Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Jana ilikuwa siku njema sana kwangu hii ni baada ya kusikia tamko la serikali kuhusu bei elekezi ya mbolea. Nasema nimekunwa sana Kwa sababu hili lilikuwa aibu kubwa mwaka Jana . Mimi ni mkulima wa mahindi mashamba yapo mkoani Rukwa.
Mwaka Jana nimeshindwa kumudu kabisa bei ya mbolea hekari moja nimekunwa napata hata Tani 3au mbili na nusu lakini kulingana na kushindwa kumudu gharama za mbolea nimejikuta mwaka huu ekari Moja napata Tani Moja tu!
Nasema Asante sana kwako rais na wizara ya kilimo, ombi langu ni kuhusu hii benki ya kilimo inavyoonesha ,Kuna aina ya wakulima wanaopata mikopo kupitia benki hii .na ninahisi Kuna mabwanyenye wanapewa pesa hata mashamba hawana.
Benki ya kilimo ipo kwenye majiji makubwa lakini sio vijijini ambako ndio Kuna walengwa haswaa. Lakini pia Kuna urasimu mkubwa na masharti magumu sana ambayo mkulima wa kawaida hawezi kumudu ,naiomba serikali iwe inafuatilia hao wanaokopeshwa kama kweli ni wakulima.
Nahisi sio wakulima kwa sababu hakuna mkulima anaeenda kuomba mkopo kutoka vijijini na akapewa, wanapeana wenyewe Kwa kujuana ,niombe pia benki hii ifungue matawi vijijini