Rais ampe nishani Charles Kimei

kikwete akutaka kumpa mwenyewe kwa sababu zake binafsi
mbona huo usalama wa taifa haujamshauri kuhusu peter noni na wengine wengi tu.....
 
Pesa nyingi halali zilipitia CRDB kwenda kufanya kazi haramu. Ukisikia fedha za EPA...........kwa njia moja au nyingine utakuta CRDB imejihusisha. Sasa hiyo Nishani ya nini??
 

Na ndio nchi nyingi wamekuwa na msemo kwa waTanzania kuwa akili zao ni evereji .
 

Huyu Charles si Mswahili kama usemavyo, katoka pwani gani ya Afrika Mashariki mpaka awe Mswahili? Ungesema huyu ni mTanzania, labda ingekuwa sawa, kama ni mTanzania, lakini uSwahili? hana, hata chembe.
 
Pesa nyingi halali zilipitia CRDB kwenda kufanya kazi haramu. Ukisikia fedha za EPA...........kwa njia moja au nyingine utakuta CRDB imejihusisha. Sasa hiyo Nishani ya nini??
Kimei ni mtaalamu wa kuangalia fedha atazipata wapi. Sasa kaletewa hela nyingi tuuazikatae??.
 
Katika benki zenye huduma mbovu Tanzania na kauli chafu kwa wateja hasa kutoka kwa tellers na wahudumu wengine CRDB inaongoza.

Unaweza ukapata faida kwa sababu huduma zako zina monopoly lakini siyo bora kwa maana ya customer care. Kilichomshinda Kimei ni kazi za kupeana pale CRDB. Hii inasababisha nidhamu ya kazi inapotea na watu hawaheshimu walio juu yao.

CRDB ni rahisi sana kukuta mtu,mke wake na watoto wawili wote wameajiriwa pale,kitu ambacho watu wenye ethics za biashara hawawezi kufanya. Mfano Kuna kitengo kimoja kina watu 14 na kati ya hao watu 4 ni ndugu wa kuzaliwa na watu 2 ni binamu zao. Jumla ni watu 6 ndugu ndani ya kitengo kimoja. Kimei mwenyewew ameonyesha mfano mbaya kwani watoto wake kama wawili wameajiriwa pale CRDB,mmoja headquarters mwingine alikuwa pale UDSM. Huyu wa UDSM alikuwa na sauti kwa waajiriwa wenzie na wateja kuliko hata Branch Manager. Akianza kufokea wateja pale,utadhani ni nyapara wa magereza na wafungwa wenzie kumbe anawafokea wateja.

Suala jingine ni kuwa unaweza kupata faida kwa kufanya biashara ambazo ni haramu hata kama kampuni yako ni halali. Mfano CRDB ilitumika kuhamisha pesa kutoka BOT bila hata kuhoji uhalali wake huku Anti-Money Laundering Act ikiitaka kufanya hivyo. Barclays Bank afadhali walihoji na kukataa baadhi ya pesa,lakini hii benki inayoongozwa na "mzalendo" ilipokea bila hata kuhoji.

Nakubali kuwa Kimei ni msomi na ana uzoefu wa kutosha wa mambo ya fedha. Amekuwa Director wa usimamizi wa mabenki kabla ya nafasi aliyonanyo sasa. Siamini kama kilichofanyika BOT alikuwa hajui au watu wa chini yake walimzunguka. Kama kweli ni mzalendo na anaitumia elimu yake vizuri angezuia ile pesa kuibiwa. Tujiulize ni pesa kiasi gani ambayo imewahi kuibiwa hatujagundua?


I had rather die poor, other than stealing from Tanzanians.
 

Mwaka huu mengi yataonekana, hapa mkuu anatoa fadhila ili mradi tu mwakani mkuu arudi. Kapewa nishani kwa ufisadi mzuri alioufanya kwani kwa sehemu kubwa pesa za EPA ambazo ndizo zilimweka jamaa kwenye kiti. Nafikiri kuna jambo lililofichika hapa kwa ajili ya mwakani ndo maana kapewa hiyo nishani ili alifanikishe. Kama mafisadi ndo wa kupewa nishani, basi tutegemee wengine kama kina Chenge, mawaziri wote na viongozi wote wanaokabiliwa na kashfa ya ufisadi, kinazombe, mwenye asili ya ki asia na wengine kama hao kupewa nishani, JAMANI SIJUI FAMILIA YA BALALI IKADAI NISHANI YAO, au??????????????. jk hasipo wapa yuko atarini.

HUUUUUUUUUUI tumeisha.
 
....Bado Tanesco jamani...Shirika linapumulia mashine naona Dr. Idrisa Rashid nae anastahili nishani kwa kuchemka na Tanesco yake!!!
 
Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Mimi nimefunga account yangu ya CRDB kwa sababu ya usumbufu wao na sio kwa kupenda. Tumepe nishani ya aina gani? Labda ungelipendekeza, isipokuwa siyo ya ubora wa huduma za bank
 
kikwete akutaka kumpa mwenyewe kwa sababu zake binafsi
mbona huo usalama wa taifa haujamshauri kuhusu peter noni na wengine wengi tu.....
Haya mambo hata ukiyafukia chini kiasi gani..yanaibuka here and there as a reminder that justice has to be done.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…