Please press- UNWATCH thread option immediately for this B's to be put where it belongs are the end of the Kenyan news section
Fun fact
Rwanda is 7bn$ economy
Rwandas budget is 2bn$
Rwandas population is 10mn
Kenya is the Largest FDI investor in Rwanda
And Rwanda has a working airline
Ethiopia is a 55bn$ economy
Ethiopian budget is 14bn$
Ethiopia's population is 99mn
And has a working airline
Kenya's budget is 65bn$
Kenya's budget is 23bn$
Kenya's population is 48mn
And we have a working airline
Nusu ya badjet ya kenya inakwenda kwenye wizi na ufisadi
Yafichuka Sh8 bilioni zilifujwa katika Wizara ya Ugatuzi
Imepakiwa - Thursday, June 23 2016 at 21:24
Kwa Mukhtasari
Zaidi ya Sh8 bilioni zilifujwa katika Wizara ya Ugatuzi na Mipango ya Kitaifa katika mwaka wa kwanza wa utawala wa serikali hii ya Jubilee, Kamati ya Bunge kuhusu Uhasibu wa Pesa za Umma (PAC) imebaini.
ZAIDI ya Sh8 bilioni zilifujwa katika Wizara ya Ugatuzi na Mipango ya Kitaifa katika mwaka wa kwanza wa utawala wa serikali hii ya Jubilee, Kamati ya Bunge kuhusu Uhasibu wa Pesa za Umma (PAC) imebaini.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Rarieda Nicolas Gumbo amemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Kerioko Tobiko kuwafungulia mashtaka makatibu wa wizara waliohudumu katika wizara hiyo nyakati hizo.
PAC ilisema kufikia sasa wizara hiyo haiwezi kuelezea jinsi pesa hizo zilivyotumika.
Hii ni kutokana na kisa cha mwaka 2015 ambapo rejista ya mali iliyonunuliwa na wizara hiyo ilionyesha kuwa bei zao ziliongezwa kupita kiasi.
Kwa mfano, ilibainika kuwa runinga moja ya kisasa iliyotumika katika afisi ya aliyekuwa waziri katika Wizara hiyo Bi Anne Waiguru ilinunuliwa kwa Sh1.8 milioni badala ya bei ya kawaida ya Sh100,000.
“Maafisa wakuu katika wizara ya Ugatuzi na Mipaka walishindwa kujibu maswali yaliyoulizwa kuhusu matumizi ya pesa hizo.
Maafisa hao waliongozwa na aliyekuwa Katibu mara tatu lakini kila mara waliomba kupewa muda kutoa maelezo,” PAC inasema kwenye ripoti iliyowasilishwa bunge leo na Bw Gumbo.
Aliyekuwa Katibu katika wizara hiyo wakati huo Dkt Peter Mangiti alifutwa kazi na sasa anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na kupotea kwa Sh791 milioni katika Shirika la Vijana kwa Huduma ya Kitaifa (NYS), kamati hiyo ilisema.
Sasa wabunge watapata fursa ya kuijadili kwa kina ripoti hiyo kabla ya kuipitisha au kuikataa.
Nibora kuwa na kidogo kikatumika vyema