Rais atoe tamko waraka wa rasimu ya katiba mpya wa CCM’

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,346
Kuwa watu wachache kujifungia ofisini hapo Lumumba na kutoka na kikaratasi wanachookiita mbadala wa maoni ya mamilioni ya wananchi ni dharau na matusi kwa Watanzania.

Napendekeza mbunge mmoja jasiri wakianza mjadala na magamba wakawa wanajadili rasimu ya Lumumba, aichane mbele ya bunge ili kupeleka ujumbe kwa wananchi kuwa ni lazima mawazo yao yaheshimiwe na mtu au kikundi cha watu...

tamko-564x272.jpg

Rais Jakaya Kikwete

Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Posted Alhamisi,Februari27 2014 saa 24:0 AM

"Hakukuwa na sababu ya kuweka Tume ya Mabadiliko ya Katiba iwapo nao wanakuja na waraka wao, tunatakiwa kuboresha yaliyomo kwenye rasimu ili tuweze kupata Katiba yenye maoni ya watu,"
Dodoma/Iringa/Dar. Waraka unaodaiwa kuandaliwa na CCM kwa ajili kuwaelekeza wajumbe wake kwenye Bunge Maalumu la Katiba kutetea msimamo wa Serikali mbili umepokewa kwa hisia tofauti huku Rais Jakaya Kikwete akitakiwa kujitokeza hadharani kueleza msimamo wake.

Waraka huo uliibuliwa na gazeti hili jana ukibainisha sura ya Serikali mbili inayotakiwa na CCM, likiwamo pendekezo la kuanzisha Baraza la Wawakilishi la Tanzania Bara.
Miongoni mwa waliozungumzia waraka huo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa ambaye amemtaka Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kutoka hadharani na kuweka wazi msimamo wake kuhusiana na mchakato wa Katiba Mpya.

Dk Slaa alieleza kushangazwa kwake na hatua ya CCM kuandika waraka aliodai umebadili vipengele vyote muhimu katika Rasimu ya Pili ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya kukusanya maoni kwa wananchi.

Pia amemtaka Rais Kikwete kutozindua Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kwa madai kwamba kiutaratibu, linajitegemea na hata katika historia ya Katiba zilizowahi kuandikwa hazijawahi kusainiwa na rais.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea ubunge katika Jimbo la Kalenga, Iringa kupitia Chadema, Grace Tendega uliofanyika katika Kijiji cha Tanangozi, Kata ya Mseke.

Alisema Rais Kikwete na chama chake wanataka kubadili mambo yote muhimu yaliyoandikwa katika Rasimu ya Pili inayojadiliwa mjini Dodoma, huku akijua kuwa zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania ndiyo waliotoa maoni.
Wengine wauponda
Mjumbe wa Bunge la Katiba, James Mbatia alisema ushawishi katika jambo lolote siyo dhambi, lakini hakutarajia ushawishi huo kufanywa na CCM, tena katika jambo nyeti kama mchakato wa Katiba.

"Kama suala ni Serikali tatu, hayakuwa mapendekezo ya Jaji Warioba, bali ya tume nyingi zilizowahi kuundwa na Serikali inayotokana na chama hicho tawala. Kuna Tume za Jaji Robert Kisanga, Francis Nyalali, William Shelukindo, Amina Salum Ali na sasa Joseph Warioba. Zote hizi zimependekeza Serikali tatu."

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema CCM kutengeneza waraka huo ni sawa na `utekaji nyara' wa maoni ya wananchi na kuweka maoni ya wana CCM katika Katiba Mpya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo-Bisimba alisema kitendo cha CCM kutengeneza waraka wake ni kukwamisha upatikanaji wa Katiba bora.

"Hakukuwa na sababu ya kuweka Tume ya Mabadiliko ya Katiba iwapo nao wanakuja na waraka wao, tunatakiwa kuboresha yaliyomo kwenye rasimu ili tuweze kupata Katiba yenye maoni ya watu," alisema.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Gaudence Mpangala alisema iwapo CCM kimesambaza waraka huo, kinafanya makosa kwa kuendeleza misimamo isiyokuwa na hoja za msingi kwa Watanzania… "CCM kusambaza waraka huo ni dalili mbaya za kuleta machafuko miongoni mwa wajumbe…"

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholas Mgaya alisema hatua ya CCM kusambaza waraka huo ni kutapatapa kwa kuwa yaliyomo hayatawezekana kupitishwa na Watanzania.
Mgaya alisema waraka huo umevunja Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayozuia kusambaza maoni ya makundi katika mchakato huo.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alisema tatizo siyo kuwa na msimamo wa chama kupitia waraka huo, bali kuusambaza… "Sijaupata waraka huo lakini kitendo cha kuusambaza tu kisheria ni makosa, walitakiwa kutumia nafasi na wajumbe wake kupeleka hoja hizo bungeni," alisema Kibamba.

