SI KWELI Rais Emmanuel Macron alisema Ulaya haiwezi kutegemea hisia za mtu mwenye umri wa miaka 79 akimrejelea Trump

SI KWELI Rais Emmanuel Macron alisema Ulaya haiwezi kutegemea hisia za mtu mwenye umri wa miaka 79 akimrejelea Trump

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
8.jpg
 
Tunachokijua
Emmanuel Macron ni Rais wa Nane wa Ufaransa.

Baada ya kuanza kwa muhula wa pili wa urais wa Donald Trump nchini Marekani, Emmanuel Macron aliwahimiza viongozi wa Ulaya kuongeza bajeti ya ulinzi ili kupunguza utegemezi wa bara hilo kwa Marekani kwa masuala ya usalama.

Akizungumza na wanajeshi wa Ufaransa tarehe 20 Januari 2025, Macron alionya kwamba Ulaya lazima ijiandae kwa siku zijazo ambapo Marekani inaweza kubadilisha mkazo wake wa kijeshi kwenye maeneo mengine. “Tutafanya nini Ulaya kesho ikiwa mshirika wetu Marekani ataondoa meli zake za kivita kutoka Bahari ya Mediterania? Ikiwa watapeleka ndege zao za kivita kutoka Atlantiki hadi Pasifiki?” alisema.

Madai

Nukuu inayosambaa mtandaoni ikidaiwa kutolewa na Emmanuel Macron, kwamba alisema: “Ulaya haiwezi kutegemea hisia za mtu mwenye umri wa miaka 79.”

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kupitia nyenzo za kidigitali umebaini kwamba nukuu hiyo ni potoshi, kwani Rais Macron hajawahi kusema maneno hayo kama yanavyosambazwa.

Kupitia utafutaji wa maneno muhimu, hakuna chanzo cha kuaminika au rasmi kilichomnukuu Macron akisema maneno hayo.

Macron alisema kwamba Ufaransa haitashiriki katika operesheni yoyote za kufungua njia ya Bahari ya Hormuz, akiepuka kuhusika na kauli zilizotolewa na Donald Trump. Alifafanua kuwa Ufaransa si sehemu ya mzozo na haitahusika katika operesheni za kijeshi katika hali ya sasa.

Apoulizwa kuhusu sababu za Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kushindwa kujiunga na operesheni za kijeshi nchini Iran, Rais wa Marekani Donald Trump alisema kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na Waziri Mkuu wa Ireland Micheál Martin Ikulu ya White House “Atatoka madarakani hivi karibuni, basi tutaona.”​
Back
Top Bottom