Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hatari snNgumu kumeza.Ati chanjo haitambuliki na Saudi Arabia? This is nonsense.kwa maana hiyo wanaamini haifanyi kazi au si salama.Mbona sasa Gwajima anatiwa hatiani bure? Ina maana chanjo haijawa approved na WHO??
wachanjwe tu hakuna namnaKweli kuchanjwa mara ya pili chanjo ya aina nyingine hapo wanawafanyia utafiti wazanzibar kama kuna effect kwa kuchanja mara mbili.
Afya kwanza maana ndio mtaji #1. Kuna haja gani ukimbilie kuchanjwa ksbb ya hijja?. Ukikosa mwaka mmoja hijja,ukaifanyia nyumbani tu huku ukisikilizia chanjo nzuri kuna ubaya gani?. Ona sasa madudu mliyopigwa nayo.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
Jamaa kanichekesha sana
Nipe maana hijja. Kufupisha ukiniambia ni maombi,basi nyumbani sehemu yenye utulivu MUNGU anakusikia zaidi kuliko sehemu ingine.Hakuna Hijja ya mtu kuifanyia nyumbani kwake katika Sharia ya Uislam.
Mungu anazidi kuwaaibisha.Mimi binafsi siipendi CCM kabisa, Ila kuna baadhi ya viongozi kidogo naona wana afadhali mmojawapo ni Hussein Mwinyi.
Raisi Mwinyi ni kiongozi mzuri sana, lakini hii haifanyi yeye kutotenda makosa. Raisi Mwinyi wakati wa kuagiza chanjo ya corona aliwahakikishia Wazanzibar kuwa chanjo wanayoleta ni salama sana hivyo wasiwe na wasiwasi wowote.
Akaenda mbali na kusema wameamua kuagiza chanjo kwa kuwa kuna watu wanahitaji kwenda "hijja", hivyo ni lazima walete chanjo watu wachanje waende hijja.
Alisisitiza sana kuwa kwenda hijja kuna vikwazo kwa wasiochanjwa hivyo chanjo hizi zitafanya Wazanzibar kwenda hijja bila kikwazo. Leo serikali hii hii imetoa taarifa kuwa waliopata chanjo wanapaswa tena kuchanja kwa kuwa chanjo waliochanja mwanzo haitambuliki huko Saudi Arabia.
Haya ni masihara kabisa kwenye afya za watu, ilipaswa kabla ya kuagiza chanjo ilipaswa Serikali ijiridhishe. Leo unawaambia watu warudie kuchanjwa chanjo nyingine tofauti na Sinovac, ikiwa mwanzo ulitumia kigezo cha hijja ili wakubali kupata chanjo.
Haya ni makosa makubwa ambayo Rais umeyafanya, inapaswa uwaombe radhi wote waliopata chanjo.
Kwa kuwa kama chanjo waliyopata haitambuliki sehemu takatifu Kama Makka, je usalama wa hiyo chanjo upo wapi?
Nileteeni Gwajimaaaa😂😂😂😂😂😂😂chanjo chanjo chaaaanjoooo
WaSaudia ni Mungu?Mungu anazidi kuwaaibisha.