Rais Kenyatta adokeza kuhusu shule na makanisa kufunguliwa

Rais Kenyatta adokeza kuhusu shule na makanisa kufunguliwa

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
809
Reaction score
729
1591105374818.png

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza Wizara ya Elimu na ile ya Usalama wa Ndani kuharakisha mwongozo na mikakati ya kufungua shule na maeneo ya ibada itakayohakikisha usalama wa wanafunzi walimu na waumini.

Alisema haya huku idadi ya walioambukizwa iliyotolewa jana ikiwa 59 huku watano wakifariki, Nairobi na Mombasa. Jumla ya maambukizi sasa yamefika 2021 na waliokufa ni 69.

Rais alisema kwamba wazazi hasa walio na wanafunzi wanaofanya mitihani mwaka huu wana wasiwasi kuhusu hatima ya watoto wao na mikakati inafaa kufanywa ili kufungua shule kwa utaratibu.

“Ninaagiza wizara ya Elimu kuharakisha na kukamilisha mashauriano yanayoendelea na washikadau yatakayofanikisha shule nchini kuanza kufunguliwa,” alisema.

Rais alisema mwongozo wa kufungua shule unafaa kushirikisha kanuni ambazo shule na taasisi za elimu zitazingatia ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi.
 
Wameanza kumuiga Rais Magufuli
Katika kazi ulopewa ni kwamba uliambiwa uhakikishe kila uzi una kuwa wa kwanza kujibu?
Kuna muda unakuwa na hoja kweli ila sa ingine ni kama kero.

Kila mahali upo alafu unalazimishia tuu iwe kusifu na kuabudu. Hata kama mada haiko hivyo.
 
Wanyarwanda muda wowote wanaweza wakarudi kwenye lockdown sijui kwanini hawawezi hata kumweleza ukweli dikteta Kagame kuwa hii si sawa hata kidogo.
 
Wanyarwanda muda wowote wanaweza wakarudi kwenye lockdown sijui kwanini hawawezi hata kumweleza ukweli dikteta Kagame kuwa hii si sawa hata kidogo.
Kwani walishafungukiwa?
 
Katika kazi ulopewa ni kwamba uliambiwa uhakikishe kila uzi una kuwa wa kwanza kujibu?
Kuna muda unakuwa na hoja kweli ila sa ingine ni kama kero.

Kila mahali upo alafu unalazimishia tuu iwe kusifu na kuabudu. Hata kama mada haiko hivyo.
uko sahihi kabisa...huyo jamaa ni kama anavizia thread yoyote ikianzishwa yeye lazima atupie mapambio ya kusifu, nadhani atakuwa analipwa kulingana na kigezo hicho!.
 
Back
Top Bottom