peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wamemuondoa kwa nguvu Kaimu Rais wa chama hicho, Dinah Mathaman na kumchagua mjumbe mwingine kuongoza kikao.
---
Rais CWT atolewa kikaoni kwa nguvu
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wamemuondoa kwa nguvu Kaimu Rais wa chama hicho, Dinah Mathaman na kumchagua mjumbe mwingine kuongoza kikao kinachoendelea jijini Dodoma leo Ijumaa Desemba 16, 2022.
Mathaman ametolewa kwa nguvu akisukumwa na wajumbe kisha kumzonga hadi nje ya ukumbi huku wakipiga kelele za kutomtaka kwenye chama hicho.
Hata hivyo, Mwananchi linafahamu kuwa sababu kubwa iliyomfanya kiongozi huyo kutolewa nje kwa nguvu ni uamuzi wake kulazimisha ajenda namba tatu ijadiliwa kama namba saba badala ya kufuata mtiririko.
Chanzo: Mwananchi