SI KWELI Rais Biya amemteua mtoto wake kuwa makamu wa Rais

SI KWELI Rais Biya amemteua mtoto wake kuwa makamu wa Rais

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1775627940868.png

1775628399349.png

Screenshot 2026-04-08 090946.png

Screenshot 2026-04-08 091207.png
 
Tunachokijua
Paul Biya ni rais wa pili wa Cameroon. Aliingia madarakani tarehe Novemba 06, 1982 kufuatia kujiuzulu kwa rais Ahmadou Ahidjo tarehe Novemba 04.

Madai

Kumekuwapo na taarifa iliyoripotiwa na vyombo mbalimbalivya habari kuwa Rais Biya, amemteua mtoto wake, Franck Emmanuel Biya, kuwa Makamu wa Rais kufuatia kuanzishwa kwa nafasi hiyo ambayo haikuwepo nchini humo tangu mwaka 1972.

Taarifa hiyo inaeleza uamuzi huo unakuja sambamba na mabadiliko ya kikatiba yaliyoipa nafasi ya Makamu wa Rais mamlaka makubwa, ikiwemo kurithi urais moja kwa moja endapo rais aliyepo madarakani atafariki, atajiuzulu au kushindwa kutekeleza majukumu yake. Taarifa hiyo imechapishwa na Nipashe, The Citizen, Mwananchi na ITV.


Je, ni kweli Rais Biya ameteua mtoto wake kuwa makamu wa Rais?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia nyenzo za kidigitali umejiridhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Cameroon linaeleza kuwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni zikidai kuwa Rais Paul Biya amemteua mwanawe, Franck Emmanuel Biya, kuwa Makamu wa Rais, si ya kweli.

Inaelezwa kuwa taarifa hii ilianza kusambaa nchini Nigeria, kisha Ghana, na baadaye kuchukuliwa na baadhi ya kurasa za Facebook nchini Cameroon.

Hadi sasa, Paul Biya hajatangaza rasmi sheria inayounda nafasi ya Makamu wa Rais. Kwa kawaida, Bunge linapopitisha muswada, Rais hulazimika kuutia saini na kuutangaza hadharani ili uwe sheria. Hatua hii bado haijafanyika, hivyo hakuna uteuzi wowote wa Makamu wa Rais kwa sasa.

Zaidi ya hayo, hata kama uteuzi utafanyika baadaye, waraka unaosambazwa mtandaoni ni wa kughushi. Katika mazingira kama haya.

Aidha taarifa ya The Cable imewanukuu Maafisa wa wizara ya mambo ya nje ya Cameroon ambao haijawataja, kwamba wamekanusha taarifa za uteuzi wa Franck Emmanuel Biya katika gazeti la TheCable.

“Tarehe 4 Aprili 2026, Bunge la Cameroon liliipitisha marekebisho ya kikatiba ya kihistoria yanayounda nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri,” wizara ilisema katika taarifa yake kwa TheCable"

“Lakini Makamu wa Rais lazima ateuliwe na Kiongozi wa Taifa kuhakikisha kuendeleza mamlaka.


“Hadi sasa, hakuna mtu aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo.”
​
Kumbe sio kweli !? Samuya alikuwa Tayari Kesha chukua peni na karatasi ili achukue notes 😀
 
Sasa mbona hadi vyombo vikubwa hapa chini zimeingia mkenge?

JF chukueni maua yenu mpo makini sana
 
Back
Top Bottom