Rais Dkt. Magufuli, Waziri Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa Makonda zuieni hii ‘ Harambee ‘ Kubwa lao ya Yanga FC kwani ‘ itatakatisha ‘ Fedha

Rais Dkt. Magufuli, Waziri Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa Makonda zuieni hii ‘ Harambee ‘ Kubwa lao ya Yanga FC kwani ‘ itatakatisha ‘ Fedha

Klabu ya Yanga inategemea Kufanya ‘ Harambee ‘ yake waliyoipa jina na ‘ Kubwa Lao ‘ ikiwa ni njia ya Kujipatia Fedha nyingi za Kufanyia Usajili na Kuendesha Shughuli zote za Klabu ili mradi tu na Wao Yanga wawaige Simba SC japo ‘ Kiuhalisia ‘ uwezo huo hawana.

Viongozi wote niliowataja hapo juu msikubali ‘ Harambee ‘ hii ifanyike kwani huko kutakuwa na ‘ Utakatishaji Pesa ‘ mkubwa mno halafu kutatoa ‘ mwanya ‘ pia kwa ‘ Wauza ‘ Unga wakubwa wan chi hii Kujipenyeza huko kisha wakaharibu huu Mpira wetu ambao tayari sasa Klabu ya Simba inaung’arisha.

Wakatazeni / Wazuieni upesi tafadhalini. Na kama Yanga wanataka Kujipatia Pesa za Kihalali basi walazimisheni ' wawaige ' Simba SC kwa Kuwa na Muwekezaji Mmoja tu na ambaye anajulikana na anatambulika vyema kama ilivyo kwa Mohammed Dewji ila mkiruhusu tu hiyo ' Kubwa Lao Harambee ' ya Yanga Mwezi ujao pale Diamond Jubilee kuna ' Uhuni ' mkubwa utafanyika na Soka la Tanzania litachafuliwa.

Wametenga Viti 1000 vya Watu kuchangia Tsh 50,000/ pia wameweka Viti 100 vya Watu kuchangia Tsh 1,000,000/ na wameweka tena Viti 50 vya Watu kuchangia Tsh 10,000,000/. Kwa Jicho la Tatu la ' Kiuchunguzi ' na kwa hali mbaya ya Uchumi iliyopo nchini Tanzania kwa sasa hapa kunatengenezwa ' Utakatishaji ' Pesa na Watu wajanja wajanja hasa ( Wauza Unga ) na wenye Maslahi mabaya Kiuchumi na Tanzania yetu ' Kujipenyeza ' huko kisha wakaishia Kuharibu mpira wa Tanzania.

Na nawaomba pia hata akina TAKUKURU hadi Watu wa TRA nao pia wasikae mbali na hiyo ' Kubwa Lao Harambee ' yao.

Nawasilisha.
Umekosea huo mstari uliosema hali ngumu ya kiuchumi wakati serikali imetangaza uchumi unakua kwa asilimia 7.6

Bila shaka wewe unatumika na mabeberu...lazima uhojiwe.
 
Hizo pesa zinaweza hata kukusaidia wewe kukupunguzia umaskini maana unakula mlo mmoja kwa siku na unalala kwenye miti gymkana kama kunguru
 
Kaka unafahamika kwamba wew ni Simba kindaki ndaki sasa unapokuja na Mada Kama hizi tunajua Ni chuki binafsi

Weka Ushahidi wako hapa kama Mimi GENTAMYCINE ni mwana Simba SC Mkuu. Nadhani JamiiForums nzima ni Wewe tu pekee ndiyo hadi leo hii hujui kuwa Mimi ni mwana Yanga kabisa na hata katika hiyo Harambee nitachangia Kuku Jogoo Wawili na Bata Mzinga Mmoja kwa Klabu yangu Kubwa ya Yanga ambayo imeshinda Taji kwa mwaka huu wa Pili mfululizo wa Kutoshiriki Michuano yoyote ile ya Kimataifa.
 
Hapana Mkuu najaribu tu kuwa Mzalendo kwa nchi yangu ndiyo maana nimewatahadharisha hao Wakuu tajwa hapo. Halafu usisahau kwamba Mimi GENTAMYCINE ni Yanga Mwenzio Mkuu.
Nilikuwa naheshimu nyuzi zako lakini leo umedhihirisha kuwa wewe ni walewale tu. Ulichoandika wala hakijulikani. Umebwabwaja maneno lakini hujasema hizo hela zinatakatishwa vipi au hao watu unaowaita wauza unga wanafaidika vipi kwa kuichangia yanga. Mimi ni shabiki wa simba lakini nawaunga mkono yanga kwa mipango hii. Ni mipango halali kabisa ya kujipatia kipato kama club.
 
