Rais Joe Biden apinga kuomba radhi baada ya kutoa kauli ya kutatanisha kumuhusu Rais Vladimir Putin

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu amesema hataomba radhi baada ya kutamka hivi karibuni kwamba rais wa Russia Vladimir Putin “hawezi kusalia madarakani”, akisisitiza kwamba “alionyesha hasira ya kimaadili”, na sio wito wa kuondoa utawala wa Moscow.

“Watu kama hao sio wa kuongoza nchi, lakini wanaongoza. Licha ya kuwa ni viongozi haimanishi kwamba siwezi kuelezea hasira yangu kuhusu hilo”, Biden aliwambia waandishi wa habari Jumatatu kwenye White House.
Amesema “sikuwa nikieleza mabadiliko ya sera”.

“Jambo la mwisho ambalo siwezi kufanya ni kuingia kwenye vita vya ardhini na vita vya nyuklia na Russia,” Biden amesema, wakati akitupilia mbali hisia kwamba matamshi yake yanaweza kuongeza mivutano juu ya vita nchini Ukraine.

Wakati huo huo, wanajeshi wa Russia wamesitisha harakati za kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, huku wakionekana kulenga tena maeneo ya mashariki mwa Ukraine, kulingana na afisa mwandamizi wa wizara ya ulinzi ya Marekani.

Takriban watu 5,000 wakiwemo zaidi ya watoto 200, waliuawa katika mji wa kusini wa Mariupol, ambao ulishambuliwa vikali kwa mabomu na Russia tangu uvamizi uanze mwezi uliopita, kulingana na afisi ya Meya wa mji huo.

VOA Swahili
 
Biden anaweza kuuawa na CIA ili Kuepusha vita vya nuclear. Anaonekana uzee unamuendea vibaya

Rais wa Marekani hana uamuzi wa peke yake kuanzisha mashambulizi ya nuclear. Anaweza kupayuka anavyotaka lakini hana unilateral control of nuclear launch authority.

Autocrats kama Putin na Kim wana absolute power na uamuzi wa mwisho kwenye silaha za nuclear.
 
Tupo kwenye majadiliano jamani
20220329_110906.jpg
 
Nina uhakika angekuwepo raisi aliyepita wa marekani trump angeingia vitani UKRAINE mzima mzima bila NATO yule ndo angeiharibu Usa kiukweli wananchi wa USA walifanya la maana kumuondoa trump madarakani
Sasa Trump angekuwa ndo Rais Russia asingeingia vitani na Ukraine na uenda NATO Ingekuwa sasahivi inavunjika !

Trump alikuwa na uswahiba na Putin, na Trump wala asingekubali ombi la Ukraine kuwa member wa NATO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ndo mana trump walimuondoa walishamjua akili yake ,kuivunja NATO ni kosa kubwa sana ,wakati USA inafahamu umuhimu wake na faida zake katika maslahi yake ya kiuchumi na kijeshi
 
Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu amesema hataomba radhi baada ya kutamka hivi karibuni kwamba rais wa Russia Vladimir Putin “hawezi kusalia madarakani”, akisisitiza kwamba “alionyesha hasira ya kimaadili”, na sio wito wa kuondoa utawala wa Moscow.

“Watu kama hao sio wa kuongoza nchi, lakini wanaongoza. Licha ya kuwa ni viongozi haimanishi kwamba siwezi kuelezea hasira yangu kuhusu hilo”, Biden aliwambia waandishi wa habari Jumatatu kwenye White House.
Amesema “sikuwa nikieleza mabadiliko ya sera”.

“Jambo la mwisho ambalo siwezi kufanya ni kuingia kwenye vita vya ardhini na vita vya nyuklia na Russia,” Biden amesema, wakati akitupilia mbali hisia kwamba matamshi yake yanaweza kuongeza mivutano juu ya vita nchini Ukraine.

Wakati huo huo, wanajeshi wa Russia wamesitisha harakati za kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, huku wakionekana kulenga tena maeneo ya mashariki mwa Ukraine, kulingana na afisa mwandamizi wa wizara ya ulinzi ya Marekani.

Takriban watu 5,000 wakiwemo zaidi ya watoto 200, waliuawa katika mji wa kusini wa Mariupol, ambao ulishambuliwa vikali kwa mabomu na Russia tangu uvamizi uanze mwezi uliopita, kulingana na afisi ya Meya wa mji huo.

VOA Swahili

Vikosi vya Urusi bado tu havijafika Kyiv!
 
Nina uhakika angekuwepo raisi aliyepita wa marekani trump angeingia vitani UKRAINE mzima mzima bila NATO yule ndo angeiharibu Usa kiukweli wananchi wa USA walifanya la maana kumuondoa trump madarakani
Sidhani.. Trump na Putin walikuwa na kiushkaji flan hivi. Huenda angekuwepo madarakani hata vita ya Ukraine na Urusi isingetokea kipindi chake
 
Putin mgomvi sana

Toka tukiwa nursery aliwahi iba penseli za darasa zima

Jamaa kila asubuhi tulkua tunampelekea vitumbua

Ugomvi wake na zeleznsky ni mambo ya mademu tu kuna kidemu kinaitwa Rose wanakigombea toka la tano
 
Back
Top Bottom