"Makubwa wala sii kidogo. Unajua nimefika hapa Bongo ndio nimepata darsa haswa la nchi inakwenda wapi. Umaskini wetu sii wa mali ila ni hadi akili zetu hivyo ni tegemeo langu nyie wasomi ambao mna mwamko zaidi muijenge fikra mpya badala ya kuburuza buruza hoja.
Tanzania ni nchi maskini, kama Mmasai mwenye ng'ombe elfu tatu akivaa lugeba na viatu vya matairi. Sasa unapotaka kumkosoa Mmasai usianze na habari za Mmasai kuwa na simu ya mkono ama kapanda ndege wakati huku kwao hana kitu, hamtaelewana hata kidogo. Mpe darsa linalohusiana na tamaduni yake kisha ukairekebisha kiustaarabu pale inapopwaya.
Kikwete ana makosa mengi sana ya kiuongozi ambayo nina hakika tukianza kuyataja hapa tutajaza kurasa kibao lakini ujenzi wa hoja ya kile anachotakiwa kukifanya, yaani matakwa yetu, nadhani ndio inatakiwa kuwa mbele ya ujumbe wowote ule. Mkosoe kisha mpe darsa la kipi kinatakiwa kufanyika na sii maswali juu ya maswali.
Tunawafahamu wana siasa hawakosi majibu, Obama amekusanya mabilioni kwa uchaguzi wake, leo tukitaka kumchambua kwa kima alichoweza kukusanya kwa uchaguzi na tukalinganisha na umaskini wa watu waishio South East Chicago basi tutakuwa tunampoteza kabisa! Kila fedha ina umuhimu, majukumu na matumizi yake kulingana na wakati wake.
Tanzania yetu mfumo wa ukusanyaji fedha ni mbaya sana. Matumizi ya fedha za nje na ndani ni vichekesho vitupu yaani asili ya Mwafrika, tunakimbilia kujenga majumba, kuendesha magari makubwa, kuhonga na kutafuta sifa za U Pedejee mitaani kuliko future ya maisha yetu. Mfumo wa maisha ya Mwafrika ni siku kwa siku iwe leo tunamtazama Kikwete tofauti na jamii yenyewe jamani.
Kila taasisi ya Kimataifa iliyokuja hapa wameshindwa ku deal na sisi wala hujafika Ikulu. Taasisi zote za UN wameinua mikono, mashirika mengi ya nje yamejikata kwa sababu ya rushwa iliyokufuru, kila Mtanzania leo hii ni striker wanatafuta magoli na sifa za ushindi.
Mkuu wangu Rev. Tanzania imeharibika kiasi kwamba haiwezi kurekebishwa pasipo kuwa na Dikteta, Mawazo yenu yanaweza kuwa mazuri sana lakini yote yanajenga Upole na huruma kwa kiongozi kitu ambacho hakiwezi kuondoa adha yetu. Na Kikwete anaonekana mbovu kwa sababu anajaribu kuwaridhisha wananchi wenye hulka ya ubadhilifu, ndio maana kodi yetu hukusanywa kabla mtu hajafanya biashara! Uliona wapi mkuu wangu ati kodi ya mapato inakadiliwa kabla hujafungua biashara. Ukitengeneza bilioni au upate hasara, hiyo kodi yao imeshalipwa kwa mwaka ama miezi sita.
Watu wana majumba (waliyopewa na serikali ya Mkapa) leo wakikodisha kwa dola 3,000 kwa mwezi na hawalipi kodi ya mapato hata ndululu. Nyumba ambazo kwanza zilikuwa za viongozi wa mashirika haya haya tunayoyapigia kelele leo kujenga ama kununua. Tumerudi kuwa wapangaji na ujenzi wa nyumba yoyote mpya tunashtuka kwa thamani ya majumba wanayojengwa!
Tujiulize sisi wenyewe tumeishia wapi kudai majumba yaliyo uzwa na Mkapa? Tumefikia wapi kudai asilimia katika madini, ardhi na mali zetu zinazoibiwa kila siku kwa misaada ya Watanzania wenyewe. Kila Waziri ana share katika mashirika yote makubwa yanayoendesha uchumi wa nchi. Kila mwalimu ana shule yake, kila daktari ana zahanati yake, kila mtaalam ana kitengo chake private cha kazi nje ya ajira yake. Na hakuna kazi isiyokuwa na malipo hata iwe kupatia TIN namba kwa makusanyo ya kodi ya serikali, yaani mtu ananyimwa namba ya kujisajiri kulipa kodi hadi atoe kidogo. Utamwongoza kondoo zizini kama Kondoo na sii kama mbuzi!
Jamani mwee... acheni jamani msifanye mchezo!"