Rais Hussein Mwinyi amfukuza Mkandarasi, asitisha Mkataba wake

Huyu nae Kazi yake ni kukurupuka na kulalamika kila siku 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220704-103407.png
    80.4 KB · Views: 3
  • Screenshot_20220704-103435.png
    42.9 KB · Views: 3
Kakamilisha %ngapi? Maana yake hana uwezo wa kifedha. Ukipewa mradi uwe na fedha siyo kila hatua ulipwe ndo ufanyekazi.
Mkandarasi anakopeshwa pesa mwanzo wa mradi tu. Pesa ambayo inarejeshwa kupitia malipo atakayolipwa kwa kazi atakayofanya. Na huu mkopo hapewi mpaka atoe Bond ya benki itakayomhakikishia mwenye mradi kuwa huo mkopo utalipwa.
Baada ya hapo Mkandarasi analipwa kwa kazi aliyofanya na ikakubaliwa kuwa imetimiza kiwango na mshauri. Malipo hayo yanatakiwa yafanywe katika muda fulani. Yakicheleweshwa, mkandarasi anakuwa na haki ya kulipwa riba na kuomba nyongeza ya muda wa kumalizia kazi. Akicheleweshwa zaidi, anakuwa na haki ya kuvunja mkataba.
Kwa sababu hii, malipo ya mkandarasi si fadhila bali ni haki yake. Kumcheleweshea malipo kwa kuamini kuwa atatumia pesa zake kutekeleza mradi ni kutomtendea haki. Mradi unatakiwa kujengwa kwa pesa zilizomo katika mkataba na sio kutoka kwingine.

Amandla...
 
Makandarasi wengi hawajui kutayarisha programu ya kazi. Wanafuata tu maelekezo ya client ili kumridhisha. Unaweza kukuta kuwa huu mradi usingeweza kumalizika ndani ya miezi sita lakini mkandarasi akaahidi kufanya hivyo kwa kuhofia kuukosa mradi.
Aidha, makandarasi hawakagui eneo la mradi ili kujua changamoto zake. Changamoto hizi ni pamoja na upatikanaji wa vifaa na vibarua. Sidhani kama unaweza kupata vibarua kirahisi wa kumwaga zege Zanzibar wakati wa mwezi wa Ramadhani.
Makandarasi hawatoi tahadhari mapema za ucheleweshwaji kutokana na mapungufu ya mshauri ( kuchelewa kupitisha kazi, mapungufu katika michoro, kuchelewesha uandikaji wa certificate ya malipo n.k.), client(kuchelewa kukabidhi eneo la mradi, kuchelewa kupata mkandarasi msaidizi hasa wa umeme, kuchelewesha malipo, kuchelewa kutoa uamuzi wa mambo ya kimkataba n.k).
Matokeo ya haya yote ni mkandarasi kubebeshwa lawama zote, anazostahili na asizostahili.

Amandla...
 

Bila Kumumunya maneno huo mradi PESA ndio tatizo
 
Kakamilisha %ngapi? Maana yake hana uwezo wa kifedha. Ukipewa mradi uwe na fedha siyo kila hatua ulipwe ndo ufanyekazi.
Hiyo ndio akili ndogo ya watu wengi.
Mradi ni wa mwenye Mradi na ndiye anatakiwa kuwa na fedha ya kutosha na kwa wakati kutekeleza fedha.
Ni wale wajinga tu wanaofikiri unaweza kumlipa mkandarasi wakati uupendao, tena kwa kuchelewa , halafu kazi iende mwa kasi aipendayo!
 
Na imani nyingine potofu ni kufikiri unaweza kumfukuza mkandarasi utakavyo. Pamoja na kuwa Rais ametoa agizo lakini mkataba hautasitishwa mpaka pale mwenye mradi ( aliyetajwa kwenye mkataba) amuandikie mkandarasi yq kuvunja mkataba akitoa pia sababu za kuuvunja. Mkandarasi asiporidhishwa na hizo sababu anaweza kuomba arbitration. Kama akiona isiwe shida, atawasilisha madai ya kazi aliyoifanya na gharama nyingine kama zipo ( za kuvunja kambi na kuondoa vifaa vyake vya kufanyia kazi). Hii nayo itakuwa na matatizo kwa sababu anayepaswa kuhakiki hilo deni ni mshauri ambae nae ametimuliwa! Kwa hali hiyo mkandarasi anaweza kwenda Mahakamani na kuweka zuio mpaka atakapolipwa pesa zake.

Aidha, kama mshauri ndie aliyetarisha michoro inabidi kibali chake ili michoro yake iendelee kutumiwa na huyo mshauri mpya unless mkataba wake na mwenye mradi umetoa haki miliki ya michoro kwa mshitiri.
Baada ya kuweka yote haya sawa inatakiwa apatikane mkandarasi mwingine wa kuimalizia kazi. Huyu mkandarasi mpua nae anaweza kudai pesa za kuanza mradi. Aidha, quotation yake inaweza kuwa kubwa kuliko huyo aliyefukuzwa kutokana na vitu kupanda bei na hivyo gharama ya mradi kuongezeka.

Aidha, inaweza kubidi kutafuta ma sub contractor wapya, ambayo nayo itachelewesha mradi.

Kwa kawaida, hatua ya kuvunja mkataba inatakiwa kuwa ya mwisho baada ya juhudi zote za kunusuru mradi kushindikana. Mkandarasi anapochelewesha mradi bila sababu inayoridhishwa anakatwa pesa katika malipo yake mpaka kiwango kilichowekwa katika mkataba kinapofikiwa. Ikifika hapo anafukuzwa.

Haya mambo ya kufanya maamuzi jukwaani yana gharama zake. Uzuri tu ni kuwa makandarasi wengi wazawa wanaogopa kuchukua hatua wanapoonewa kwa kuhofia kuwa watanyimwa kazi nyingine.
Haya mambo ya mikataba yafanywe kwa ueledi na sio siasa.

Amandla...
 
Mkuu umelidadavua vyema ili vilaza na wanasiasa waweze kuelewa kile wanachokifanya na madhara yake.
Huyu mkandarasi aliyefukuzwa mambo kweli hajaishia hapo.
Na ni kweli msimamizi anaweza kukataa michoro yake kutumika baada ya yeye naye kutimuliwa kinyemela.
Raus Mwinyi kanunua tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…