JK ni mbumbu sana, lini highway ikawekwa matuta, huyu jamaa si kila leo anasafili.... Siyo kwenye highway, cha kushangaza huyo waziri ana PhD ya Construction engineering kwa nini ............
Mkuu Kokolo nadhani hapo kidogo naomba nitofautiane nawe maradufu kwa kumuita Mkuu wa Kaya ni MBUMBU.... Angalia kwenye posts zangu zilzopita na utaona kuna logic which may not be what you will like lakini ni facts of life. Pili ukiweza nenda kwenye google au other search engine uangalia maneno [B
]"HIGHWAY"[/B] na
"FREEWAY" kisha usome tena post yako!!!
I regret to say wewe ndio mbumbu!!! Highway nyingi zina Matuta Tanzania... pamoja na Mandela Road... sidhani kuna high way Tanzania kama hiyo... lakini ndio hivyo tena vijana wetu wa chuo kikuu wamekuwa huenda wanagongwa!!!
Mkuu tupo pamoja lakini Mandela ya Jijini sio Highway.... Sana sana ni Major Urban arterial (au ring road) being the major road going around the city!! Zaidi ya hilo tupo pamoja Mkuu!!
kama rais.......haya matuta highway yameua sana, .......sehemu zenye matuta hakuna vibao, na kama ni mgeni wa barabara lazma ulivae, pia hayo matuta hayana reflecting color ambayo inasaidia kuliona hata ukiwa mbali.matuta yenyewe hayana proper dimensions, unakuta tuta kuuubwwa na haliko smooth kabisa na barabara.wangeyatoa tu kwenye highways.
Mkuu tupo pamoja lakini ukiangalia design speed ya barabara zetu zote Tanzania ni 120kmph lakini we restrict them to 80kmph considering the situation.... Issue ya ajali sababu ya tuta mostly ni uzembe wa madereva (pamoja na kwamba matuta hayana reflection & signs - zimeibiwa) kama dereva alikuwa anenda at 80kmph sioni kwa nini gari ipinduke kwenye matuta......!! Hilo la kuyatoa Mkuu ni kitu ambayo haipo, tutapoteza watu wengi sana na uharibifu wa mali kutokana na madereva wanaoendesha mwendo wa kasi, so THE MATUTAS ARE HERE TO STAY!!
Moran na wengine,
Ngoja nianzie.....
Highway designs vary widely.......
Mkuu nice definition lakini naomba uangalie zaidi kwenye Basic definition ya HIGHWAY in conjuction with FREEWAY (ambapo tunapata Autobahns etc
Rais wetu naye ni Kilaza sana; sijui kama kweli an.......
Matuta ya barabarani husababisha barabara kupata shock loads ambazo hufupisha maisha yake. Watu wa Dar wanakumbukua kuwa barabara zote zilizowekewa matuta zimekuwa zinaanza kuharibikwa kwenye matuta haya haya. Kwenye nchi za wenzetu, matuta barabarani ni hadimu sana na yakiwepo huwa yamejengwa kwa staili fulani ambayo hupunguza makali ya shock loads, na vile vile matuta hayo huwekwa katika residential roads tu ambako magari makubwa hayapiti. Na zaidi ya yote matuta hayo huwa ni kwa ajili ya kuwatahadharisha madereva badala ya kuwaadhibu, kwa kawaida huwa yamepakwa rangi inayoonekana kutka mbali wakati wote (usiku na mchana) na kunakuwa na alama mbalimbali kutahadharisha madereva kuwa huko mbele kuna matuta.
Kupunguza ajali kwenye highway zetu inabidi tuache ufisadi ili tujenge barabara za njia mbili mbili; zaidi ya hapo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu tu.
Mkuu Kichuguu hilo la Raisi kuwa kilaza kidogo naomba tutofautiane sana.... Raisi ni kama mkuu wa idara, yey anategemea kupokea maelekezo kutoka kwa washauri wake.... Sasa leo JK anatakiwa awe injinia (when tatizo ni roads), daktari (kwenye afya), mwanasheria nk... hiwezekani.... Huwezi kumuita Mkuu wa kitengo (for this case, nchi) kilaza eti sababuw ashauri wake wamechemsha!!
