Rais Dk. Hussein Ally Mwinyi atuma salamu za pole kwa Rais mstaafu Aman Karume kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume

Rais Dk. Hussein Ally Mwinyi atuma salamu za pole kwa Rais mstaafu Aman Karume kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
10,592
Reaction score
15,404
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Amani Abeid Karume, pamoja na familia, ndugu na jamaa, kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume, aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, kilichotokea leo, tarehe 21 Septemba 2026.

Rais Dkt. Mwinyi amesema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa, akieleza kuwa anaungana na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki cha majonzi.

Amesema Marehemu Mama Fatma Karume amekuwa sehemu muhimu ya historia ya Zanzibar na Tanzania, akiwa mwenza wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar.

Soma Pia: Bi Fatma Karume Afariki dunia

Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu amsamehe na amrehemu Marehemu Mama Fatma Karume na amjaalie makaazi mema Peponi, pamoja na kuipa familia subira katika kipindi hiki kigumu.
Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji'un.

IMG_3404.jpeg
 
Back
Top Bottom