RAIS WA UFARANSA ATUA NCHINI KENYA
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amempokea rais wa Ufaransa Emmanuel Macron nchini humo ikiwa ni mara yake ya kwanza kuzuru afrika mashariki.
Rais Uhuru alimkaribisha Macron ikulu na kushuhudia uzinduzi wa gari aina Peugeot 3008 iliyoundwa nchini Kenya.
Akizungumza Ikulu jijini Nairobi, rais Uhuru amesema anataka kutengeneza taifa linalonunua vitu vilivyotengenzwa nchini humo.
‘‘ ningependa kurudia kuwa ni mpango wa serikali kuhamasisha falsafa ya nunua Kenya, Jenga Kenya .
nategemea taifa zima litakuwa likitumia magari yalioundwa hapa nchini pamoja na vifaa vyake’’ alisema Uhuru Kenyatta.
Aidha, ameongeza kuwa anamatumaini ziara ya kihistoria ya Macron nchini humo itazidisha wawekezaji kutoka Ufaransa pamoja na kuongeza watalii kati ya nchi hizo mbili.
Wakati huo huo, Kiongozi huyo wa Ufaransa amealikwa kuhudhulia maadhimisho ya miaka 25 ya mauaji ya kimbali nchini Rwanda ambayo yamepangwa kufanyika
mwezi ujao April 7.
HAPA NDIO UTAJUA NI BORA VITENDO KULIKO MANENO,WENZETU WAMESHAPIGA HATUA KUBWA SANA..sisi huku bongo tunazurura tuu[emoji16]🙄🙄
View attachment 1046039
View attachment 1046040
View attachment 1046041View attachment 1046042
Sent using
Jamii Forums mobile app