Wabunge CCM wanena

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema katika hali ya kawaida, kila kundi katika jamii lina fikra zake kuhusu mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na haki ya kupendekeza kile ambacho linaona kinafaa kuongezwa au kuondolewa na kwamba kuwa na mtazamo tofauti kuhusu jambo fulani ni kitu ambacho hakizuiliki.

"Binafsi ningependa kupata waraka kutoka kila kundi ili nisome na kujua mawazo mazuri yaliyopendekezwa. Ukipitia ni wazi kuwa utakutana na mambo mazuri tu. Hili ni jambo ambalo lipo wazi kabisa."
Hata hivyo, Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa (CCM) alisema chama hicho hakijagawa rasimu yoyote.
Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla alisema hana hakika iwapo waraka huo umesambazwa kwa wajumbe.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy naye alisema hajauona waraka huo, kauli ambayo iliungwa mkono na Mbunge wa Muleba

Kaskazini, Charles Mwijage.

Jana, gazeti hili lilichapisha taarifa za kuonekana kwa waraka huo, ambao pamoja na mambo mengine, umetoa mapendekezo katika ibara 42 za Rasimu ya Katiba ya Tume na kupangua hoja mbalimbali ikiwamo ya muundo wa muungano huku ikitaka mfumo wa Serikali mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho.
Habari hii imeandikwa na Sharon Sauwa na Fidelis Butahe (Dodoma), Kelvin Matandiko (Dar) na Geofrey Nyang'oro (Iringa).

Chanzo mwananchi .
 
nani ataipeleka bungeni mpaka ichwanweeeeeeeeee, wewe umeshaambiwa ni siri, utaitoa wapi uichane, gongo mbaya, inaaribu maini mpaka ubongo
 
Hiyo "RASIMU" yenyewe ni ya kusadikika, hakuna mwenye ushahidi juu ya uwepo wake!
 
Rasimu ni ya Warioba ni aibu CCM kuwa rasimu yake kwani nayo si ilitoa maoni mbele tume?...sasa rasimu nyingine yatoka wapi? je sheria inaruhusu rasimu kuandaliwa na makundi?....CCM inakwenda na punde itatumia mabavu na hapo ndo watabondwa vibaya kwani risasi haitazuia.....na kama wanasikia na wasikie.
Kuwa watu wachache kujifungia ofisini hapo Lumumba na kutoka na kikaratasi wanachookiita mbadala wa maoni ya mamilioni ya wananchi ni dharau na matusi kwa Watanzania.

Napendekeza mbunge mmoja jasiri wakianza mjadala na magamba wakawa wanajadili rasimu ya Lumumba, aichane mbele ya bunge ili kupeleka ujumbe kwa wananchi kuwa ni lazima mawazo yao yaheshimiwe na mtu au kikundi cha watu...
 
nani ataipeleka bungeni mpaka ichwanweeeeeeeeee, wewe umeshaambiwa ni siri, utaitoa wapi uichane, gongo mbaya, inaaribu maini mpaka ubongo

I can't argue with a stupid. I know you will drag me down your level and beat me with experience. ..
 
Hiyo "RASIMU" yenyewe ni ya kusadikika, hakuna mwenye ushahidi juu ya uwepo wake!

Ipo mkuu....sema imetolewa hard copy. Naamini Wazalendo wanaichapa na siku si nyingi itakuwa hapa.
 
Wachumia tumbo ccm wameamua kumsaliti mwenyekiti wao kwa kuharibu mchakato wa katiba mpya
 
Tunatakiwa Watanzania tufunge na kusali kwa ajili ya ujinga wa Ccm, wanao ona hii nchi ni yao na hakuna wa kuwa ambia kitu, basi huyu Mungu wa kweli tunae mwamini akawaonyeshe kwamba wao sio watawala wa milele wa hii nchi. Mungu akaiangamize Ccm kwa mateso na dharau wanazo zionyesha dhidi yetu.
 
Kinachowasumbua hawa mafisadi ni unafiki, wakiwa kwa wananchi wanadai wanaangalia utaifa zaidi, wakijifungia ndani wana panga namna ya kubakia madarakani na kuendelea kufisidi nchi. ama kweli Tanzania hii miaka kumi tumetwishwa zigo zito sana, tunajuta!
 
Kuwa watu wachache kujifungia ofisini hapo Lumumba na kutoka na kikaratasi wanachookiita mbadala wa maoni ya mamilioni ya wananchi ni dharau na matusi kwa Watanzania.

