econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Rais kanikatisha tamaa Sana. Kwenye hotuba yake ya leo hajatoa suluhisho la kudumu kuhusu utekaji. Yeye kajikita kwenye kuwatisha mabalozi na chama Cha CHADEMA kwamba anawafuatilia kila kikao wanachofanya .
Kwa kifupi Rais hajashughulika na kiini Cha tatizo Bali amejikita kwenye matokeo. Yani anazunguka mbuyu baadala ya kuukata. Yeye hasira zake na muda wake amemalizia kuwakemea mabalozi na kuwatisha CHADEMA.
Pia ameonesha dharau kwenye tukio la juzi kwa kusema kifo Cha Ally Kibao ni Cha kawaida Kama vifo vingine. Ni kama anajaribu kutetea jinsi mauaji yalivyo fanyika. Maana jinsi alivyotekwa na kuuawa ile haikuwa kawaida.
Nilitegemea Rais kwenye hotuba yake Leo afanye yafuatayo:
1. Akemee matukio ya kutekana na kuuana.
2. Kuliwajibisha jeshi la Polisi kwa kushinda kulinda Raia.
3. Kuwasihi CHADEMA watulie wasubirie matokeo ya kamati ya uchunguzi kuhusu mauaji ya Ally Kibao.
4. Kuagiza mara moja walihusika na unyama ule wakamatwe.
5. Kuunda Tume Maalum kuchunguza mienendo ya Polisi kwenye kuteka na kuua raia.
6. Kuweka wazi taarifa za kiintelijensia kuhusu wanaofanya utekaji na lengo lao
Soma Pia: Rais Dkt. Samia: Nina taarifa ya kikao chao cha Arusha, wanapanga uhalifu, Serikali ya Tanzania haiondoshwi hivyo