Rais Joe Biden apinga kuomba radhi baada ya kutoa kauli ya kutatanisha kumuhusu Rais Vladimir Putin

Rais Joe Biden apinga kuomba radhi baada ya kutoa kauli ya kutatanisha kumuhusu Rais Vladimir Putin

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu amesema hataomba radhi baada ya kutamka hivi karibuni kwamba rais wa Russia Vladimir Putin “hawezi kusalia madarakani”, akisisitiza kwamba “alionyesha hasira ya kimaadili”, na sio wito wa kuondoa utawala wa Moscow.

“Watu kama hao sio wa kuongoza nchi, lakini wanaongoza. Licha ya kuwa ni viongozi haimanishi kwamba siwezi kuelezea hasira yangu kuhusu hilo”, Biden aliwambia waandishi wa habari Jumatatu kwenye White House.
Amesema “sikuwa nikieleza mabadiliko ya sera”.

“Jambo la mwisho ambalo siwezi kufanya ni kuingia kwenye vita vya ardhini na vita vya nyuklia na Russia,” Biden amesema, wakati akitupilia mbali hisia kwamba matamshi yake yanaweza kuongeza mivutano juu ya vita nchini Ukraine.

Wakati huo huo, wanajeshi wa Russia wamesitisha harakati za kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv, huku wakionekana kulenga tena maeneo ya mashariki mwa Ukraine, kulingana na afisa mwandamizi wa wizara ya ulinzi ya Marekani.

Takriban watu 5,000 wakiwemo zaidi ya watoto 200, waliuawa katika mji wa kusini wa Mariupol, ambao ulishambuliwa vikali kwa mabomu na Russia tangu uvamizi uanze mwezi uliopita, kulingana na afisi ya Meya wa mji huo.

VOA Swahili
Rais wa Ukraine jinga sana
 
Piganeni tu tuje tuwatawale shenz type nyie wazungu,
Ndio mutajua kama feni wenzenu zamani tulikuwa tunaita banka
 
Back
Top Bottom