Rais Dkt. Samia ampa miezi mitatu Waziri Aweso ahakikishe maji yametoka Mtyangimbole Songea - Ruvuma

Rais Dkt. Samia ampa miezi mitatu Waziri Aweso ahakikishe maji yametoka Mtyangimbole Songea - Ruvuma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

View: https://www.youtube.com/live/Dx_r5P6246s

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akiweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji Mtyangimbole Songea Mkoani Ruvuma, leo tarehe 24 Septemba, 2024, amempa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha maji yanapatikana ndani ya miezi mitatu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng Mwajuma Waziri ni wachapakazi sanana wanafanya kazi nzuri hivyo kuwapa miezi mitatu kuhakikisha maji yanapatikana ndani kwa wakazi wa Mtyangimbole kwani tayari mradi huo umefikia asilimia 50% na wananchi wana matumaini makubwa sana.

Mradi huo uliogharimu kiasi cha Bilion 5.5 na utakaohudumia wananchi zaidi ya elfu kumi na nne umewekewa jiwe la msingi na Mhe Rais Samia leo tarehe 24 Septemba 2024 kwa niaba ya miradi 30 inayoendelea kutekelezwa vijijini Mkoani Ruvuma.

IMG-20240924-WA1191.jpg
IMG-20240924-WA1192.jpg
IMG-20240924-WA1002.jpg
IMG-20240924-WA1190.jpg
IMG-20240924-WA1003.jpg
 
AWEZO HANA UWEZO NI MWIZI MKUBWA NA MSANII WA KUTUMIA MEDIA KUJIPAISHA ILA KIUFUPI HAFAI HATA KUWA DIWANI: CC SA100
 
Angekuwa wachapakazi hapo ulipo ungekuta maji.

Sifa kubwa ni mchapa kazi ameoa wanawake wawili.
 
Wanakaribishwa kwenye mgao wa maji (mabomba kuwa kama mapambo) asilimia kubwa ya watanzania hawana maji hata wengi wana mapambo ya mabomba...
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng Mwajuma Waziri ni wachapakazi sanana wanafanya kazi nzuri hivyo kuwapa miezi mitatu kuhakikisha maji yanapatikana ndani kwa wakazi wa Mtyangimbole kwani tayari mradi huo umefikia asilimia 50% na wananchi wana matumaini makubwa sana.

Mradi huo uliogharimu kiasi cha Bilion 5.5 na utakaohudumia wananchi zaidi ya elfu kumi na nne umewekewa jiwe la msingi na Mhe Rais Samia leo tarehe 24 Septemba 2024 kwa niaba ya miradi 30 inayoendelea kutekelezwa vijijini Mkoani Ruvuma.
Tulioko kwenye sekta hiyo tunamjua vizuri.

Jizi kubwa, mamlaka za maji kaweka watu wake , ndiko ulaji wake unakopitia.
Ni mtaalamu wa kubwabwaja na Mike na media.
Huyu jamaa ni billionea, hongera kwake.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Haya ni maneno ya Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan
Screenshot_20240924-133422_1.jpg
Screenshot_20240924-133329_1.jpg

Kazi iendelee.Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Lipi washike watoto wetu, wanaambiwa wajifunze kiswahili.
Leo tena How are you!
Nasikia kuna mmoja alienda huko wanaita kimataifa kuiwakilisha Tanganyika akakutana na how do you feel, akabaki kubwabwaja ze ze ze health!
 
Tusoma na kuwa na uelewa na lugha mbalimbali za kimataifa ili kuweza kupata hata fursa za kibiashara,ajira,uchumi n.k.
 
Back
Top Bottom