana. Tatizo kama ilivyo katika mambo mengi Tanzania, hakuna watekelezaji wenye kujua wanachokifanya.
Hii huduma ingetusaidia sana sisi tulio nje, tena ingetufanya tupeleke hela zaidi nyumbani kuliko ilivyo sasa.
CRDB wangekuwa na kipeperushi kidogo, kwenye tovuti yao pembeni ya Application Form kinachoelezea Terms & Conditions zote pamoja na Questions & Answers za maswali yote wanayoulizwa na wateja kila siku kuhusu Tanzanite account haya malalamiko yangepungua kwa 99%.
Ushauri wa Bure kwa Ms Jenifer Tondi na timu yako hapo CRDB.
- Tarehe Tue Sep 01, 05:53:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
Tumia western union, achana na longolongo za wabongo. Pesa yako inakupa tabu kisa nini?
- Tarehe Tue Sep 01, 06:19:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
moneygram ndiyo the cheapest way,western union huduma zao ni ghali.
- Tarehe Tue Sep 01, 07:19:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
Asante mdau wa India kwa kutufahamisha kuhusu Tanzanite Account. Nilikuwa nafikiria kufungua hiyo Account lakini sasa basi.
- Tarehe Tue Sep 01, 07:20:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
MIMI NIKO CANADA NATUMIA WASOMALI KUTUMA PESA BONGO NA KUJA HUKU HUWEZI KUAMINI JAMAA WAKO SAFI SI MCHEZO.ACHANENI NA HIZO BENKI ZA KIBONGO NI LAANA
- Tarehe Tue Sep 01, 08:34:00 PM, Mtoa Maoni:
Anonymous
E bwana mdau wa India ...bora wewe umepata moyo wa kuirusha hii kwa michuzi!
Kwanza nchi yetu hatubadiliki ..wao CRDB wanafanya jitihada za kutangaza Tanzanite na kula hela za bure kabisa za wenye Hisa kwa kuwatafuta wateja bila kuweka mipango madhubuti ya kuwatunza...
Mimi nina hiyo account lakini kwa sababu ya mizengwe nimeshidwa kuanza kuitumia kabisa ..nilikuwa na maswali ambayo yangejibiwa then ningeanza kutumia account yangu lakini jitihada zangu zimekuwa hazizai matunda ikiwa ni pamoja na kumuandikia email Jennifer Ntondi!!
Swala la mawasiliano nyumbani hata kwa watu wenye exposure na shule zao bado ni tatizo ..kazi umepewa ni kwa nini usiifanye?
Ngoja nimuulize Jennifer kwa sababu ndi ye mwenye dhamani ya Tanzanite ..em niambie churn rate per month ya TANZANITE...naona inazidi hata subscription rate....
Em tujifunze ..tuwaelemishe wateje vema ..ili waweze kuweka pesa zao nyumbani kwa maendeleo ya nyumbani!!
Jamaaaaaaaaani Tanzania tubadilike!! nyakati zile za zamani zimepita ....
CRDB WE NEED CHANGE NOW!
- Tarehe Tue Sep 01, 10:04:00 PM, Mtoa Maoni:
WAKUTI
Asante sana mdau kuleta mada hii. Mimi wameniliza euro 1000 hivi hivi hati hawajui zimeenda wapi. sasa sijui kama bank yenyewe ndo wezi au wafanya kazi ndo wezi. sisahau walivyonisumbua nilipokwenda kuchukua pesa pale azikiwe yaani mpaka nimeenda kuongea na manager ndo wakanipa huku euro 1000 zikiyeyuka kisha wamebakiza euro 100 kama balance nami nimewaachia sitoweka pesa kwao tena hawa jamaa.