Napendekeza mbunge mmoja jasiri wakianza mjadala na magamba wakawa wanajadili rasimu ya Lumumba, aichane mbele ya bunge ili kupeleka ujumbe kwa wananchi kuwa ni lazima mawazo yao yaheshimiwe na mtu au kikundi cha watu...
Kama inavyotarajiwa mfumo wa serikali tatu hautapita kwa hiyo sio vibaya kwa kundi linalopendelea serikali mbili kuonesha jinsi ya katiba. Wengi waliopendelea serikali tatu wamejikuta ni maoni ya jazba na baada ya tafakuri wanapendelea serikali mbili. Mfano ni mwenyekiti wa cuf Prof Lipumba ambaye amesema hadharani anapendelea mfumo wa serikali mbili unaokidhi maslahi ya pande zote za muungano.
 
Kwa uthibitisho upi?
 
Hata takwimu za warioba zimepingwa kwamba kiutafiti hazikidhi kuthibitisha watanzania wanataka serikali tatu.

zimepingwa kwa vigezo vipi... vya sheria au vya statistics... wanaopinga walitakaje?
 
[h=1][/h]
tamko-564x272.jpg
Rais Jakaya Kikwete

Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Posted Alhamisi,Februari27 2014 saa 24:0 AM

“Hakukuwa na sababu ya kuweka Tume ya Mabadiliko ya Katiba iwapo nao wanakuja na waraka wao, tunatakiwa kuboresha yaliyomo kwenye rasimu ili tuweze kupata Katiba yenye maoni ya watu,”
Dodoma/Iringa/Dar. Waraka unaodaiwa kuandaliwa na CCM kwa ajili kuwaelekeza wajumbe wake kwenye Bunge Maalumu la Katiba kutetea msimamo wa Serikali mbili umepokewa kwa hisia tofauti huku Rais Jakaya Kikwete akitakiwa kujitokeza hadharani kueleza msimamo wake.

Waraka huo uliibuliwa na gazeti hili jana ukibainisha sura ya Serikali mbili inayotakiwa na CCM, likiwamo pendekezo la kuanzisha Baraza la Wawakilishi la Tanzania Bara.
Miongoni mwa waliozungumzia waraka huo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa ambaye amemtaka Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kutoka hadharani na kuweka wazi msimamo wake kuhusiana na mchakato wa Katiba Mpya.

Dk Slaa alieleza kushangazwa kwake na hatua ya CCM kuandika waraka aliodai umebadili vipengele vyote muhimu katika Rasimu ya Pili ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya kukusanya maoni kwa wananchi.

Pia amemtaka Rais Kikwete kutozindua Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kwa madai kwamba kiutaratibu, linajitegemea na hata katika historia ya Katiba zilizowahi kuandikwa hazijawahi kusainiwa na rais.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea ubunge katika Jimbo la Kalenga, Iringa kupitia Chadema, Grace Tendega uliofanyika katika Kijiji cha Tanangozi, Kata ya Mseke.

Alisema Rais Kikwete na chama chake wanataka kubadili mambo yote muhimu yaliyoandikwa katika Rasimu ya Pili inayojadiliwa mjini Dodoma, huku akijua kuwa zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania ndiyo waliotoa maoni.
Wengine wauponda
Mjumbe wa Bunge la Katiba, James Mbatia alisema ushawishi katika jambo lolote siyo dhambi, lakini hakutarajia ushawishi huo kufanywa na CCM, tena katika jambo nyeti kama mchakato wa Katiba.

“Kama suala ni Serikali tatu, hayakuwa mapendekezo ya Jaji Warioba, bali ya tume nyingi zilizowahi kuundwa na Serikali inayotokana na chama hicho tawala. Kuna Tume za Jaji Robert Kisanga, Francis Nyalali, William Shelukindo, Amina Salum Ali na sasa Joseph Warioba. Zote hizi zimependekeza Serikali tatu.”

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema CCM kutengeneza waraka huo ni sawa na `utekaji nyara’ wa maoni ya wananchi na kuweka maoni ya wana CCM katika Katiba Mpya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo-Bisimba alisema kitendo cha CCM kutengeneza waraka wake ni kukwamisha upatikanaji wa Katiba bora.

