Rais anapodanganya Umma na kulialia eti Umasikini...

Wakuu zangu,

Nitarudia kusema kwamba tujenge nchi kwa kukosoa mambo anayoyafanya rais kwakumwelekeza yapaswayokwanikulinganisha matumizi ya vitumbalimbali pia inaonyesha ifinyu wa kufikiria kwetu.

Kwa mfano mkazi wa Marekani anaweza kuwa akilipa kodi ya pango dollar 800 hadi Elfu moja na kawa hana fedha za kulipa masomo yake ambayo ni chini kabisa ya kiwango anacholipia pango la crib yake. Matumizi ya Usafiri yakawa juu ya chakula au mavazi yake, hii haina maana mtu huyo ni mchovu wa kufiki.

Umaskini ama Utajiri wa mtu, nchi haipimwi kwa vigezo hivyo hata kidogo.
 

Heh! Makubwa
 
Politicians wetu naona wamekuwa muflis siku hizi. Wakati watu wanataka kuona action wao bado wamejisahau kwenye kutunga hadithi. Hizi simulizi za hadithi zitaisha lini?

Ukweli ni kuwa hatujaamua kufanya kweli maana uwezo tunao. Priorities zetu pia zinawekwa sehemu zisizo na tija. Kwa mfano hizi safari za wakubwa zisizoisha zinaongeza tija gani kwetu?
 
Kishoka, cha ajabu ni kitu gani hapa?kwani wewe humjui JK kilasiku ni kuombaomba na kudanganya danganya iwe kwa Watanzania ama wasio Watanzania.
 
Heh! Makubwa
"Makubwa wala sii kidogo. Unajua nimefika hapa Bongo ndio nimepata darsa haswa la nchi inakwenda wapi. Umaskini wetu sii wa mali ila ni hadi akili zetu hivyo ni tegemeo langu nyie wasomi ambao mna mwamko zaidi muijenge fikra mpya badala ya kuburuza buruza hoja.

Tanzania ni nchi maskini, kama Mmasai mwenye ng'ombe elfu tatu akivaa lugeba na viatu vya matairi. Sasa unapotaka kumkosoa Mmasai usianze na habari za Mmasai kuwa na simu ya mkono ama kapanda ndege wakati huku kwao hana kitu, hamtaelewana hata kidogo. Mpe darsa linalohusiana na tamaduni yake kisha ukairekebisha kiustaarabu pale inapopwaya.

Kikwete ana makosa mengi sana ya kiuongozi ambayo nina hakika tukianza kuyataja hapa tutajaza kurasa kibao lakini ujenzi wa hoja ya kile anachotakiwa kukifanya, yaani matakwa yetu, nadhani ndio inatakiwa kuwa mbele ya ujumbe wowote ule. Mkosoe kisha mpe darsa la kipi kinatakiwa kufanyika na sii maswali juu ya maswali.

Tunawafahamu wana siasa hawakosi majibu, Obama amekusanya mabilioni kwa uchaguzi wake, leo tukitaka kumchambua kwa kima alichoweza kukusanya kwa uchaguzi na tukalinganisha na umaskini wa watu waishio South East Chicago basi tutakuwa tunampoteza kabisa! Kila fedha ina umuhimu, majukumu na matumizi yake kulingana na wakati wake.

Tanzania yetu mfumo wa ukusanyaji fedha ni mbaya sana. Matumizi ya fedha za nje na ndani ni vichekesho vitupu yaani asili ya Mwafrika, tunakimbilia kujenga majumba, kuendesha magari makubwa, kuhonga na kutafuta sifa za U Pedejee mitaani kuliko future ya maisha yetu. Mfumo wa maisha ya Mwafrika ni siku kwa siku iwe leo tunamtazama Kikwete tofauti na jamii yenyewe jamani.

Kila taasisi ya Kimataifa iliyokuja hapa wameshindwa ku deal na sisi wala hujafika Ikulu. Taasisi zote za UN wameinua mikono, mashirika mengi ya nje yamejikata kwa sababu ya rushwa iliyokufuru, kila Mtanzania leo hii ni striker wanatafuta magoli na sifa za ushindi.

Mkuu wangu Rev. Tanzania imeharibika kiasi kwamba haiwezi kurekebishwa pasipo kuwa na Dikteta, Mawazo yenu yanaweza kuwa mazuri sana lakini yote yanajenga Upole na huruma kwa kiongozi kitu ambacho hakiwezi kuondoa adha yetu. Na Kikwete anaonekana mbovu kwa sababu anajaribu kuwaridhisha wananchi wenye hulka ya ubadhilifu, ndio maana kodi yetu hukusanywa kabla mtu hajafanya biashara! Uliona wapi mkuu wangu ati kodi ya mapato inakadiliwa kabla hujafungua biashara. Ukitengeneza bilioni au upate hasara, hiyo kodi yao imeshalipwa kwa mwaka ama miezi sita.

Watu wana majumba (waliyopewa na serikali ya Mkapa) leo wakikodisha kwa dola 3,000 kwa mwezi na hawalipi kodi ya mapato hata ndululu. Nyumba ambazo kwanza zilikuwa za viongozi wa mashirika haya haya tunayoyapigia kelele leo kujenga ama kununua. Tumerudi kuwa wapangaji na ujenzi wa nyumba yoyote mpya tunashtuka kwa thamani ya majumba wanayojengwa!

