DOKEZO Rais hili la mbolea umenikuna sana. Nakuomba ifanyieni uchunguzi Benki ya Kilimo, kuna jambo halipo sawa

DOKEZO Rais hili la mbolea umenikuna sana. Nakuomba ifanyieni uchunguzi Benki ya Kilimo, kuna jambo halipo sawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Raisi ana kazi kubwa sana, watu wengi akili hawana kabisa. Walimu walishindwa kueilewa 23.3 ni kwa kina nani.

Naona kabisa wakulima nao wanaandaa lawama bila kuelewa utaratibu utaotumika kupata hiyo mbolea ya ruzuku. Si kila duka la pembejeo litakua na mbolea ya ruzuku. Na Kuna masharti lazima mkulima ayafuate ili kupata hiyo mbolea ya ruzuku.
Jitolee ya urea na dap tu love! Nataka nilime 😔
 
Jitolee ya urea na dap tu love! Nataka nilime [emoji17]
Katika kitu sipendi ni kukuona unapata shida yoyote to yeye wangu. Sio urea na dap tu nipo tayari kukupa mtaji wa kilimo.

Lakini ukiniomba ushauri ntakuambia USITHUBUTU kulima. Kilimo ni zaidi ya betting, kitu pekee ntakushauri ni kuwa middleman(dalali) wa kilimo na hapo ndio pesa ilipo. Naposema dalali namaanisha sio kama wale wa sokoni hapana, namaanisha wale wa kwenda kulalia wakulima na kuja kuuza kwa bei juu.

Nimewekeza hii kitu babati, Dom na Arusha. Acha locals walime, wewe nenda kawalalie
 
Ngoja bas niingie kwenye udalali....nilitaka nijaribu kilimo pia
 
Ngoja bas niingie kwenye udalali....nilitaka nijaribu kilimo pia
Eneo ulilopo wanalima sana nn? Na nini kinanunuliwa sana na wanatoka nje ya eneo lilipo. Mfano upo iringa, nini watu kutoka dar, au sehemu nyingine hufuata sana hapo? Muda mzuri wa kununua ni kipindi Cha mavuno
 
Mbeya,mahindi maharage,mpunga na viaz mviringo vyote Watu wa dar huja kujumua huku
 
Mbeya,mahindi maharage,mpunga na viaz mviringo vyote Watu wa dar huja kujumua huku
Mbona sasa umekaa na utajiri huo? Tena hakuna kitu rahisi kukaa nacho kama mpunga.

Viazi mviringo na maharage mbona napo ni rahisi sana? Hapo unatafuta wanyonge wako interior huko kipindi wanakaribia kuvuna unawalalia, unakuja kuwauza hao wanaotika dar
 
Sawa,Asante nitajitahidi kulifanyia Kaz🤜
 
Jana ilikuwa siku njema sana kwangu hii ni baada ya kusikia tamko la serikali kuhusu bei elekezi ya mbolea. Nasema nimekunwa sana Kwa sababu hili lilikuwa aibu kubwa mwaka Jana . Mimi ni mkulima wa mahindi mashamba yapo mkoani Rukwa.

Mwaka Jana nimeshindwa kumudu kabisa bei ya mbolea hekari moja nimekunwa napata hata Tani 3au mbili na nusu lakini kulingana na kushindwa kumudu gharama za mbolea nimejikuta mwaka huu ekari Moja napata Tani Moja tu!

Nasema Asante sana kwako rais na wizara ya kilimo, ombi langu ni kuhusu hii benki ya kilimo inavyoonesha ,Kuna aina ya wakulima wanaopata mikopo kupitia benki hii .na ninahisi Kuna mabwanyenye wanapewa pesa hata mashamba hawana.

Benki ya kilimo ipo kwenye majiji makubwa lakini sio vijijini ambako ndio Kuna walengwa haswaa. Lakini pia Kuna urasimu mkubwa na masharti magumu sana ambayo mkulima wa kawaida hawezi kumudu ,naiomba serikali iwe inafuatilia hao wanaokopeshwa kama kweli ni wakulima.

Nahisi sio wakulima kwa sababu hakuna mkulima anaeenda kuomba mkopo kutoka vijijini na akapewa, wanapeana wenyewe Kwa kujuana ,niombe pia benki hii ifungue matawi vijijini
Subiri kwanza utekelezaji , usije baadaye ukaanza kulia baada ya kuambiwa usubiri vita ya Ukraine iishe
 
Back
Top Bottom