PreGE2025 'Rais Hatukudai' Vs 'Kisesa Tunakudai”; Unafiki wa Kisiasa Unaovaa Joho la Ustaarabu Vs Siasa za uwajibishaji

PreGE2025 'Rais Hatukudai' Vs 'Kisesa Tunakudai”; Unafiki wa Kisiasa Unaovaa Joho la Ustaarabu Vs Siasa za uwajibishaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Korogwe.jpg

​
Katika majukwaa mengi ya kisiasa nchini Tanzania, imekuwa kawaida kwa wabunge na viongozi wengine wa kisiasa kutumia kauli kama “Rais hatukudai, bali tunakupongeza” kila wanapopata nafasi ya kuzungumza mbele ya Rais. Mara nyingi, baada ya kusema hivyo, huendelea kueleza matatizo makubwa yanayowakabili wananchi wao kama ukosefu wa maji, barabara mbovu, vituo vya afya visivyo na dawa, au shule zilizochakaa. Huu ni mfano hai wa unafiki wa kisiasa, unaojificha nyuma ya lugha ya pongezi lakini kwa ndani ukijawa na kilio cha madai ya maendeleo.

Unaweza kusoma > Mpina: Rais Samia jimboni Kisesa tunakudai, wanaosema 'hatukudai' fedha zao zihamishiwe Kisesa

Kauli ya Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina “Kisesa tunakudai” imeibua mjadala mpana. Tofauti na wengi wanaozungumza kwa lugha ya kuomba au kumsifia Rais, Mpina aliongea kwa sauti ya madai, akisisitiza kuwa jimbo lake lina haki ya kupata maendeleo na huduma za msingi. Japo alichosema ni kweli na halali kwa mujibu wa Katiba inayomtaka mbunge kuwasemea wananchi wake, alipata lawama na kushambuliwa vikali kwa lugha hiyo, kana kwamba kumkumbusha Rais wajibu wake ni kosa.

Nauliza: Kwanini kusema ukweli kwa lugha ya madai kunachukuliwa kama ukosefu wa adabu, ilhali pongezi zisizowekwa kwenye mizani ya hali halisi hupewa sifa?

Soma > Rais Samia hataki Wabunge wa CCM wanaomchalenji? apaniki baada ya Luhaga Mpina kumwambia ''Kisesa tunakudai''

Ukweli ni kuwa wanasiasa wengi wanaamini kuwa kumfurahisha Rais ni mkakati wa kisiasa wa kujihakikishia uungwaji mkono au kupendelewa. Wanatumia sifa kama kinga ya kisiasa, huku wakificha udhaifu wa serikali katika kuwahudumia wananchi.

Tabia hii inaleta taswira ya viongozi wanaoamini kuwa maendeleo ni hisani kutoka kwa Rais, badala ya haki ya msingi kwa kila Mtanzania. Kauli ya “Rais hatukudai” ni kujisalimisha kwenye mfumo wa utii badala ya uwajibikaji. Ni kujikomba kisiasa, na hatimaye kudumaza uongozi wa ukweli unaotegemea hoja na uhalisia wa matatizo ya wananchi.

Kwa msingi huu, Mpina hakukosea kusema “Kisesa tunakudai”, aliwakilisha sauti ya wananchi wake kwa ujasiri. Kushambuliwa kwake ni kielelezo cha siasa zisizotaka ukweli kusemwa, bali sifa na taswira ya utii.

Kama taifa, tunahitaji viongozi wa aina ya Mpina wanaothubutu kudai haki bila woga, si wale wanaokimbilia sifa huku wananchi wao wakiteseka kimya kimya.
 
Kwani watu wanajielewa na hawa tunao wapa ulaji ndio basi tena, wakishatangazwa brain inaturn upsidedown UBINAFSI UNAANZA KUOTA MPAKA MIAKA MITANO IMALIZIKE NDIO UBINADAMU NA UZALENDO UNARUDI
 
Back
Top Bottom