Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Manispaa, Mabaraza ya Miji na Halmashauri za Wilaya za Unguja na Pemba katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ leo Mei 20, 2025.
Miongoni mwa waliopata uteuzi huo ni pamoja na aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, Sabra Issa Machano ambaye ameteuliwa Kuwa Mkurugenzi Baraza la Manispaa ya Magharibi B Unguja, Kabla ya uteuzi Sabra alikuwa ni Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.
Wengine ni Moh'd Simba Hassan ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Magharibi "A", Unguja. Adam Abdulla Makame ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Kaskazini "A", Unguja. Juma Mohamed Juma Mmanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Mji, Wilaya ya Kaskazini "B", Unguja.
Pia, Mwanaisha Alli Said ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Mji, Wilaya ya Kati, Unguja. Mussa Haji Mussa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kusini, Unguja. Shuwena Hamad Ali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa
Baraza la Mji, Wilaya ya Wete, Pemba. Hamad Khatib Saleh ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni, Pemba.
Aidha, Shida Kombo Mohammed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Chake Chake, Pemba. Muumin Abeid Salum ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Mji, Wilaya ya Mkoani, Pemba.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 20 Mei, 2025