Asante kwa kukubali kuwa hata nchi za wenzetu matuta yapo tena zaidi kwenye residential areas... Mkuu nilisema huko mbele katika highways zetu zote matuta hayapo porini eti, yapo kwenye maeneo ya miji/vijiji (ukumbuke hii ni Bongo ambapo hatuna bypasses around towns/settlements).... Kuhusu shock loads mkuu hapo hebu rudi kwenye types of loadings expected from multiple axles, we consider that one too.... Nakubaliana nawe kuwa kuna tatizo la design za matuta yetu (standardization nilishaongelea kwenye posts huko nyuma). Swala la alama tumegundua kwamba rangi zinapauka na kufutika with time nasi ni wavivu wa kufanya periodic maintenance, pia kwenye signs kama kawa watu wanaiba.... Solution ilikuwa kuweka what we call "Rumble strips" ambazo zinamfanya dereva achukue tahadghari once anazikanyaga na hivyo kupunguza mwendo!! Hilo la eti kwenye makazi ya watu huko kwa wenzetu inakuwa ngumu kulikubali kama "valid argument" kwani tunajua kuna ujenzi unaweza kutokea, kuna watu wanahama na kuhamia, kuna service trucks nk nina uhakika zinapita hayo maeneo pia - au nimekosea Mkuu!!
Barabara za njia mbili?? Wow, Mkuu kwa sasa tunajitahidi kuweka lami kwenye barabara zetu hilo la kuweka njia mbili nadhani ni a long throw lakini tutafika (long term solution), in the mean time MATUTA lazima yaendelee tu Mkuu!!
Prof. Kichuguu......maneno mazito sana hayo.........mwenye masikio na asikie na aliye na macho aone.......na aliye na utashi atekeleze.
1.kuweka matuta ktk highway ni ku-defeat the purpose ya highway
2.Ndugu Rais.......kama jambo lilifanywa kimakosa haku-justify kosa kuendelea/kuendelezwa...............kuwekwa kwa matuta ktk barabara ulizozitaja haina maana makosa hayo yaendelee...............utakumbuka waziri Magufuli alikuwa ameshaanza kuyaondoa hayo matuta.......kwa kufuata ushauri wa wataalamu
3.kuepusha ajali kwa namna moja (kuweka matuta) kunaweza kuleta ajali kwa namna nyingine.........
4.JK......Kumbuka kuna kitu kinaitwa EEE i.e Engineering, Education and Enforcement.......these must go together to achieve the purpose of many designs...............KINACHOTUSHINDA SIYE ni ENFORCEMENT!........ndio maana unashuhudia maghorofa yanaporomoka na ajali zisizoisha barabarani
To sum up wakuu ni hizi definition kama nilivyosema:
1. A freeway also known as a highway, superhighway, autoroute, autobahn, autopista, autovía, autostrada, dual carriageway, expressway, or motorway is a type of road designed
for safer high-speed operation of motor vehicles through the elimination of at-grade intersections.
2. Highway is a term commonly used to designate major roads intended for travel by the public between
important destinations, such as cities.
Wakuu tusisahau kuwa Engineering ni ku translate zile basic principles za nature into a tool to solve our problems.... Tatizo hapa sio kwamba kwa nini barabara zetu hazlingani na za wenzetu bali ni tunafanya/tumefanya nini kutumia maendeleo ya wenzetu katika kutatua matatizo yetu!! Kwa upande wangu ni kama nilivyosema huko mwanzo, wahusika tumezemba kuangalia chanzo cha ajali na hivyo kupelekea wananchi kupeleka malalamiko yao kwa wale wanaowasikiliza (wanasiasa, akiwemo Raisi). Kwa upande wangu badala ya kusema hatutaki matuta tulitakiwa kukaa chini na kuyaBORESHA matuta yetu ili yaweze kuwa kwenye standard ambayo yatatimiza wajibu husika ambao ni kupunguza spidi za magari kwenye maeneo/makazi ya watu; na kwa wakati huohuo kupunguza uharibifu wa magari, barabara na hata kupunguza kero kwa madereva na hata kupunguza vifo vya so called "Madereva wazembe"
Kunradhi kwa mlolongo mrefu sana lakini imebidi!!!
Naomba kuwakilisha!!