Rais Dkt. Samia Aipa Hongera NSSF

Rais Dkt. Samia Aipa Hongera NSSF

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

RAIS DKT. SAMIA AIPA HONGERA NSSF

Na MWANDISHI WETU, Katavi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi kwa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) baada ya kuelezwa mafanikio mbalimbali ambayo NSSF imeyapata katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake.

Pongezi hizo alizitoa tarehe 13 Julai, 2024 wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye kilele cha Wiki ya Wazazi kilichofanyika Mjini Mpanda Mkoani Katavi.Ambapo wafanyakazi wa Jumuiya ya Wazazi ni wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Bi. Lulu Mengele amesema Mfuko unamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia kwa namna alivyofungulia nchi, ambapo wafanyakazi kwenye sekta ya biashara, viwandani ambao ni sekta binafsi kwa ujumla wameongezeka na kuiwezesha NSSF kupata wanachama wengi na michango mingi kutokana na ongezeko hilo la wafanyakazi ambao kimsingi ni wanachama wa NSSF.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tunakupongeza sana na tunakutakia kila la heri kwa kazi kubwa unayoifanya, umefungua fursa mbalimbali ambapo wakati unaingia madarakani mwaka 2021 thamani ya NSSF ilikuwa ni Shilingi Trilioni 4.8 lakini sasa imepanda kwa juhudi kubwa ambazo umefanya tumefikia Trilioni 8.5,” amesema Bi. Mengele.

Amesema NSSF inaendelea kuboresha mifumo yake ya TEHAMA ambapo hivi sasa mwajiri anaweza kumuandikisha na kumchangia mwanachama wake kulekule alipo na pia mwanachama anaweza kuangalia taarifa zake mbalimbali bila ya kulazimika kufika katika ofisi za Mfuko na kuwa hatua hiyo imerahisisha huduma kwa wanachama.

Akizungumzia ushiriki wa NSSF katika Kilele cha Wiki ya Wazazi, Bi. Lulu alimueleza Mhe. Rais Dkt. Samia kuwa Mfuko ulishiriki Maonesho yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi kwa kuwa wafanyakazi wa Jumuiya ya Wazazi ni wanachama wa NSSF kama zilivyo Jumuiya nyingine za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Bi. Lulu amesema wametumia maonesho hayo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wanachama waliotembelea kwenye Banda hilo, matumizi ya mifumo kwa waajiriwa na waajiri wakiwa popote wanaweza wakapata taarifa zao za michango na kuchangia bila kulazimika.

Amesema NSSF inaendelea kufanya vizuri kwa kuweka kipaumbele wanachama.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-07-13 at 23.13.39.mp4
    16.2 MB
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.40.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.40.jpeg
    361 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.41.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.41.jpeg
    361.8 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.43.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.43.jpeg
    327.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.45.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.45.jpeg
    570.9 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.46.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.46.jpeg
    365.2 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.47.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 23.13.47.jpeg
    840.5 KB · Views: 7
Huyu mama Hana kumbukumbu? Juzi akiwa Dar alipomwapisha mkurugenzi mpya alisema wamekula hela za anastaafu, wiki moja baadaye wameshajirekebisha na kufanya vizuri kiasi cha kusifiwa?
 
NSSF INA MRADI MMOJA TU ULIOLETA FAIDA NI SALENDER BRIDGE TU mengine ni porojo za mtu mweusi
 
Hivi Mradi wa maghorofa ya Kigamboni-Mikwambe yamepata wateja,au fedha za wanachama zimezama.
Hawa Jamaa kikokotoo cha 25/33 walianza zamani kabla PSSSF na bunge halijapitisha Sheria iliyolalamikiwa.Lakini wachangiaji kutoka sekta binafsi hawakupata watetezi wengi.
Mwezi June 2024 nilisikia kwenye vyombo vya habari kuwa wizara ya Mambo nje na ushirikiano wae Afrika Mashariki wanataka kujenga ghorafa pacha jijini Nairobi kwa ubia na NSSF,bado NSSF hawajajifunza kuwa uwekezaji wa kwenye Majengo return yake ni ndogo na inachukua muda mrefu.wasirudie makosa ya Mikwambe Kigamboni
 
Back
Top Bottom