POTOSHI Rais Donald Trump asema kwa yanayoendelea nchini Kenya kama angekuwa Rais wa Kenya angejiuzulu

POTOSHI Rais Donald Trump asema kwa yanayoendelea nchini Kenya kama angekuwa Rais wa Kenya angejiuzulu

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
1754547881353.png
 
Tunachokijua
Donald Trump ni Rais wa 47 wa Marekani ambaye alichaguliwa dhidi ya aliyekuwa makamu wa Rais Kamala Harris mwezi Novemba 2024, na kumfanya kuwa rais aliyechaguliwa kuhudumu mihula miwili isiyofuatana. Rais Trump alianza kutumikia muhula wake wa pili katika ikulu ya White House baada ya kuapishwa tarehe 20 Januari 2025 akihudumu pamoja na Seneta wa Ohio, J.D. Vance, kama Makamu wa Rais.

Mara kadhaa kumekuwepo na video mbalimbali zinazosambazwa mtandaoni zikimuhusisha Rais Trump kuzungumzia kuhusiana na masuala kadhaa kutoka Kenya na Tanzania, ambapo baada ya ufuatiliaji wa kina wa JamiiCheck zilibainika kuwa ni potoshi. Rejea hapa na hapa.

Video iliyochapishwa Facebook kuhusu Rais Trump

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Facebook anayetumia jina la 'Nyandarua Guy' alichapisha video inayomuonesha Rais Donald Trump akisema kwa yanayoendelea nchini Kenya kama angekuwa Rais wa Kenya angejiuzulu.

Je ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search umebaaini kuwa kipande hicho cha video ni sehemu ya hotuba ya kwanza ya Donald Trump ya Julai 18, 2024, baada ya tukio la kupigwa risasi lililotokea katika mkutano wa hadhara Julai 13, 2024 huko Butler, Pennsylvania nchini Marekani alipokuwa mgombea wa Urais.

Aidha kipande cha video kinachosambazwa mtandaoni kimepotoshwa kwa kuwekewa sauti isiyo halisi, kwani Rais Trump hakutoa kauli hiyo kuhusu yanayoendelea Kenya.

Vilevile kifaa cha utambuzi wa maudhui yaliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde kinabainisha kuwa, sauti hiyo kwa asilimia 64.3 imetengenezwa kwa teknolojia hiyo.
screenshot-2025-08-07-165256-png.3435508
Back
Top Bottom