POTOSHI Rais Ibrahim Traore anataka kuifanya kiswahili kuwa lugha rasmi ya taifa la Burkina Faso

POTOSHI Rais Ibrahim Traore anataka kuifanya kiswahili kuwa lugha rasmi ya taifa la Burkina Faso

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Wakuu

====
Ni kweli kuwa Rais wa Burkina Faso anataka kuidhinisha kiswahili kuwa lugha ya taifa badala ya Kifaransa? Msaada Kwa mwenye ukweli wa taarifa hizi??
Swahili Burkina 21 AUg.jpg
 
Tunachokijua
Kila taifa ulimwenguni lina lugha zake ambazo linatumia kwa ajili ya mazungumzo. Lugha zinaweza kupewa hadhi tofauti katika taifa husika kulingana na utaratibu waliojiwekea taifa husika matahalani kunaweza kuwa na lugha ya taifa, lugha ya kazi na lugha rasmi nk.

Madai

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii hivi karibuni wamechapisha tarifa inayodai kuwa Rais wa BurkinaFaso Ibrahim Traore anataka kuiondoa lugha ya kKifaransa kuwa lugha rasmi nabadala yake kukifanya Kiswahili kuwa ndiyo lugha rasmi ili kukuza utamaduni wa Afrika.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa Taarifa hiyo ni Potoshi.

Nchi ya Burkina Faso ilianza mchakato wa kuondoa lugha ya kifransa kuwa lugha rasmi mwaka 2023 hii ikiwa ni katika hatua za sehemu ya utekelezaji wa moja ya dhamira kuu za mpito ambayo inajumuisha kuanzisha mageuzi ya kisiasa, kiutawala na kitaasisi kwa nia ya kuimarisha utamaduni wa kidemokrasia na kuunganisha utawala wa sheria.

Vyanzo mbalimbali vikaripori rasmi kuwa Burkina Faso imeachana na lugha ya kifaransa kama lugha ya Taifa, mathalani chombo cha habari cha RFI kilichapisha taarifa Disemba 7, 2023 ikieleza kuwa Kifaransa si lugha ya Taifa tena nchini Burkina Faso.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kufanya hivyo lugha ya Kifaransa iliachwa kama lugha ya kazi, Africa news waliandika kuwa miongoni mwa mabadiliko yanayofanyika ni

“kuanzishwa kwa lugha za kitaifa kama lugha rasmi badala ya Kifaransa ambacho kinakuwa lugha ya kazi”

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa lugha zilizopewa nafasi ya kuchukua nafasi ya lugha ya Kifaransa ni lugha ya Mooré, Mossi, Dioula na Fula

Hata hivyo hakuna taarifa zozote za hivi karibuni zinazoeleza kuwa lugha ya kiswahili kuwa itaanza kutumika nchini Burkina Faso kama lugha rasmi badala ya kifaransa ili kukuza utamaduni wa Afrika.
Back
Top Bottom