Rais kaonesha udhaifu kwenye eneo la uteuzi

Rais kaonesha udhaifu kwenye eneo la uteuzi

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Sidhani kama Rais alikuwa hana 'info' zozote za wimbi la wateule wake kukimbilia kwenye vyeo vya kisiasa kipindi cha uchaguzi mkuu akajipanga mapema. Teuzi hizi za muda mfupi unamteua leo kesho kutwa unamtengua kwa sababu zozote zile ukiacha kifo, zinanipa wasiwasi kama ana washauri wazuri kwenye eneo hili.

Kwa sisi tuliowahi kuajiriwa na kuajiri, tunaamini kuajiri mfanyakazi au kuteua mtumishi ni 'process', kuajiri sio jambo la kukurupuka, unapoajiri unategemea kukaa naye kwa kipindi kirefu ili uone matunda yake, ukifanya makosa kwenye kuajiri unaweza kuharibu reputation ya kampuni yako uliyoijenga kwa kipindi kirefu.

Teuzi tengua zinazofanywa na Rais hazina afya kwa maendeleo ya taifa letu kwanza zinatia hasara (gharama) kubwa, pili hazimpi mteuliwa nafasi ya kujipanga na kufanya utekelezaji wa mipango yake kwa ufanisi, matokeo yake zinamfanya mteuliwa kuonekana hafai na kuharibu CV yake.

Inaonyesha aidha Rais anateua kwa mapenzi yake tu bila kufuata misingi ya utumishi wa umma au anateua kwa kufuata upepo wa kisiasa.

Ifike mahala sasa watumishi wa umma waliopo kama ma DAS, ma DC, ma RC hata Mawaziri wawe wanapewa muda wa kuamua kujiuzulu nafasi zao ili kugombea nafazi za kisiasa angalau mwaka mmoja kabla ya uchaguzi vinginevyo wabaki na vyeo vyao hadi uchaguzi upite. Huwezi kuwa Waziri wakati huo huo unagombea ubunge ukatekeleza majukumu yako kwa ufanisi na bila upendeleo. Imekuwa vurugu sasa.
 
Wanaokimbilia Ubunge hawana uhakika na uteuzi wao ajira zao zinategemea na mkulu kaamkaje
 
Ndio maana tumeiomba kamati kuu iwafyekelee mbali wale wote waliotuacha mtoni!

Bwasheee kuna mtu katenguliwa hata kabla ya kuapishwa

Naye katia nia au?

Ameteuliwa kuwa RC wa Njombe ijumaa kuchukua nafasi ya Ole sendeka alikua anasubiri kuapa kesho leo katenguliwa kachaguliwa Mtu mwingine toka TANROADS Mwanza

Niulizie kwa Mzee Mgaya😄😄
 
Ni udhaifu mkubwa mno kuteua na kutengua within 2 days kama hakuna aliyefariki kati ya hao wawili. Madhara ya kuipersonalize taasisi ya urais haya. Hizi blunders hatukuwahi kuziona enzi za JK hata kama alikua branded kuwa dhaifu.
 
Bwasheee kuna mtu katenguliwa hata kabla ya kuapishwa

Naye katia nia au??

Ameteuliwa kuwa RC wa Njombe ijumaa kuchukua nafasi ya Ole sendeka alikua anasubiri kuapa kesho leo katenguliwa kachaguliwa Mtu mwingine toka TANROADS Mwanza

Niulizie kwa Mzee Mgaya😄😄
Yule hajatenguliwa ameachwa kukamilisha majukumu ya kitaifa zaidi!
 
Quinine,

Para ya mwisho..."anateua kwa mapenzi yake tu"...ndio maana alishadeclare inategemea atakavyoamka siku hiyo.
 
Kwani kuna habari gani huko
Hivi ndivyo ilivyokuwa mkuu.
IMG-20200719-WA0009.jpg
 
hajaonyesha udhaifu wowote hapo ajira zote serikalini lazima vifanyiwe vetting na kwenye uongozi kuna kitu kinaitwa LMCI ambayo ni muhimu sana kuzingatiwa inaitwa kwa kirefu last minute critical information watu wa TISS wanaweza kukuletea LMCI na huwezi kuidharau kwahiyo unatengua maamuzi yako
 
Tulia wewe ,unafikiri taasisi ya urais ni kijiwe cha kahawa?
 
Rais

hajaonyesha udhaifu wowote hapo ajira zote serikalini lazima vifanyiwe vetting na kwenye uongozi kuna kitu kinaitwa LMCI ambayo ni muhimu sana kuzingatiwa inaitwa kwa kirefu last minute critical information watu wa TISS wanaweza kukuletea LMCI na huwezi kuidharau kwahiyo unatengua maamuzi yako
Sawa, sasa huyo aliyetenguwa siku mbili baada ya uteuzi hao TISS hawakumletea LMCI.
 
Basi wawe wanajiuzulu utumishi wa umma mapema wakagombee ubunge.
Saivi sheria inawaruhusu watangeze nia hata watumishi ambao sio wakisiasa ila wakipitishwa na vyama vyao utumishi wao unakomea hapo hata kama hatashinda uchaguzi
 
Saivi sheria inawaruhusu watangeze nia hata watumishi ambao sio wakisiasa ila wakipitishwa na vyama vyao utumishi wao unakomea hapo hata kama hatashinda uchaguzi
Kama mwaka mzima mkuu wa mkoa anautumia kupanga kugombea unategemea ufanisi hapo, kama vipi kanuni za utumishi zibadilishwe.
 
Kama mwaka mzima mkuu wa mkoa anautumia kupanga kugombea unategemea ufanisi hapo, kama vipi kanuni za utumishi zibadilishwe.
Kama anajipanga mwaka mzima naamini Mkuu atakuwa anajua kupitia RSO/DSO na wengineo wanaompatia taarifa
 
Back
Top Bottom