Hivi, ni kitu gani huyu mshabiki wa simba amefanya, mbona mimi sioni cha ziada sana kuwazidi kina Tenga na wengine.Nimekuwa mkosoaji mkubwa wa TFF kutokana na sababu za waamuzi na upendeleo, lakini mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Karia amefanya na ziada kwenye mpira wetu....
Walianza hivi hivi kwa mwenda zakeMmeshaanza, nitajie rekodi 3 tu alizovunja huyo Karia mpaka ulete hoja ya kuongezewa muda.
Ni vingi sana aloo. Vichache ni udhamani mnono kwa vilabu, Simba kufika robo finali za CAF mara kadhaa mfululizo, Yanga kucheza cheza finali za CAF, timu za taifa kufanikiwa, ligi yetu kuwa Bora Africa, Tanzania ku host mashindano ya CAF, Simba kucheza super cup, nk.Hivi, ni kitu gani huyu mshabiki wa simba amefanya, mbona mimi sioni cha ziada sana kuwazidi kina Tenga na wengine.
Mmeshaanza, nitajie rekodi 3 tu alizovunja huyo Karia mpaka ulete hoja ya kuongezewa muda.
Anaefanya vizuri apongezweNimekuwa mkosoaji mkubwa wa TFF kutokana na sababu za waamuzi na upendeleo, lakini mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Karia amefanya na ziada kwenye mpira wetu. Amevunja rekodi nyingi kwenye tasinia ya mpira ambazo hazitaki maelezo mengi kuyataja.
Kwakuwa amefanya na ziada basi na wadau wa mpira tumtendee na yeye Cha ziada. Tumpe muda zaidi aweze kuikamilisha ndoto yake ya kuiandaa afcon 2027. Yeye ndiye anaejua mganga alipo.
yeye ndio anadhamini kwa pesa yake, yeye ndio anaingia uwanjani kucheza? au nini amefanya specifically? Yeye mshabiki wa simba siku zote huwa anaizunguka yanga ishindwe utasemaje kufanikiwa kwa yanga kumetokana na yeye?Ni vingi sana aloo. Vichache ni udhamani mnono kwa vilabu, Simba kufika robo finali za CAF mara kadhaa mfululizo, Yanga kucheza cheza finali za CAF, timu za taifa kufanikiwa, ligi yetu kuwa Bora Africa, Tanzania ku host mashindano ya CAF, Simba kucheza super cup, nk.
Hata champions league imepata wadhamini na kuonyeshwa live. Wafanyabiashara biashara Wana imani nae, ana mahusiano mazuri na serikali, mpira wa wanawake Leo hii uko mawinguni.
Usisahau kuwa ni Karia aliyeruhusu Yanga na timu nyingine ziruhusiwe kusajili wachezaji 12 wa kigeni, maana yake angesema ni wachezaji 3 TU wa kigeni tusingeweza kuwaona Maxi, Aziz, zouzou, aucho, musonda, lomalisa, diara, na Yao uwanjani kwa wakati mmoja kwenye mechi moja wakicheza pamoja. Sasa hivi kwenye mechi za Yanga unaona wazawa 3 TU.yeye ndio anadhamini kwa pesa yake, yeye ndio anaingia uwanjani kucheza? au nini amefanya specifically? Yeye mshabiki wa simba siku zote huwa anaizunguka yanga ishindwe utasemaje kufanikiwa kwa yanga kumetokana na yeye?
Uko sahihi, lakini hii demokrasia ndio chanzo Cha nchi zetu kuvurugika na kubakia nyuma kama hivi. Uingereza waliitawala dunia na wanaendelea kusikika ingawa wao Wana uongozi wa kifalme (no democracy), unataka hutaki mfalme ndio kiongozi wa nchi. Maendeleo ya Rwanda, Uganda na Tanzania Yana tofauti gani kubwa sana ingawa Rwanda na Uganda Wana Marais haohao miaka yote? Je, Tanzania na Kenya tunaobadilisha Marais wetu kila miaka 10 kupita tuna nafuu gani kuliko Uganda na Rwanda? Tuanzie hapo kwanzaMimi nashauri Katiba ya TFF ifuatwe. Kama imeweka ukomo wa mihula miwili, basi ni vyema ukafuatwa. Leodgar Chilla Tenga alikuwa ni rais bora kabisa wa TFF. Lakini muda wake ulipofika, aliondoka kwa hiyari.
Hivyo tuachane na haya mawazo mfu ya kufikiri mtu mmoja ndiyo ana uwezo wa kuongoza kuliko wengine
Wala hakuna mpango wowote, haya ni maoni na maono yangu binafsi. TFF na serikali ya Mama Samia wameanzisha jambo lao la 2027, wamejikomiti kuwa wataandaa mazingira ya mashindano hayo kufanyika Tanzania. Hili ni jambo kubwa sana kisera na kibajeti kulitimiza kwa 100% maana 2027 sio mbali sana. Mfano, unaweza kumchagua Rais wa nchi na rais wa TFF mpya mwenye vipaumbele tofauti na afcon/mpira, hatakubali atenge pesa nyingi hivyo kujenga viwanja na badala akatenga hela nyingi kwenda kuchimba mabwawa ya samaki kila wilaya kama aliyoahidi wakati wa kampeni zake za uchaguzi. Na yule wa TFF akasema kipaumbele ni kujenga academics kwa Soka la vijana, au serikali na TFF wakavirugana. Tumeshaona nchi zikipokwa kuandaa mashindano na kupewa nchi nyingine.Nilijua tu kuna propaganda za tff kuongeza muda.....ngoja tusubiri tuone najua kuna nguvu kubwa huko nyuma kuongeza muda......katiba !! Ngoja tuone
Hujanijibu....hapo umepiga siasaWala hakuna mpango wowote, haya ni maoni na maono yangu binafsi. TFF na serikali ya Mama Samia wameanzisha jambo lao la 2027, wamejikomiti kuwa wataandaa mazingira ya mashindano hayo kufanyika Tanzania. Hili ni jambo kubwa sana kisera na kibajeti kulitimiza kwa 100% maana 2027 sio mbali sana. Mfano, unaweza kumchagua Rais wa nchi na rais wa TFF mpya mwenye vipaumbele tofauti na afcon/mpira, hatakubali atenge pesa nyingi hivyo kujenga viwanja na badala akatenga hela nyingi kwenda kuchimba mabwawa ya samaki kila wilaya kama aliyoahidi wakati wa kampeni zake za uchaguzi. Na yule wa TFF akasema kipaumbele ni kujenga academics kwa Soka la vijana, au serikali na TFF wakavirugana. Tumeshaona nchi zikipokwa kuandaa mashindano na kupewa nchi nyingine.