“Hakukuwa na sababu ya kuweka Tume ya Mabadiliko ya Katiba iwapo nao wanakuja na waraka wao, tunatakiwa kuboresha yaliyomo kwenye rasimu ili tuweze kupata Katiba yenye maoni ya watu,” alisema.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Gaudence Mpangala alisema iwapo CCM kimesambaza waraka huo, kinafanya makosa kwa kuendeleza misimamo isiyokuwa na hoja za msingi kwa Watanzania… “CCM kusambaza waraka huo ni dalili mbaya za kuleta machafuko miongoni mwa wajumbe…”

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholas Mgaya alisema hatua ya CCM kusambaza waraka huo ni kutapatapa kwa kuwa yaliyomo hayatawezekana kupitishwa na Watanzania.
Mgaya alisema waraka huo umevunja Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayozuia kusambaza maoni ya makundi katika mchakato huo.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alisema tatizo siyo kuwa na msimamo wa chama kupitia waraka huo, bali kuusambaza… “Sijaupata waraka huo lakini kitendo cha kuusambaza tu kisheria ni makosa, walitakiwa kutumia nafasi na wajumbe wake kupeleka hoja hizo bungeni,” alisema Kibamba.

Wabunge CCM wanena

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema katika hali ya kawaida, kila kundi katika jamii lina fikra zake kuhusu mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na haki ya kupendekeza kile ambacho linaona kinafaa kuongezwa au kuondolewa na kwamba kuwa na mtazamo tofauti kuhusu jambo fulani ni kitu ambacho hakizuiliki.

“Binafsi ningependa kupata waraka kutoka kila kundi ili nisome na kujua mawazo mazuri yaliyopendekezwa. Ukipitia ni wazi kuwa utakutana na mambo mazuri tu. Hili ni jambo ambalo lipo wazi kabisa.”
Hata hivyo, Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa (CCM) alisema chama hicho hakijagawa rasimu yoyote.
Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla alisema hana hakika iwapo waraka huo umesambazwa kwa wajumbe.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy naye alisema hajauona waraka huo, kauli ambayo iliungwa mkono na Mbunge wa Muleba

Kaskazini, Charles Mwijage.

Jana, gazeti hili lilichapisha taarifa za kuonekana kwa waraka huo, ambao pamoja na mambo mengine, umetoa mapendekezo katika ibara 42 za Rasimu ya Katiba ya Tume na kupangua hoja mbalimbali ikiwamo ya muundo wa muungano huku ikitaka mfumo wa Serikali mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho.
Habari hii imeandikwa na Sharon Sauwa na Fidelis Butahe (Dodoma), Kelvin Matandiko (Dar) na Geofrey Nyang’oro (Iringa).

Chanzo mwananchi .
 
zimepingwa kwa vigezo vipi... vya sheria au vya statistics... wanaopinga walitakaje?
Katika utafiti kuna kitu inaitwa 'sampling' ili kuhakiki kama una 'sample' wakilishi. Inadaiwa kitakwimu maoni kuhusu idadi ya serikali sio wakilishi.
 
Kuwa watu wachache kujifungia ofisini hapo Lumumba na kutoka na kikaratasi wanachookiita mbadala wa maoni ya mamilioni ya wananchi ni dharau na matusi kwa Watanzania.

Napendekeza mbunge mmoja jasiri wakianza mjadala na magamba wakawa wanajadili rasimu ya Lumumba, aichane mbele ya bunge ili kupeleka ujumbe kwa wananchi kuwa ni lazima mawazo yao yaheshimiwe na mtu au kikundi cha watu...

Is schedule of amendments allowed or not? If not allowed what is that assembly doing?
 
Hata takwimu za warioba zimepingwa kwamba kiutafiti hazikidhi kuthibitisha watanzania wanataka serikali tatu.

Ila takwimu za kwako ndo zimethibitisha kuwa wananchi wanataka serikali2? Maoni hayo ulikusanya lini?!
 
Ama kweli CCM kuna vihio , na kama waraka huu ni wao na huyo Nnauye amekanusha ,siku au ikijulina wazi ni wao <Je anaweza kujiuzulu kwa kuukanusha waraka huo ?

Cha msingi hapa ni hili baraza la wawakilishi ,Je ni la Tanzania Bara au ni la Tanganyika ??? Nimeusoma huo tuliomegewa sijaona TANGANYIKA ikitajwa kunani CCM ? Je kuna nchi inaitwa Tanzania Bara ? Je ni nchi hii ndio ilioungana na ZANZIBAR ?
CCM msifanye watu wajinga na nyie mkajiona werevu nawengine wote ni mapoyoyo ,nikisimama hilo Baraza La Wawakilishi la TANZANIA BARA ,hili litakuwa chini ya serikali gani ? Maana wawakilishi wa Zanzibar ni wa serikali yao ya Zanzibar ,msitwambie mmeunda Nchi inaitwa Tanzania bara. Napumua kidogo !!!
 
Huo ni msimamo wa kila chama hakuna chaa ajabu isipokuwa wewe unaona ajabu
 
Back
Top Bottom