Rais Hussein Ali Mwinyi akipokea salamu za pole kutoka kwa viongozi na taasisi mbalimbali baada ya kufiwa na Baba yake Hayati Ali Hassan Mwinyi

Nani amefanyia finishing hilo jengo? Hakuona kama anahatarisha usalama wa kiongozi
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole Ikulu Mnazi Mmoja kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Ndomba ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mzinga kwa niaba ya uongozi wa shirika hilo, kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Rais Dk. Mwinyi ameshukuru uongozi wa shirika hilo kwa kuja kumfariji.

📅 19 Machi, 2024.
📍Ikulu, Zanzibar.

 




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wasafi Nasibu Abdul Juma almaarufu Diamond Platinumz na ujumbe wake Ikulu Mnazi Mmoja tarehe 20 Machi 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameushukuru uongozi wa Wasafi kwa kuja kumfariji na kushiriki katika mazishi ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na utayari wao kushiriki kutangaza mazuri yanayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Halikadhalika Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Nassib Abdul amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari na kuvuka malengo ya ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 hususani katika sekta ya elimu.

Vilevile Wasafi wameahidi kuendelea kushirikiana na Rais Dk.Mwinyi na kumuunga mkono kuyatangaza mazuri yote anayotekeleza kwa wananchi wa Zanzibar, pia wamemkabidhi zawadi ya nyimbo maalum kwa ajili ya kazi nzuri alizofanya iliyotungwa na wasanii kutoka Wasafi.
 
Sasa hii nayo ndio nini? Inasaidia nini wananchi? Nyie wala lips wa sinza huwa hamna kazi za kufanya?
 
Hata wale watu waliouawa wakati wa uchaguzi nao wapewe pole
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wasafi Nasibu Abdul Juma almaarufu Diamond Platinumz na ujumbe wake Ikulu Mnazi Mmoja tarehe 20 Machi, 2024.

Aidha Rais Dk. Mwinyi ameushukuru uongozi wa Wasafi kwa kuja kumfariji na kushiriki katika mazishi ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na utayari wao kushiriki kutangaza mazuri yanayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Halikadhalika Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Nassib Abdul amempongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari na kuvuka malengo ya ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025 hususani katika sekta ya elimu.

Vilevile Wasafi wameahidi kuendelea kushirikiana na Rais Dk. Mwinyi na kumuunga mkono kuyatangaza mazuri yote anayotekeleza kwa wananchi wa Zanzibar, pia wamemkabidhi zawadi ya nyimbo maalum kwa ajili ya kazi nzuri alizofanya iliyotungwa na wasanii kutoka Wasafi.

🗓️20 Machi, 2024.
📍Ikulu, Zanzibar.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole nyumbani kwake Ikulu Laibon, Dar es Salaam kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson kufuatia kifo cha Aliyekuwa Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alifariki dunia tarehe: 29 Februari, 2024.
 

Attachments

  • IMG-20240401-WA0001.jpg
    680.4 KB · Views: 1
  • IMG-20240401-WA0002.jpg
    842 KB · Views: 1
  • IMG-20240401-WA0000.jpg
    63.3 KB · Views: 1
  • IMG-20240401-WA0003.jpg
    922.6 KB · Views: 1
Kuna watu pepo zao waliziazia hapa duniani angalia faurniture za hiyo nyumba, carpet vigae, hapo ndo useme ccm haijaleta maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…