#COVID19 Rais Hussein Mwinyi waombe radhi waliochanjwa Zanzibar, umewakosea sana

#COVID19 Rais Hussein Mwinyi waombe radhi waliochanjwa Zanzibar, umewakosea sana

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Mimi binafsi siipendi CCM kabisa, Ila kuna baadhi ya viongozi kidogo naona wana afadhali mmojawapo ni Hussein Mwinyi.

Raisi Mwinyi ni kiongozi mzuri sana, lakini hii haifanyi yeye kutotenda makosa. Raisi Mwinyi wakati wa kuagiza chanjo ya corona aliwahakikishia Wazanzibar kuwa chanjo wanayoleta ni salama sana hivyo wasiwe na wasiwasi wowote.

Akaenda mbali na kusema wameamua kuagiza chanjo kwa kuwa kuna watu wanahitaji kwenda "hijja", hivyo ni lazima walete chanjo watu wachanje waende hijja.

Alisisitiza sana kuwa kwenda hijja kuna vikwazo kwa wasiochanjwa hivyo chanjo hizi zitafanya Wazanzibar kwenda hijja bila kikwazo. Leo serikali hii hii imetoa taarifa kuwa waliopata chanjo wanapaswa tena kuchanja kwa kuwa chanjo waliochanja mwanzo haitambuliki huko Saudi Arabia.

Haya ni masihara kabisa kwenye afya za watu, ilipaswa kabla ya kuagiza chanjo ilipaswa Serikali ijiridhishe. Leo unawaambia watu warudie kuchanjwa chanjo nyingine tofauti na Sinovac, ikiwa mwanzo ulitumia kigezo cha hijja ili wakubali kupata chanjo.

Haya ni makosa makubwa ambayo Rais umeyafanya, inapaswa uwaombe radhi wote waliopata chanjo.

Kwa kuwa kama chanjo waliyopata haitambuliki sehemu takatifu Kama Makka, je usalama wa hiyo chanjo upo wapi?
 
Afya kwanza maana ndio mtaji #1. Kuna haja gani ukimbilie kuchanjwa ksbb ya hijja?. Ukikosa mwaka mmoja hijja,ukaifanyia nyumbani tu huku ukisikilizia chanjo nzuri kuna ubaya gani?. Ona sasa madudu mliyopigwa nayo.

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Back
Top Bottom