Mimi napendekeza Gentamycine atuombe radhi sisi wafuasi wa nyuzi zake kwa kuleta uzi ambao kwa kweli naweza kuuita pumba kwa leo.
 
N
Klabu ya Yanga inategemea Kufanya ‘ Harambee ‘ yake waliyoipa jina na ‘ Kubwa Lao ‘ ikiwa ni njia ya Kujipatia Fedha nyingi za Kufanyia Usajili na Kuendesha Shughuli zote za Klabu ili mradi tu na Wao Yanga wawaige Simba SC japo ‘ Kiuhalisia ‘ uwezo huo hawana.

Viongozi wote niliowataja hapo juu msikubali ‘ Harambee ‘ hii ifanyike kwani huko kutakuwa na ‘ Utakatishaji Pesa ‘ mkubwa mno halafu kutatoa ‘ mwanya ‘ pia kwa ‘ Wauza ‘ Unga wakubwa wan chi hii Kujipenyeza huko kisha wakaharibu huu Mpira wetu ambao tayari sasa Klabu ya Simba inaung’arisha.

Wakatazeni / Wazuieni upesi tafadhalini. Na kama Yanga wanataka Kujipatia Pesa za Kihalali basi walazimisheni ' wawaige ' Simba SC kwa Kuwa na Muwekezaji Mmoja tu na ambaye anajulikana na anatambulika vyema kama ilivyo kwa Mohammed Dewji ila mkiruhusu tu hiyo ' Kubwa Lao Harambee ' ya Yanga Mwezi ujao pale Diamond Jubilee kuna ' Uhuni ' mkubwa utafanyika na Soka la Tanzania litachafuliwa.

Wametenga Viti 1000 vya Watu kuchangia Tsh 50,000/ pia wameweka Viti 100 vya Watu kuchangia Tsh 1,000,000/ na wameweka tena Viti 50 vya Watu kuchangia Tsh 10,000,000/. Kwa Jicho la Tatu la ' Kiuchunguzi ' na kwa hali mbaya ya Uchumi iliyopo nchini Tanzania kwa sasa hapa kunatengenezwa ' Utakatishaji ' Pesa na Watu wajanja wajanja hasa ( Wauza Unga ) na wenye Maslahi mabaya Kiuchumi na Tanzania yetu ' Kujipenyeza ' huko kisha wakaishia Kuharibu mpira wa Tanzania.

Na nawaomba pia hata akina TAKUKURU hadi Watu wa TRA nao pia wasikae mbali na hiyo ' Kubwa Lao Harambee ' yao.

Nawasilisha.
Ndugu yangu, mtani wangu Gentomycin wala usiwe na wasiwasi. Ninafahamu kuwa unaiombea mema klabu yetu pendwa iwe na mafanikio ila ninakutoa hofu kwani huko bwawani kwetu TRA,PCCB na wengine wapo macho. Ila ninakuhakikishia kuwa mwakani hatutokua omba omba..
 
Na zikishapatikana hizo fedha tutaanza kuibomoa hiyo timu yenu kwa kuwachukua wachezaji wenu wote mnaowategemea kama tulivyofanya kwa Yondani, Kaseja, Okwi, nk. Moo hana uwezo wa kupambana na "matajiri" lukuki wanao isapoti timu ya wananchi.
 
Acha ifanyike tu maana mwisho wa siku ni faida kwa soka ⚽ la Tz ambalo Yanga ni mdau muhimu.
 
I did not expect such awful suggestion from such person wasipokuwa na hela mnawacheka wanataka kuijkwamua ,kelele na huyo Dewji wenu anatakatisha fedha amefanya uwekezaji wapi?
Mwacheni Kenge mkubwa na upayukaji wake, usio na staaa, kila Mara kubwatabwata tu bila mpango.
 
Huu uzi ni wa ' kiboya' sana haufanani na hazi ya aliyeuleta! Moja ya nyuzi za hovyo na dhaifu kuwahi kuandikwa Jamii forums!
 
Utwala wa soka kwa sasa Tanzania unajumuisha wanachama wa SIMBA ambao ni KARIA,KIDAO,NYAMLANI,WAMBURA pamoja na MGUTO halikadhalika waziri wa wizara husika ndiyo maana wanakuwa na jeuri hiyoya kununua mechi na kupanga matokeo
 
Hapana Mkuu najaribu tu kuwa Mzalendo kwa nchi yangu ndiyo maana nimewatahadharisha hao Wakuu tajwa hapo. Halafu usisahau kwamba Mimi GENTAMYCINE ni Yanga Mwenzio Mkuu.
Leo wewe Ni mtanzania mzalendo Tena . Haya muda Ni mchache Mambo Ni mengi
 
Kijeshi hapo unawaacha wafanye hilo tukio, unapandikiza wapelelezi inatia watu nyavuni
 
Back
Top Bottom