Tujiulize sisi wenyewe tumeishia wapi kudai majumba yaliyo uzwa na Mkapa? Tumefikia wapi kudai asilimia katika madini, ardhi na mali zetu zinazoibiwa kila siku kwa misaada ya Watanzania wenyewe. Kila Waziri ana share katika mashirika yote makubwa yanayoendesha uchumi wa nchi. Kila mwalimu ana shule yake, kila daktari ana zahanati yake, kila mtaalam ana kitengo chake private cha kazi nje ya ajira yake. Na hakuna kazi isiyokuwa na malipo hata iwe kupatia TIN namba kwa makusanyo ya kodi ya serikali, yaani mtu ananyimwa namba ya kujisajiri kulipa kodi hadi atoe kidogo. Utamwongoza kondoo zizini kama Kondoo na sii kama mbuzi!

Jamani mwee... acheni jamani msifanye mchezo!"
 
i always get annoyed to hear when he speak on radio or television, i wish majority of tanzanias would know that he might have good smile, he might be talking about people problems regularly, he might have nice looking face but he does not have what it takes to be a president who can make country prosper!

apart from his big smile and handsome face he has no plan to make this country prosper may b we are paying the price as during the campaign, former president mkapa was making funny of oppisition presidential ugly faces, did we choose the handsome?
 

Wealth is a function of Consumption, saving and investment. from economics simplified

Lets start from here......
 
Wealth is a function of Consumption, saving and investment. from economics simplified

Lets start from here......
The thing is... such simplification does not apply in the same measure to a Masai!
 

And yet we have another five years term with him. Atapona mtu kweli????
 

Usemayo Gembe ni kweli jamaa anaongea vitu ambavyo huwezi amini kwani vinaongewa na msomi na pili ni rais wa nchi huyo. Jamaa keshatutia aibu kibao lakini jamaa nafikiri huwa wanatucheka kuwa badala ya kumchagua mtu kwa kuangalia vitu vya msingi sisi tunaangalia sura. Haya wale waliongalia sura itende sasa iyo sura.
 
Ni hasara kubwa kwetu. Kiasi cha dola za Marekani milioni 15 ni nyingi kwa nchi masikini kama Tanzania lakini tumeamua kuwa ukarabati huo utakuwa umekamilika katika muda mfupi.

Rev,
Nakumbuka niliwahi kuandika kuwa huyu mheshimiwa JK yeye anafikiri kazi ya raisi ni kuomba misaada, na inaelekea hana hata aibu kuwa omba-omba.

Hivi ni lini ataacha hii aibu anayoipaka nchi kwa kuzunguka dunia nzima akitumbua halafu akiambiwa aongee ni kulalamika tu na kuomba misaada?

Shame on you JK.
 


kweli kabisa...ndo maana hatulii nchini...
 
Nimechoshwa na hili neno Tanzania eti ni nchi masikini. Nchi masikini ipi imejaliwa rasilimali zote tulizonazo kama ardhi nzuri yenye kufaa kwa kila aina ya mimea, madini ya kila aina ambayo hata nchi zingine hazina, mito mikubwa, maziwa na bahari. Utaiita hiyo nchi masikini kweli au tunadanganyana tu? Misri ni nchi jangwa sana wanatumia maji yanayotoka Ziwa Victoria angalia utajiri wao. Sisi tumeshindwa hata kutumia robo ya maji ya Maziwa na Mito tuliyonayo hapa kwetu achilia mbali madini na Bahari.
"Something must be wrong within our heads".
 
Rev.Kishoka,

..naomba kutoa dokezo.

..msaada aliotoa Gaddafi ni shilingi bilioni 1.5.

..wanadai fedha hizo zitajenga nyumba 200.

..sasa hebu linganisha na bilioni 2.5 zilizotumika kujenga nyumba moja ya Gavana wa BOT.

..halafu linganisha na gharama za kumpeleka JK na ujumbe wake kwenda kumshukuru Gaddafi huko Libya.
 
The irony is, sisi tuna utajiri wa maliasili mpaka zinafurika, literaly speaking maji mengi mpaka mito inafurika, utajiri huo.

Wenzetu Libya hawana maji lakini utajiri walio nao wanautumia vizuri.

Hapa issue kubwa si umasikini, bali umasikini unatokana na nini.
 
Matatizo ya Watanzania na Umaskini wao sasa vinatokana na maamuzi yao wenyewe. Waliamua 2005 kuwa na leadership mediocre na naive. Utamaduni wa kijiweni na mazungumzo ya juu juu tu bila uchambuzi makini wa kina.

Watanzania mwaka wa 2005 wangeweza kumchagua Profesa Ibrahim Lipumba au Freeman Mbowe; lakini wakakimbilia mediocrity kwa "kishindo". We deserve this punishment now!

Anyway, Tanzanians have another chance this October to show if they have learnt from past mistakes. Let us see if CHADEMA can nominate someone like Professor Mwesiga Baregu. He certainly can't make such shameful analysis of our economic situation as was done in Tripoli, Libya a few weeks ago.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
kutangulia kusoma madrasaat badala ya elimu inayomfungua mtu kichwa kwanza ni tatizo, elimu aliyosoma kwa kiasi imeathiliwa na alimu ya awali ile ya kukaririshwa mambo
 
asili ya kabila lake siyo watu wa kufikiri, kuchambua na kuboresha bali ni wa kucheza ngoma mno kuliko kazi,....wakilima mchicha wao kwao ni shamba kubwa mnooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…